Nikiwa na 1.5-2M naweza pata sound gani kali ya nyumbani ya heshima

Tukiachana na maswala ya mwonekano, huu ushauri wako wa kununua spika na power mixer naona ni bora zaidi
 
Nimekasirika sana na haya ma radio ya mchina, nataka sound ya nzuri ya kijanja yenye kutoka mziki halisi kuanzia vyombo mpaka mkitobwa haja sio wa pwaaa pwaa pwaa

Naombeni mawazo yenu tafadhali ikiwezekana na location..
Mkuu budget kubwa sana unaweza ukajipa homework mwenyewe ukatengeneza hometheatre badala ya kununua pre made.

Unanunua speaker la kulia, kushoto, subwoofer etc.unaweka kutokana na eneo lako.
 
Mkuu budget kubwa sana unaweza ukajipa homework mwenyewe ukatengeneza hometheatre badala ya kununua pre made.

Unanunua speaker la kulia, kushoto, subwoofer etc.unaweka kutokana na eneo lako.
Ishu ni kupata speakers zenye impedance na watts za kumatch na Amp ndio kazi. Inahitaji kuwa mjanja kidogo otherwise uki mis-match unaeza jikuta umekaanga Amp.

All in all customized system zinatoaga sound nzuri zaidi.
 
Tukiachana na maswala ya mwonekano, huu ushauri wako wa kununua spika na power mixer naona ni bora zaidi
Mziki wa fidek hizi spika ndogo za laki 5 ni nzuri sana, kwanza unafanya mziki ndani na nje pia.

Una uhakika wa kukaa na mziki wako kwa miaka hata 10 na zaidi.

Unakuwa na mziki mkubwa saana, kiasi kwamba shughuli yote ya furaha ama msiba utautumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingia instagram, watafute hawa jamaa : electrohub _Kenya, vitu walivyo navyo ni kwa wanaojua na kupenda muziki mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app

Hawa jamaa na mimi niliwaona Instagram then siku moja nikabahatika kutembelea showroom yao, jamaa wana vitu classic hatari.
Wana ma Hi-Fi na ma speakers ya kila aina hela yako tu
 
Hawa jamaa na mimi niliwaona Instagram then siku moja nikabahatika kutembelea showroom yao, jamaa wana vitu classic hatari.
Wana ma Hi-Fi na ma speakers ya kila aina hela yako tu
Jamaa wana vinu vile ambavyo waswahili hatujavizoea..

Mswahili akiweka sea piano lake geto anakuambia hakuna kinu cha kutoa mziki kama hiki..
 
Huo mziki mbona ni kama spika za kuuzia flashi kitaani 🤣🤣🤣🤣
 
Hawa jamaa na mimi niliwaona Instagram then siku moja nikabahatika kutembelea showroom yao, jamaa wana vitu classic hatari.
Wana ma Hi-Fi na ma speakers ya kila aina hela yako tu
Jamaa nilikuwa siwajui ila nmeona leo, wako na ukali wa kila aina kina Polk audio, Denon na Klispch...all high end stuff ila bei zake wataziweza wakazi wa kanda ya Oysterbay na Masaki labda hamna hamna wa Mbezi Beach kidogo watafurukuta.
 
Hiyo pesa inatosha tengeneza mziki wako where hautokuwa disappointed

Nunua car sub la inch 12 hivi kama ni pioneer or jbl or jl audio

Rms ya watts 300 kupanda had 600 ni nyingi sana ...

Sub moja na box lake

Kisha tafuta amp kama ni monoblock unaeza beba cha alpine bei ni nzuri kuliko pioneer ya saizi hiyo hiyo itasukuma tu bass

Kisha tafuta amp 4ch labda ...kisha itaftie speaker kama ni component speaker utafute na coexial pair watts zake altleast zigonge 70w rms

Box zake zipo kibao

Kisha radio na audio processor..na mambo madogo madogo

Result ni zaidi ya vi radio vya ajabu ajabu tena milion mbili haiishi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…