Nikiwa kama Rais wa Mashabiki 'lia lia' wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana hapa JamiiForums naomba kuwajua Wenzangu tafadhali

Suzuki hakua Rapper lakini mkuu.
Uko sahihi tena kwa 100% Mkuu na Heko.

Hii ni Historia ya Marapa ( Atalaku ) wa Congo DR...

Kihistoria Mwanzilishi Mkuu wa Kurapu ( Atalaku ) katika Nyimbo huko Congo DR ni Hayati Kabasele Yampanya ( Pepe Kalle )

Mbunifu Mkuu wa Kurapu ( Atalaku ) katika Nyimbo huko Congo DR ni Djuna Mombafu ( Bileku Mpasi ) Kijana aliyelelewa vyema kabisa na Hayati Pepe Kalle.

Aliyenogesha Kurapu ( Atalaku ) huko Congo DR ni Yombo Lumbu ( Tutu Calugi ) na huyu ndiyo Mlezi wa Rapa Kipenzi changu Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE ) na pia ndiyo Mwalimu wa Marapa ( Atalakus ) wengi wa Congo DR kwa miaka 15 iliyopita.

Marapa ( Atalakus ) wa Bendi ya Wenge BCBG ya sasa yake JB Mpiana na ile ya Jumla iliyokuwa Wenge Musica BCBG 4 X 4 ( Les Anges Adourables ) walikuwa ( ni hawa Wafuatao.... )

1. Roberto Wunda Enkokota
2. Tutu Calugi ( Yombo Lumbu )
3. Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE )
4. Noah Mukendi ( Kilimanjaro )
5. Faustine Nzinga Yankobo ( CELLULAIRE )
6. Pajo
7. Bin Laden
8. Fusee Degairel

Marapa ( Atalakus ) bora wa Kiujumla kwa Congo DR ( japo wapo Wengi tu ) mpaka ile Congo ya Brazaville ni hawa Wafuatao....

1. Mukeba Kalondji ( Bill Clinton )
2. Rwinga Keps ( Brigade Sabatier )
3. Eyale Kalondji ( KEROZENE )
4. Mozami Muviu ( CELEO )
5. Rwa Davide
6. Mazikou Ghislain ( Kila Mbongo )
7. Arafat Wanya
8. Gesac
9. Kirikou
10. Zaparo Degere
11. Parabolique
12. Mboshi Bola
13. Theo Mbala
 
Nimependa sana madoido yaliyomo kwenye hii Nyuzi. Kwa kweli wewe ni Mnazi wa BCBG.

Mimi ni Mwanaukoo wa Wenge Musica BCBG 4*4 Tout Terrain— Vijana Watanashati wenye mitindo ya kijanja waliokuwa wakipiga kazi nyakati na hali zote, kama Gari yenye uwezo wa kuvuta tairi zote, 4*4. Ndio band ya kwanza kuihusudu Kongo. Hivyo familia zote zilizozaliwa kutokea kwenye familia hiyo ya WMBCBG4*4TT mimi ni shabiki. Wenge El Paris yake Marie Paul, Wenger Ponderation ya Blaise Bula, WMMM ya Werason, Wenge Tonya Tonya ya Dominguez, Le Maquis de Maison Mere yao kina Ferre, Mulopwe na Bill Clinton na hata sasa Les Marquis International ya Ferre. Wanawenge wote wanachokitu cha kipekee ambacho huwezi kipata QLI au kwa Wazekwa, ule u-BCBG. Swagga kwenye style zao za kughani, rumba, mavazi na mavazi. u-BCBG ni alama kwenye muziki wa Kongo.

Mimi sio mshabiki wa Mpiana. Lakini Toka 1990 hadi leo hakuna mwanamuziki mwenye sauti tamu kama Mpiana. Kwanza ni sauti isiyo na mpayuko-imepoa, pia ni ya asili—sio artificial kama ya Koffi. Hii ndio hufanya popote Mpiana anapotia Verse, hufanya verse yake iwe bora zaidi. Kwenye No Comment Shengen huwa nasikiliza na kuirudia verse yake hata mara kumi.

