Nikki wa Pili ayape heshima mavazi ya kitaaluma. Achague kuwa PhD holder ama abaki na swagger zake za kisela

Hizo Poor Hair Distribution huwa zinarithiwa au nunuliwa???

Endeleeni kununua tu......
 

Una PhD?
 
Kama issue ni usomi na maadili,ukiaaanza na Nikki wa pili utakuwa umemuonea saana...Naomba uanze kwa Maprofesa wetu kadhaa ambao kimaadili wameudhalilisha mno usomi.
 
Umekariri?

Phd holder ni ndani ya kichwa na sio muonekano wa mavazi
 
Wivu wa kimasikini acha kijiba cha roho mie napenda aendelee ili ilete ushawishi wasanii wetu warudi shule Mana wengi wao ni std7 na form 4
 
Hahaha bro kabla hujaanza kukosoa mavazi ya Niki kisa anatarajia kua doctorate ungejiuliza hao waliotangulia wanafanya lipi la maana?
Tena ma profesa kabisa wanaongoza kwa anasa za kila aina, wanavyowakunja dada zetu huko vyuoni na wanawake wa bar wanavyofanyiwa na hao unaowaita wasomi walai usinge hukumu uvaaji wa Niki.

Anyway, ushasema ana kofia mbili, naamini anazitumia kila moja mahala pake, akiwa kazi yake ya hip hop atavaa kulingana na kazi yake, akiwa na wasomi wenzake atavaa kulingana na mazingira hayo.

Tukitafuta kuvaa kwa maadili tutakimbiana maana hakuna asiyejua historia ya muafrica, mavazi walituletea hao hao waliotuletea na elimu.
 
Hakuna kitu kama hicho wala hasomei PHD uzushi mtupu.

Ana masters only.
 
ngoja tukualike jukwaa la wajamaa tanzania(JULAWATA) nikki atakujibu.
 
ngoja tukualike jukwaa la wajamaa tanzania(JULAWATA) nikki atakujibu.
 
Usimpangie cha kufanya.

Hao wanaomfundisha wanajua anachokifanya nje ya darasa, hawajaona shida wakaendelea kumfundisha.

Hizo PHD zilizo mtaani zimefanya lipi la maana kuisaidia Tanzania?

Hata wakina Gigi Money wakasomee tu hizo PHD.
 
Ni mbaya sana kumpangia mtu aishi maisha unayotaka wewe
 
Mi nafikili umekulupuka tu mwenyewe wapi imeandikwa ukiwa na elimu kiwango hichi vaa hiv kingine yupo kazini lazima awe na nguvu kushawishi vijana ndio wenye mziki acha avae atakavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…