mud-oil-chafu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2020
- 587
- 954
Nilikuwa fan wake ...tatzo la mbishi ni usera mavi,kutukana kila mtu,kutukana mashabiki,media, na wasanii ,....**** sana yule dgo....now namskilza dizasta.
Habari za weekend.
Awali ya yote natambua uwezo mkubwa wa baadhi ya members wa jf linapokuja suala zima la music hasa muziki wa kufoka foka(hiphop).Nimekuwa nafuatilia kwa muda sasa katika hili jukwaa la burudani kwaa namna gani wadau wanavyochambua wasanii wa hiphop kuanzia wa hapa nyumbani hadi kule mambele.Wadau wapo ambao wanajuwa hiphop MCs ni mtu wa aina gani.
Katika nyakati fulani kulitokea ubishani ambao si wa kawaida katika muziki wa hiphop hapa Bongo,kwa wakati huo vijana wawili ambao walikuwa wapo hot by that time walikuwa wanalinganishwa,pambanishwa katika uandishi,bars,metaphor na flow kwa ujumla.Vijana hao ni nikki mbishi na nikki wa pili.
Kwa siku ya jana jumamosi ni siku ambayo niliitumia kusikiliza kazi za hawa wawili yaani ngoma kwa ngoma kuanzia ngoma zao za mwanzo mwanzo hadi za hivi karibuni,kusema ile ukweli wale waliokuwa wana mlinganisha nikki mbishi na nikki wa pili naomba wamuombe radhi mbishi.Jamaa ni mwandishi bora kwa wakati wote ana flow vizuri sana.
Kusema ile ukweli hawakumtendea haki mbishi na alidharauliwa sana.
Karibuni tuseme ukweli kabla hajatangulia mbele za haki.