Pili kwenye Show, hakuna mwanamuziki anayemfikia Mpiana. Show zake zina ubora sana kwa maana ya unadhifu wa wachezaji, mpangilio wa safu, na nidhamu ya wanamuziki wake—So much professional, uchaguzi na mtiririko bora wa nyimbo kwenye Show. Nilipata ona video moja, Alain Makaba anasema mwenye maana halisi ya 'Vijana watanashati' ni Mpiana. Hii unaweza liona hata kwenye Matamasha yake. Top notch concerts.

Hizi ndio nyimbo bora kabisa kwangu za Mpiana;

Rhumba;
48 hours gecoco.
Jeannette.
Feux De Amor.
Education; Hii education nilimkubali sana jamaa, kwa sababu ya Topic aliyoigusia humu—Malezi ya watoto. Ametoa somo kubwa sana ya namna gani tunapaswa walea watoto wetu na maisha yetu wazazi yanavyoweza athiri makuzi ya watoto kiafya na kinidhamu.

Sebene;
Titanic—bado hii ndio Sebene bora zaidi kutoka kwa Mpiana.
T.H (Touj Humble—Daima Mnyenyekevu); Kama kawaida Tutu Kaludji kaua.

Nyimbo isiyonichosha ya Wenge BCBG ni Masuwa.
 
Popote pale ulipo Mkuu Salute tu Kwako.
 
Katika vitu niliumia kuhusiana na muziki ni kuvunjika kwa Wenge BCBG. kuna mashine kali kama Likala Moto Suprise Kapangala Wille mutu. Na ili ya kwanza kabla ya kutoa Pentagon kuna wanaume walifanya kazi Allain Makaba, Didier Masela kuna akina Ali Mponda huyu nasikia ni kichaa alikuwa anapiga konga. Noel Ngaima Makanda na sauti yake ya NINGA.
 
Uko sahihi tena kwa 100% Mkuu na Heko.

Hii ni Historia ya Marapa ( Atalaku ) wa Congo DR...

Kihistoria Mwanzilishi Mkuu wa Kurapu ( Atalaku ) katika Nyimbo huko Congo DR ni Hayati Kabasele Yampanya ( Pepe Kalle )

Mbunifu Mkuu wa Kurapu ( Atalaku ) katika Nyimbo huko Congo DR ni Djuna Mombafu ( Bileku Mpasi ) Kijana aliyelelewa vyema kabisa na Hayati Pepe Kalle.

Aliyenogesha Kurapu ( Atalaku ) huko Congo DR ni Yombo Lumbu ( Tutu Calugi ) na huyu ndiyo Mlezi wa Rapa Kipenzi changu Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE ) na pia ndiyo Mwalimu wa Marapa ( Atalakus ) wengi wa Congo DR kwa miaka 15 iliyopita.

Marapa ( Atalakus ) wa Bendi ya Wenge BCBG ya sasa yake JB Mpiana na ile ya Jumla iliyokuwa Wenge Musica BCBG 4 X 4 ( Les Anges Adourables ) walikuwa ( ni hawa Wafuatao.... )

1. Roberto Wunda Enkokota
2. Tutu Calugi ( Yombo Lumbu )
3. Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE )
4. Noah Mukendi ( Kilimanjaro )
5. Faustine Nzinga Yankobo ( CELLULAIRE )
6. Pajo
7. Bin Laden
8. Fusee Degairel

Marapa ( Atalakus ) bora wa Kiujumla kwa Congo DR ( japo wapo Wengi tu ) mpaka ile Congo ya Brazaville ni hawa Wafuatao....

1. Mukeba Kalondji ( Bill Clinton )
2. Rwinga Keps ( Brigade Sabatier )
3. Eyale Kalondji ( KEROZENE )
4. Mozami Muviu ( CELEO )
5. Rwa Davide
6. Mazikou Ghislain ( Kila Mbongo )
7. Arafat Wanya
8. Gesac
9. Kirikou
10. Zaparo Degere
Impressive. Asante sana Mkuu! Umenikumbusha mambo mengi sana ya muziki wa Kongo na nyakati za kimaisha.

