Suala si nani afungwe au nani apinduliwe kama unavyopanga ratiba ya kuota. Ndoto yangu ya mwisho ina ujumbe mzito: Malkia Huihui wa Ugagagigikoko aliwatupa mkono machawa wake wote, akawapeleka kwenye mti uliojaa mamba na kuwatendea yale ya Iddi Amini baada ya kuona hawana tija.
Cha kusikitisha ni kwamba, baada ya machawa wengi kupitiwa na kupelekwa kuliwa na mamba, hapa jamvini tuliwamisi sana. Japo hawakuwa na umuhimu wowote, vile vituko vyao na sarakasi zao ndizo zilizotufanya tuwakumbuke kwa burudani. Somo hapa ni kwamba propaganda na uchawa zina kikomo chake; hata viongozi wakiamka na kukabili uhalisia, chawa huwa wa kwanza kuliwa na mfumo walioulea