Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Hahaha....unabahati kwenye Account zilikuwemo. Ungevunja ndoa ya Dada yako kwa aibu.
 
Sifa zimekuponza mkiambiwa Dar jiji la biashara muwe mnaelewa 😹😹

Tena nyie kina Ngosha ndo wabishi na ujuaji mwingi.!!
Si vibaya ukaagiza Menu list uweze kuona bei.
Ni busara kununua chakula au huduma ambayo unajua bei kabla ya kuagiza ili urizike nayo.
Mwaka Fulani niliend Jerusalem Israeli.

Nilikuwa na bajeti inayobana sana. Na natakiwa kuishi nayo hivyo hivyo kwa miezi kadhaa.

Siku moja nililala nikaamka muda wa hotel chakula kimeshaisha.

Nilishuka ghorofani na kwenda mtaa wa Hillele angalau nipate mkate maana nilikuwa na njaa kali siwezi kulaka usiku.

Nikasome Menu kwenye Cofee room.

Nilisoma(whole bread) 15Shekeli. Kwa haraka haraka haraka nikadhani ni Mkate mzima.

Nikamwambia mhudumu aniletee. Kumbe bi Slice moja tu ya mkate wa ngano.
🤣🤣🤣
Nikalillpa Dola zangu tano sawa na 15 shekeli. Nikasepa
.
 
Pole mkuu, uwe unauliza next time
Hii Sh. Ngapi hii sh ngapi hauna hela nini?

Sasa wewe jifanye unazo uone.

Kuna jamaa yangu tukiwa chuo kapata hela za boom akabeba Pisi kali Bahari Beach.

Ile pisi ikawa inamkomoa nshikaji, ikaagiza kuku mzima.

Mshikaji alijua ni elfu 30 tu hii.

Kumbe ni 50k.

Akakosa nauli ya kurudi😅😅😅
 
Ubahili ulikuzidi had Nchi za watu dr 😹😹

Mimi rafiki yangu tukiendaga wote kufunga mzigo, anashangaa nikimpa dollar 100 ale chakula na hainiumi…!!
Ila tukiwa bongo siwezi kumpa hiyo pesa kwa Tsh hata iweje🤣🤣

Hii kitu najiulizaga sipati jibu bongo pesa inaniuma.!
 
We ungesema limeanguka lenyewe Watanzania waoga sana kubishana hapo angekua Mzungu asingekubali Wazungu wabishi sana tena ukute Wataliano au Warusi.
 
Hii ilinitokea ledger plaza kule bahari beach. Breakfast ya tuvitu vitu tu halafu sasa bei... Sema sikomi kwenda huwa kuna mazingira mazuri ya kupunguza stress ila sithubutu kwenda na nyomi hata mara moja.
 
Kuna restaurant moja kigamboni marneo ya kibada tuliuziwa bei tofauti ya chakula kinachofanana mimi na jmaaa fulani hadi nilibaki nashangaa nilitaman nimwambie ila nikaamua kukausha sababu alivyotajiwa akalipa akasepa
Mkuu itakua viungo vilivyotuka ni tofauti
 
Hahahaha Mkuu Hela inauma kutokananna jinsi ulivyoipata.
Ndio maana kwenye vibanda vya chips wanawake woote wanaagiza chips Kuku.

Mamen wanangiza chips kavu akijitahidi na soseji moja🤣🤣
 
Hela hata kama unayo ni vema ukawa umeridhika na kile unachoenda kula.
 
Uulize mkuu kabla ya yote. Mm sili msosi bila kuulizq maana kuna maeneo nilikula wali tu na nyama ya ngombe afu bill inakuja 12elf iliniuma sana
 
Bahati yako ungeumbuka.
 
Wengine matapeli.....na hukupaswa kulipa maana hukupewa hizo taarifa za matengenezo mengine.
 
Hapo ulitakiwa uondoke kama upo wale watoto ndo dhamana yako wahudumu wakiwaona wanajua upo around, bahati nzuri mabasi siku hizi yapo hadi usiku, zile nguo ulizoacha kwa shemeji yako unaachana nazo.

Unapanda katarama lux ukifika manyoni ndo unampigia simu dada yako unamwambia akafate watoto wake huko ulipowaacha.
 
Hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…