Niko njia panda msaada

Ni kwel au ni movie duuuh kwel watu mnapitia mengi

Ushauri wa bure maisha ni matamu sana nakuomba tu usije uwa tafta watu wa karibu vunja ndoa kwa amani endelea na maisha yako dunia ni tamu na maisha ni matamu izo ni changamoto unapitia na zitapita,
 
Mkuu yeye alisema amepata ushahidi kwenye simu yake na kila kitu kiko wazi wapi mimi nimemhukumu? huo ndio ushauri wangu toa na wa kwako
Ndivyo anavyosema. Mimi nakuuliza, umesikia pia kutoka upande wa pili? Ndiyo au hapa? Kama hapana unajuaje kwamba anayosema mume ndiyo kweli na yale ambayo hujasikia ndiyo uwongo? Au niulize, ungekuwa na issue na mkeo na aka'share' mambo fulani kuhusu ndoa yenu, je ni sahihi watu waanze kukulaani kwa kusikia tuhuma za mkeo bila kusikia wewe unasemaje? Unaona hiyo ni sahihi au ndio utaratibu wa kuamua jambo kubwa kama hilo? Hebu nijibu hapo!
 
Counselor kama umesoma vizuri msitari wa kwanza nimekuunga mkono hoja ya kutaka yeye afanye uamuzi kutokana na nafsi yake inataka nini.
Pamoja na hivyo nikatoa maswali ambayo anapaswa ajiulize kabla ya kufanya anachohisi nafsi yake inataka.
Ukiwa mshauri siyo vibaya kumpa mtu mtazamo tofauti kidogo ambao huenda alikuwa hajaufikiria au hajaona. Siyo kila jambo ambalo nafsi inakuambia ufanye ni zuri au ni uamuzi sahihi.
Huwezi kumwambia mtu anayetaka kujiua afuate nafsi yake inataka nini.
lazima aambiwe ubaya wa kujiua.
 
1. Hili suala linahusu watu wawili.
2. Upande mmoja wa mwaume tumesikia anayosema yanayomhuzunisha dhidi ya mkewe.
3. Upande wa pili wa mkewe hatujasikia, na hatuna namna ya kusikia.
4. Katika mazingira kama haya si sahihi kumlaumu mkewe kwa kufuata maelezo ya mumewe peke yake.
5. Kufanya hivyo, tunakuwa hatutendi haki, isipokuwa kutoa ushauri unaompendelea mume.
6. Na je angeanza mkewe kulalamika tungesema mume ndiye kakosea wakati hatujui mumewe anasemaje?
7. Kwa kuzingatia hali hii nimeona nibaki neutral, kusudi baadaye ikitokea tukasikia na upande wa pili, tunaweza kuona vizuri zaidi tatizo liko upande gani au halipo kabisa.
8. Hivyo, bado natetea ushauri wangu kwamba it makes a lot of sense under the circumstances kutokuwa na ulande.
 
1. Kuna siku alikuja mtoto wa dada na mumewe, walikuwa wamekorofishana.
2. Mtoto wa dada akasema kwa vile ndugu tulio Dar wewe ndiye mkubwa, basi ndugu wa nyumbani wamesema wewe ndiye utusuluhishe.
3. Alisema anataka waachane na mumewe.
4. Nikakubali kusuluhisha, lakini nikawaambia namna yangu ya usuluhishi ni tofauti.
5. Nikashauri kwamba kila upande useme tatizo liko wapi bila kusema kwamba mume au mke ndiye tatizo (kila mmoja katika maelezo yake aseme anaona tatizo ni ABC).
6. Haikuwa rahisi kwao maana kila mmoja alikimbilia kumtuhumu mwenzake, jambo ambalo kila mara kwenye maongezi yetu niliwashauri kuachana na tuhuma maana mimi kama mshauri nitashindwa kuona tatizo.
7. Baada ya kumaliza kueleza kila upande tatizo liko wapi, nilishauri kwamba warudi nyumbani na kupanga tukutane tena baada ya wiki mbili.
8. Walipoondoka, hawakurudi tena kwangu.
9. Binafsi niliona kwamba tatizo lilipata ufumbuzi.
10. Unfortunately, baadaye, hata hivyo, walikuja kuachana.
11. Ningesema X au Y ndiye mbaya, ningekuwa adui wa mmojawapo.
12. Lakini sikutaka niwe sehemu ya tatizo lao na nadhani nilifanikiwa katika hilo.
13. Katika kutoa ushauri ni vizuri kuepuka kuwa sehemu ya tatizo - jaribu kutokuwa na upande.
 