Hapa namuongezea CNN alligator. Alikuwa akinikosha sana huyu jamaa. Nilikuwa nikimpenda sawa na Tutu kea style yao ya Kughani, hawana kelele. Wanaghani sauti zimetulia. Nyimbo aliyonikosha sana ni Attentant enzi yuko na QLI.

Mwingine ni Mboshi Lipasa. Huyu jamaa kwenye Album za Ultimatum, Droit De Veto na Sanction aliua sana humu. Kwenye concert ya Kora 2001, alinyanyua ukumbi wote.

Shamukwale ya kupesa mbongo |

Yumwale yumwana koso, lela makudile, nakusuka wapi |

Sikiliza Rond Point, Droit De Veto na Sanctions.
 
Uko sahihi tena kwa 100% Mkuu na Heko.

Hii ni Historia ya Marapa ( Atalaku ) wa Congo DR...

Kihistoria Mwanzilishi Mkuu wa Kurapu ( Atalaku ) katika Nyimbo huko Congo DR ni Hayati Kabasele Yampanya ( Pepe Kalle )

Mbunifu Mkuu wa Kurapu ( Atalaku ) katika Nyimbo huko Congo DR ni Djuna Mombafu ( Bileku Mpasi ) Kijana aliyelelewa vyema kabisa na Hayati Pepe Kalle.

Aliyenogesha Kurapu ( Atalaku ) huko Congo DR ni Yombo Lumbu ( Tutu Calugi ) na huyu ndiyo Mlezi wa Rapa Kipenzi changu Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE ) na pia ndiyo Mwalimu wa Marapa ( Atalakus ) wengi wa Congo DR kwa miaka 15 iliyopita.

Marapa ( Atalakus ) wa Bendi ya Wenge BCBG ya sasa yake JB Mpiana na ile ya Jumla iliyokuwa Wenge Musica BCBG 4 X 4 ( Les Anges Adourables ) walikuwa ( ni hawa Wafuatao.... )

1. Roberto Wunda Enkokota
2. Tutu Calugi ( Yombo Lumbu )
3. Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE )
4. Noah Mukendi ( Kilimanjaro )
5. Faustine Nzinga Yankobo ( CELLULAIRE )
6. Pajo
7. Bin Laden
8. Fusee Degairel

Marapa ( Atalakus ) bora wa Kiujumla kwa Congo DR ( japo wapo Wengi tu ) mpaka ile Congo ya Brazaville ni hawa Wafuatao....

1. Mukeba Kalondji ( Bill Clinton )
2. Rwinga Keps ( Brigade Sabatier )
3. Eyale Kalondji ( KEROZENE )
4. Mozami Muviu ( CELEO )
5. Rwa Davide
6. Mazikou Ghislain ( Kila Mbongo )
7. Arafat Wanya
8. Gesac
9. Kirikou
10. Zaparo Degere
Albam bora ya Papa Mopao Boss ya Mboka Koffi Ollomide inaitwa Magie, humo alirap mtu wa kuitwa FIFINA, unawezaje kumuacha katika orodha ya marapa bora kuwahi kutokea zaire?
 
Rapa aliye Tishio kwa sasa ni GENTAMYCINE ( Pitshou Lisimo ) wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana japo hata akina Bill Clinton ( Mukeba Kalondji ) pamoja na Gesac aliyekuwa akirapu kwa Felix Wazekwa kabla hajahamia kwa Koffi Olomide na Bendi yake ya Quarter Latin ambapo alifanya Kazi kubwa katika Album ya Monde Arabe hasa ule Wimbo mtamu wa Respect.

Mkuu unamfahama "Zaparo Deguire" wa Extra musica nouvelle horizon?? Hebu jaribu kuweka sikio lako kwa huyu mwamba
 
Roga Roga Mwenyewe ambaye Jina lake halisi ni Ibambi Ikombi ameanza kujifunza Kupiga Gitaa la Solo wakati Burkinafaso Mbokaliya akiwa 'on Fire' na huyu ni Mwalimu wake katika Fani.

