Nikiwa na shida kiukweli hua napata pesa kimaajabu,hii Ni nn?

Nikiwa na shida kiukweli hua napata pesa kimaajabu,hii Ni nn?

Japo siwezi kukumbuka matukio yote au pengine nilikuwa zizingatii but tukio la hivi majuzi limenifikirisha Sana
Niliishiwa pesa aidha kwa kulipa madeni au kwa matumiz yaliyokuwa ya lazima nikabakiwa na sh.2000 tu mfukoni na hiyo ni tarehe 15 December na natakiwa nitoboe mwezi huu,Kila nikiangalia huku na huko sio ntapataje pesa nile mm kibaruani na familia
Kopa kopa hapa na pale jamaa wanalia hawana pesa 1 aliniahidi 20 akanipa ten,mara siku ya pili kuna jamaa nilikuwa namdai kanitoa 60,000 nikapumua,sijakaa sawa mara paa kibaruani wakanipa activity ya kufanya yenye mpunga wa 900k,yaani ndani ya wiki moja ya kutokujua hatima hatimaye maisha yakabadilika ghafla na kuwa mchalo kwenye sikukuu hizi za mwisho wa mwaka
Hili jambo limenitafakarisha aisee nimeyumba na kuunga unga Sana kwa miezi 2 hii kwa sababu ya mambo ya ujenzi lakini sasa nimepumua yaani ndani ya mwezi huu tuu nitakuwa nimepata 2mln Bila kuitarajia
Sasa toka kwenye 2000 Hadi 2,000,000/-...miujiza ipo isee
 
Nikiwa na shida kweli hua napata pesa katika mazingira ya ajabu.....

Mfano nikimsaidia mtu pesa kiasi ambacho nabakiwa Sina hela, utakuta napata pesa kimaajabu.

Toka niko chuo hali hii ilikua inanitokea, ila nilikua najua bahati mbaya baadae nikagundua ni kitu ambacho kipo ndani yangu kiukweli.

Mfano nikinunua kitu kwa hela ambayo ndo iliyobakia katika akiba yangu maranyingi narudishiwa chenji hata Kama sitakiwi kupewa chenji.Mfano naweza to 1000 nikarudishiwa 9000.

Pia Kama Sina hela nikiwa na waza kuhusu Hilo mfano nikiwa katika daladala Mara nyingi konda hanidai,ananiruka,au anaweza nifata na kunipa chenji bila sababu,Hali hii hua inatokea automatically.

Kuna wakati hua nahisi kabisa Kuna tukio la kupokea pesa(ambayo sijaifanyia kazi),hasa nikiwa na shida,na Hali hiyo hutukea muda mfupi baadae.

Alafu wahanga wengi Ni wauza maduka na makonda,mfano Kuna siku nilijisemea kimoyo moyo kabisa "hivi Leo Sina hela huyu konda ataniruka" nilikua nimekaa siti ya nyuma watu wanne

Kilichotokea konda akaja akakusanya nauli kwa wale watatu Mimi akaniacha,baadae akaja na chenji ya 9600,akanipa!Hadi nikastuka.

Au nikiwa na shida ya pesa na nikawa sina inapokaribia siku husika ya kulipa lazima linatokea tukio ambalo litanipa hela ya kutimiza Jambo hilo.

Shida ni kwamba hata nikiwa na hela hua natamani bahati hizo ziendelee kutokea,ila hua hazitokei hata niigize vipi kuwa Nina shida ya hela sipati hizo bahati.

Lazima iwe kweli sina hela na ninashida kiukweli,ndo hua Hali hii inatokea harafu hutokea yenyewe tu.

Nikiwa vizuri sipati bahati Kama hizo kabisa.Hii Ni nn?
Hapo ni kwamba unahongwa na popobawa mdogo mdogo. Ipo siku yaja isiyo na jina. Ni bora ukawa unalala umejipaka baby care kwa maana hutoijua siku wala saa atakapo kuja mhongaji.
 
Napingana na wote wanao sema Ni dhuruma....

Kwa tunao amini uwepo wa Mungu Ni muweza wa yote..

Mungu anaweza aka mn'yangan'ya huyu akampa Yule.....

kwa NJIA yeyote na KWA vyovyote.....

izo ndio NJIA zake Wala sio dhuluma...

sio lazima kapu la dhahabu lishuke toka juu....

MUNGU ndie mpaji na muweza wa yote na ananjia zake.....
 
Hapo ni kwamba unahongwa na popobawa mdogo mdogo. Ipo siku yaja isiyo na jina. Ni bora ukawa unalala umejipaka baby care kwa maana hutoijua siku wala saa atakapo kuja mhongaji.
Mmmh...yeye ndo atapata tabu,na yeye ndo ajage kajipaka hiyo babycare!
 
