Ni mara chache sana JF kukuta forum ina discussion kuhusu Hip Hop toka bandiko limewekwa nimesoma kila comment kwa umakini,kuna vitu nimegundua:-
1.Wengi hatuijui Hip Hop kabisa nadhani hata misingi yake hatujui nadhani tunahitaji darasa huru maana tunaamini kwenye utamaduni ambao hatuujui kabisa.
2.Bandiko limekaa vizuri ila uchangiaji uko kishabiki 100% wale wanaompenda Nikki hawataki kuangalia upande wa pili na wale wasiompenda Nikki hawataki kujua mazuri ya Nikki.
3.kuna upande unaoamini kwenye old skool na upande unaoamini kwenye Hip Hop new Era ambayo ni ngumu sana kuigundua hasa wanapofanya midundo flani migumu.
Mtazamo wangu binafsi kuhusu Nikki Mbishi,nimemsikiliza sana joint zake honestly kuna kitu anafanya na hata mwanzo kwenye michango yangu nimesema makosa yake ni nini,bado naamini Nikki hajaacha alama kwenye utamaduni huu hata kama akiondoka sioni sehemu ambayo tutaita pengo maana bado alikua na safari ndefu ya kuji-establish kwenye industry ili awe icon kwanza ili kesho asipokuewepo kwa namna yoyote tuione ile absence yake,Nikki ki-ukweli anapenda kufanya vitu kama America mfn creating stunts(childish one),beef sizizo na msingi,kujikuza na stuff kama izo anaishi ki-50 cent au The Game wakati bado hatujafika uko na mashabiki wamechangia kum-stress dogo akaiona kesho yake kabla hajaifiki.
Kwenye Hip Hop mtu akisanda tu hata kama aliishi kwenye huu utamaduni miaka 100 basi ni MPUUZI maana hauwezi kuacha maisha yako halisi unless alikua anaigiza mwanzoni how come Nikki ana kipaji cha ku-rap then aseme sintoingia studio tena WTF kuna wahuni kibao hawana albamu,hawana muda na media zenu za kibwege wanafanya mixtape kuelimisha mitaa,hawa akina Nikki wanaotaka Hip Hop iwaletee mademu,magari na majumba walikosea sana kuja huku wangeenda kule bongo fleva wakakate mauno,kaka zake wangekua wanalilia kama yeye sidhani angekuta studio kama uyoga na watoto kama yeye wasingetamani kuishi kwenye utamaduni huu,Nikki ni sympathy seeker anachotaka watu wamuombe arudi apate attention kama ambavyo kwenye page yake ya IG anavyofanya kwa ku-screen shot waliosema akina Prof J,Chid etc tuone umuhimu wake anatakiwa akue kuzira akizoe maisha yatambana atamkataa hata Malcom kisa hawafanani ndevu.