Roga Roga unaweza Kumshindanisha tu Wapiga Gitaa la Solo kama akina Flam Kapaya wa Wenge Maison Mere ya Werrason, Ramazani Fulutuni wa Quarter Latin yake Koffi Olomide, Pitchou Concorde wa Bendi ya Felix Wazekwa na Schevchenko Patou wa Bendi yake JB Mpiana ya Wenge BCBG.

Watu sahihi tu wa Kuwafananisha au Kuwashindanisha na Burkinafaso Mbokaliya katika Upigaji mahiri wa Gitaa la Solo ni Diblo Dibala, Dally Kimoko, Beniko, Cain Madoka, Alain Makaba, Mitre Ficarre Mwamba, Dilu Dilumona na Nene Tchacou.

Hii listi ilipitishwa na magwiji wa mziki hapo DRC na Brazaville, ingawaje huyo namba 7 sio mkongo

1.Diblo Dibala
2.Dally Kimoko
3.Lokassa Ya Mbongo
4.Kimbangu Solo
5.Ngouma Lokito
6.Nene Tchakou
7.Phellipe Ferreira "Saladin"
8.Alain Makaba
9.Roga Roga
10.Sonor Digital
 
IMG_4273.jpg

With Due Respect to "WENGE MUSICA et al" ila hii bendi ya EXTRA MUSICA ndo bendi bora kutokea huo ukanda wa KONGO, na hii ilijidhiirisha kwa kuwa ni Bendi Pekee na Moja tu iliyochukua Tuzo za "KORA AWARDS"

Kwa msio jua "KORA AWARDS" ilikua ni kama ilibyo BET au GRAMMY ya Africa.
 
Albam bora ya Papa Mopao Boss ya Mboka Koffi Ollomide inaitwa Magie, humo alirap mtu wa kuitwa FIFINA, unawezaje kumuacha katika orodha ya marapa bora kuwahi kutokea zaire?
Hakuna Mtu aitwae FIFINA aliyekuwa akirapu ( akighani ) katika huo Wimbo wa Maggie bali aliyeimbwa hapo ni Tajiri ( Pedeshee ) Mmoja aitwae JEANPPY PIPINA ambaye hata JB Mpiana nae hupenda sana Kumuimba katika Nyimbo zake.

Katika hiyo Album ya Maggie Rapa ( Atalaku ) alikuwa ni Parabolique ambaye baadae Vijana waliotoka kwa Koffi Olomide na Kuunda Bendi yao ya Quarter Latin Academia nae alikuwepo na kutengeneza Pacha bora ya Marapa ( Atalakus ) akisaidiana na Mboshi Bola Rapa ( Atalaku ) ambaye alifanya Kazi Kubwa katika Album ya LOI ( ikimaanisha SHERIA ) yake Koffi Olomide.

Ni bahati mbaya niliwasahau Kuwaweka.

Cc: My Next Thirty Years
 
Katika vitu niliumia kuhusiana na muziki ni kuvunjika kwa Wenge BCBG. kuna mashine kali kama Likala Moto Suprise Kapangala Wille mutu. Na ili ya kwanza kabla ya kutoa Pentagon kuna wanaume walifanya kazi Allain Makaba, Didier Masela kuna akina Ali Mponda huyu nasikia ni kichaa alikuwa anapiga konga. Noel Ngaima Makanda na sauti yake ya NINGA.
Rekebisha hapo katika Jina la Ali Mponda na weka Jina sahihi la Ally Mbonda Mkuu.

