Kama umetembelea nchi za Western kwa mara ya kwanza umeshuka uwanja wa ndege kuna beauty flani amazing ambayo ndo mara ya kwanza unaiona na hata kupitia tu picha utaona kabisa wao wana-beauty flani nzuri tu
Hata moja ya sababu inayovutia watu wengi kukimbilia nchi za Western ziko nyingi ikiwemo fursa ila pia uzuri wa zile nchi ni moja ya sababu inayovutia watu wengi kwenda nchi za Western na zilizoendelea
Ukienda na ukikaa mda na ukirudi Tanzania unaposhuka uwanja wa jk Nyerere au KIA aisee macho yanakataa picha unayokutana nayo sio nzuri unakutana na ubaya na sio uzuri
Ukiangalia mechi za mpira wa miguu, mashindano ya tennis, diamond league za nchi zilizoendelea n.k utaona kuna beauty flani hivi ambayo huioni wakati unaangalia mechi za ligi ya Tanzania
Swali sisi tufanyaje ili tuweze kuifanya nchi yetu kuwa nzuri sababu hakuna asiyependa mazingira mazuri kama yale ya nchi za Western
NIKIWA RAIS WA TANZANIA NTAIFANYA MIJI YA TANZANIA KUWA MIZURI KAMA ILIVYO KWA WESTERN COUNTRIES
- Tukihakikisha masterplan I afuate kwa lazima basi baada ya mda miji
- Majengo yakiwa identical yaani yakiwa uniform yaani kukiwa na finish code basi itafanya miji yetu ipendeze-sio sahivi kila mtu anafanya finish code kivyake matokeo yake majengo hayapendezi
- Tukipiga paving zenye ubora wa juu kwa baadhi ya maeneo yote ya mjini basi automatic baada ya mda miji yetu itakuwa mizuri
Hiyo hali ya ubaya ambayo ipo kwenye moja ya mji hapo chini na miji yote ya Tanzania tunaweza iondoa
View attachment 3423014