Umeandika uzi wako vizuri lakini mimi napingana na wewe kwenye vitu viwili; Kwanza si kweli kwamba kwenye Quraan Mwenyezi Mungu hakuaidi uzima/uhai wa milele kwa wanadamu ukisoma Quraan katika zile aya ambazo Mwenyezi Mungu ameahidi pepo kwa waumini, nyingi Mwenyezi Mungu hutaja neema watakazopata peponi kisha humalizia na milele, maana kitu kishakuwa cha milele maana hakina ukomo na ili uzifaidi hizo neema unatakiwa uwe na uhai.
Pili unatakiwa ukumbuke kwamba mwaanadamu ni kiumbe wa matamanio kinachopenda starehe, wakati baba yetu Adam anamuasi Mwenyenzi Mungu alishushwa duniani na baada ya kushushwa duniani Mwenyezi Mungu akamwambia utaishi kutokana na muongozo nitakaowaletea huko duniani wewe pamoja na kizazi chako atakayefata amesalimika na atakaye ukata basi adhabu ya Mwenyezi Mungu itakuwa juu yake. Sasa katika miongozo ya Mwenyezi Mungu kuna jinsi ya kufanya ibada, maamrisho na makatazo yake, sasa ukiangalia kwenye makatazo mengi ni vile vitu ambavyo anavipenda mwanaadamu kama vile pombe na vitu vingine. Kwa hiyo kwa maisha haya ya dunia Mwenyenzi Mungu kavikataza ila wale watakafaulu baada ya maisha haya dunia kuzizuia nafsi zao kutokana na matamanio na kuzifata maamrisho ya Mwenyenzi Mungu basi hao ndio waliofaulu kwa hiyo Mwenyenzi Mungu ameawahidi kuwapa vitu vizuri na vile wanavyovitamani huko peponi, hakutakuwa tena na mipaka wala makatazo kwa vile walivyovitamani. Kumbuka masuala ya kuabudu na kuwekewa mipaka yanaishia duniani, Akhera ni malipo tu kama hukufuata maamrisho ya Mwenyenzi Mungu duniani utaenda motoni huko na kama ulifata utaenda peponi huko utapata starehe za maana ambazo hazina kikomo.
N.b ndio maana unaambiwa maisha haya ya duniani kwa muumini ni gereza.