Kuvunjika kwa Wenge Musica BCBG 4 X 4 ( Les Anges Adourables ) ilikuwa ni Kazi ya Koffi Olomide na Watu wa Serikali mpya iliyokuwa chini ya Hayati Rais Desire Laurent Kabila kwa kile ilichodaiwa kuwa Bendi hii ilikuwa ikifadhiliwa na kupewa Jeuri na aliyekuwa Mtoto Kipenzi wa Hayati Rais Mobutu Seseseko aitwae Jose Kongolo Mibeko ambaye alijiua katika Mto Congo akiwa anatoroka nchi baada ya Kusikia Wanajeshi wa Nyamulenge wameshaichukua nchi Congo DR ( zamani Zaire )

Karibia Nyimbo nyingi za JB Mpiana na Bendi ya Wenge Musica yake ( yao ) ni lazima tu kuna sehemu utasikia akimuimba au wakimuimba huyu Jose Kongolo Mibeko na mwishoni wakiongezea na Jina lake la Utani walilompa la Saddam Hussein ila katika Nyimbo utasikia wanarembesha kwa kusema Sadamisele.

Imetumika Nguvu Kubwa kuiua Wenge.
 
Mkuu unamfahama "Zaparo Deguire" wa Extra musica nouvelle horizon?? Hebu jaribu kuweka sikio lako kwa huyu mwamba
Nadhani kuna mahala nimemtaja katika 'List' ya Marapa bora kwa Congo DR na Congo Brazaville japo sikumuelezea Kiundani.

Anajua Kughani ( Kughani ) ila kwa uwezo mkubwa na Umahiri wa Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE ) bado ana mengi ya Kujifunza Kwake.
 
Hakuna vibao vinavyonikosha vya hawa mabwana kama Feux de I’amour na Masuwa vyote wameimba na Papa Wemba….

Nikiwa nimekaa kiti kirefu nashusha bia nikikumbuka harakati za miaka ya tisini hakika nimezeeka sasa…
 
Hii listi ilipitishwa na magwiji wa mziki hapo DRC na Brazaville, ingawaje huyo namba 7 sio mkongo

1.Diblo Dibala
2.Dally Kimoko
3.Lokassa Ya Mbongo
4.Kimbangu Solo
5.Ngouma Lokito
6.Nene Tchakou
7.Phellipe Ferreira "Saladin"
8.Alain Makaba
9.Roga Roga
10.Sonor Digital
Kuna mahala umekosea kidogo Mkuu kwani Lokassa ya Mbongo kwa Congo DR nzima ndiyo anasifika kuwa ni Baba wa Gitaa la Kati la Rythm na huyo Ngouma Lokito anasifika kuwa Baba wa Gitaa la Kibabe la Bass na wote hawa Kamwe hawajawahi Kupiga Gitaa Kinara la Solo ila kwa hao wengine uko sahihi 100% ni Mahiri wa Solo Guitar na alichowashindia Diblo Dibala ni kimoja tu kuwa Yeye anapiga Gitaa la Nyuzi 32 huku wengine wote wakiishia tu Gitaa la Nyuzi 24 tu.
 
Miaka hiyo biashara ya kusafirisha ngozi kwenda imekolea kwelikweli (Magendo) unapiga pedali la baiskeli kilimeta zaidi 80 kwenda kenya, safari zote zilikuwa usiku.

Enzi hizo Mara ni Mara kwelikweli wanaume wa shoka wamejaa, vijana wa sasa hata kichuri hawakijui pia wamekuwa dhaifu kutwa kulilia mapenzi, hakika miaka imesonga.
 
View attachment 2047072

With Due Respect to "WENGE MUSICA et al" ila hii bendi ya EXTRA MUSICA ndo bendi bora kutokea huo ukanda wa KONGO, na hii ilijidhiirisha kwa kuwa ni Bendi Pekee na Moja tu iliyochukua Tuzo za "KORA AWARDS"

Kwa msio jua "KORA AWARDS" ilikua ni kama ilibyo BET au GRAMMY ya Africa.
Kora Awards zilianza mwaka gani? Na unajuwa mfumo wanaotumia kuwapata washiriki?

Kuifananisha Wenge Musica Bcbg 4 by 4 na Extra Musica ni ukosefu wa adabu na ni kielelezo umeujuwa muziki huu wakati Mkapa anaingia madarakani.

Acha kabisa utachekwa, Extra Musica ni takataka tu mbele ya Wenge iliyokamilika, Albam yao unasikiliza nyimbo ya kwanza mpaka ya mwisho bila kuchoka.
 
Back
Top Bottom