Ushauri wangu mwambie unampereka nyumbani kwenu na kama aking'ang'ania nyumbani kwao mwambie nikikuoereka huko sitoi tumizi na utakuwa unejitalakia ili achanganyikiwe vzr usimhurumie kabisa
Acha ufala
 

Akienda kujifungua beba kila kitu chake, ukirudi uza nyumba na hama kabisa, kifupi DISAPPEAR
 
tunatolea ushauri kilichopo mezani mkuu.

kama kuna maelezo mengine yataletwa.

Hata mahakamani hakimu/jaji akishasikilzia upande mmoja anasema una kesi ya kujibu au la kisha nakumbia andaa mashahidi.

H
 
tunatoa ushauri kwa kilicho jukwaani.
 
Mbona simpo. Sukuma hiyo mbuzi kwao ikifuatana na ushahidi na talaka juu. Kama kaweza kuleta mwanaume ndani huyo kukuua ni dakika sifuri
 
tunatolea ushauri kilichopo mezani mkuu.

kama kuna maelezo mengine yataletwa.

Hata mahakamani hakimu/jaji akishasikilzia upande mmoja anasema una kesi ya kujibu au la kisha nakumbia andaa mashahidi.

H
Mazingira hapa ni tofauti kabisa na mahakamani ndugu. Makamani huwa pande zote mbili zipo: 1) upande wa mashtaka (mlalamikaji) na 2) upande wa utetezi (mlalamikiwa), na mahakama inaweza kusema upande wa utetezi una kesi ya kujibu siyo kama hukumu, bali kwamba utetezi uweze kutoa ushahidi wake ili mahakama iweze kupima kama una nguvu au hapana na baada ya hapo ndipo mahakama huweza kutoa hukumu, lakini ni baada ya kusikiliza pande mbili. Mfano, hata kwa issue ya huyu ndugu yetu, kama mkewe naye angekuwepo (kwa kuweza kujibu hizi tuhuma), tungeweza kusema shemeji hapa kakosea ili tuweze kusikia upande wake pia na kwa kufanya hivyo tuweze kupima maelezo ya pande zote mbili. Lakini kusikia tu upande mmoja na kutoa uamuzi kwa madai kwamba "huo ndio ushahidi ulio mezani" ni totally wrong". Katika kutoa ufumbuzi wa tatizo hatuwezi kusikia tu upande mmoja na kutoa ushauri dhidi ya upande ambao haujasikilizwa na kama tukifanya hivyo tunakuwa harujatenda haki (hakuna natural justice), maana hata sisi tusingependa tuhukumiwe bila kusikilizwa. Ndiyo maana mimi sikutaka niseme ni upande upi umekosea, bali kwamba kama huyu ndugu yetu in the absence of ushahidi kutoka upande wa pili, kama anampenda mkewe, then ni vizuri akamsamehe, kwa maana kwamba yeye ndiye mwenye uamuzi wa kuachana au kuendelea kuishi na mkewe, lakini sisi jambo ambalo tunaweza kufanya in good faith ni kushauri "waendelee kuishi pamoja na mkewe", na kama hampendi/amekwazika kwa kiasi kikubwa (na ndivyo ilivyo), basi ni yeye pia anayeweza kuamua vinginevyo.
 
tunatoa ushauri kwa kilicho jukwaani.
Lakini kiko nusu. Utatoaje ushauri wakati umesikia tu upande mmoja? Mfano, ukisikia tu kwamba "X kaiba" utajuaje kaiba, na kama hujui huo ushauri unaoutoa unakuwa umelenga nini? Tunaaswa siku zote, "in the absence of certainty suspend judgement".
 
Lakini kiko nusu. Utatoaje ushauri wakati umesikia tu upande mmoja? Mfano, ukisikia tu kwamba "X kaiba" utajuaje kaiba, na kama hujui huo ushauri unaoutoa unakuwa umelenga nini? Tunaaswa siku zote, "in the absence of certainty suspend judgement".
😂😂
 
Lakini kiko nusu. Utatoaje ushauri wakati umesikia tu upande mmoja? Mfano, ukisikia tu kwamba "X kaiba" utajuaje kaiba, na kama hujui huo ushauri unaoutoa unakuwa umelenga nini? Tunaaswa siku zote, "in the absence of certainty suspend judgement".
Mkuu hata kuna wakati mahakama inalazimika kutoa Hukumu baada ya kusikiliza upande mmoja.

yeye aliyeandika anajua kila kitu kikoje, hivyo ushauri wowote ataupima na kuona afuatae upi
 
yye asome kisha ataamua cha kufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…