Hapo ni kwamba unahongwa na popobawa mdogo mdogo. Ipo siku yaja isiyo na jina. Ni bora ukawa unalala umejipaka baby care kwa maana hutoijua siku wala saa atakapo kuja mhongaji.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Napingana na wote wanao sema Ni dhuruma....

Kwa tunao amini uwepo wa Mungu Ni muweza wa yote..

Mungu anaweza aka mn'yangan'ya huyu akampa Yule.....

kwa NJIA yeyote na KWA vyovyote.....

izo ndio NJIA zake Wala sio dhuluma...

sio lazima kapu la dhahabu lishuke toka juu....

MUNGU ndie mpaji na muweza wa yote na ananjia zake.....
Amina!
 
Kuna mjuba anakufatilia anakulipia Kila kitu hizo chenji huwa anasema upewe wewe baada ya kukulipia
Sasa jiandae kuliwa siku moja isiyo na jina maana umekula sana vtu vyake
 
Inatakiwa uendelee kuomba uwe na shida ili uendelee kupokea
 
"Ogopa kutodawaiwa nauli "..ningekua wwe ningelipa....maana ni hatari na nusu kiroho zaid

Kuna kupitiwa kawaida kwa dereva namba 2, sasa alitakiwa kufanya generosity ya kumkumbusha. Huko kumchunia ni kujicategorize kwenye uibaji
 
Nikiwahi kurudisha marakadhaa ila makonda hawasemagi hata Asante,zaidi anakukazia macho kana kwamba umemkosea Hadi Kuna siku abiria walimshangaa konda yani nilimwambia umezidisha chenji akaja akachukua,akarudi mlangoni na hakusema chochote.

Kuna mama mmoja muuza maji,pale ilala,nae kanizidishia Kama 5000,nikaingia na huruma sababu alikua na mtoto mgongoni,nikamwambia mbona umenizidishia,kilicho tokea aliurukia mkono wangu na kunpokonya helA Kama natoroka vile na Asante hakuna...yani kijaribugi kurudisha hua sipati positive feedback!
Kazi yako siyo kungoja shukrani as if wewe ndiye umetendewa wema. Angalia maumivu ambayo ungesababisha kwa upande wa pili. Subiri siku ukipata shoti ya dollars halafu ndipo utaelewa somo. Kuna watu hawaelewagi somo hadi wapukunyuliwe kwa msukosuko. Tenda wema nenda zako.
 
Baba angu mzazi alinifundisha hili Jambo.....
"Mkono unao toa ndio unapokea"

Siku zote mkono wa birika huwa haupati kitu......

Siku zote Ukitoa dhabihu ya kujimaliza kutoka moyoni mungu hawezi kukupungukia.....

Kutokana na tabia hii nyumbani kwetu hakukuwai kupungukiwa wageni....
Mzee wangu alikua Ni mtoaji sanaa alikua anasaidia Sana watu na hajawai pungukiwa kitu.....
Thanks sana
 
Hakika,nakumbuka siku ambayo konda alikuja kanizidishia chenji nikiwa nimekaa siti ya nyuma na wale watu watatu,nilikua nimetokea kumsalimia mwalimu alinifundisha zamani sana,

Nilipo fika kwake basi alikua Ana shida zake nyingi hasa za kifamilia,alinieleza,nikapatwa na huruma.

Nakumbuka mfukoni nilikua na 10000,ambayo nilipewa na kaka angu,kwa ajili ya nauli ya kesho yake kwenda kwenye interview,kutokana na huruma nikampa ile hela yote wakati tunaagana,nikabakiwa na nauli tu ya kunirudisha nyumbani.

Sasa wakati nipo katika gari,ndo akili ikanirudia vizuri nikawa nawaza kesho kwenye interview nitaenda na nauli gani,hela yote nimempa mwalimu?

Wakati nawaza hayo ndo inatokea konda akaniletea Kama 9600,wakati hakunidai nauli na sikumpa hela mm.
Bado hata kama ungeendelea kuwa trustworthy usimdungue konda, huko mbele ya safari ungepata iliyo halali & kiroho safwi
 
Kweli kabisa, mm hii ya kutodaiwa nauli ilikuwa inanitokea sana tu lakin baadae naweza poteza pesa kwenye mazingira ya utata nikaamua niiche hiyo tabia, konda akisahau sasa hivi namkumbusha na mwishowe sipotez pesa tena
This is law of course & blessing --- "curble" ama karma. What goes around, usually comes around.
 
Back
Top Bottom