Nikiwa Rais, kila tukio la jaziba za wananchi kunihusu, Itakuwa sehemu yangu ya kujirudi na siyo kukimbilia kuhukumu, Kikwete kwenye hili namkumbuka

Nikiwa Rais, kila tukio la jaziba za wananchi kunihusu, Itakuwa sehemu yangu ya kujirudi na siyo kukimbilia kuhukumu, Kikwete kwenye hili namkumbuka

Bulelaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1,342
Reaction score
3,247
There are things that happen in society involving any leader, they always have the appearance of bringing laughter to the heart and not being angry and condemning people to jail!

Kuna mfano halisi wa maandamano ambayo yamewahi kutokea kipindi chq uongozi wa Mwalimu Nyerere,

Wanawake waliandamana, kisa, kuliadimika nguo zao za kuvaa!

Ikawa walipoandamana, Mwalimu aliwaruhusu wakafika hadi maeneo ya Ikulu kuonesha hasira zao dhidi yake

Walupofika, Mwalimu alicheka sana, kisha akawaambia, mnaandamana kwa sababu hamna nguo? Je hizo mlizojifunga kiwewe na nyingine mkipepersha juu siyo nguo?

Ninachotaka kusema ni kwamba, Kuwa kiongozi siyo lazima kila mtu umdhibiti mpaka akuheshimu mpaka picha zako azisujudie sisemi kwamba watu waache kuheshimu viongozi wao, laa! Lakini, siyo kweli kabisa nchi yenye watu zaidi ya m60 na ndani yake kuna vichaa, wavuta madawa ya kulevya uliochangiwa na viongozi hao hao kutodhibiti uingizwaji wa vilevya hivyo! kiongozi unalazimika kuwataka waheshimu mpaka zile picha, ni vizuri ila isiwe mpaka kuvutana mpaka kuwapeleka jela

Iwapo ningelikuwa ndiyo mimi wanachoma picha zangu kama kiongozi wao, ningelazimika kuwasikiliza ili kama lipo la mimi kuboresha, basi nifanye hivyo, kama hakuna, basi ni kupuuza, nisingelazimika kuingia kwenye dhambi hizi ndogondogo

Kuna mambo mengi sana wananchi hufanya na kuonekana yanachukiza, lakini ukikaa kwa uzuri, unagundua ni ya kufurahisha na kuuchangamsha moyo!

Embu chukulia mfano, watu wa Kenya siku moja wajikute tu wapo Tanzania, ila kiongozi wao abaki huko huko, vilevile Watanzania wawe upande Kenya na kipngozi wao abakie hapa, halafu vurugu zianze huku Tanzania kama walivyozoea watu wa Kenya, inamaana wote wataishia kupigwa lisasi na ama kupelekwa jela kwa sababu tu wanaandamana kupinga kitu ambacho kama ni nchi kuchelewa kufikia maendeleo, wananchi na nchi yao kwa pamoja watachelewa!

Nadhani kuna mahali tunapaswa kuacha furaha zaidi itawale na watu wawe huru kufanya yale yanayoruhusiwa na katiba na mengine yafanyike tu kwa hekima za viongozi wetu,
 
Back
Top Bottom