Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Nimecheka kifala
 
Siku nyingine uliza bei kabla ya huduma wala sio ushamba.
Ushauri wa busara sana huo.

Mi nshajifunza siku nyingi sana hayo mambo, tena kwa kitu kidogo tu, soda.

Nimefika sehemu,... 'tupe soda'.. tukanywa mbili mbili kwa maongezi zaidi tukiwa watatu.

Kila kona bei ya soda inajulikana ni 500/-, nikatoa noti ya Sh. 5,000/-nikitumaini kurejeshewa 2,000/-.

Mhudumu naye akawa anasubiri buku, hadi nilivyoidai kwa sauti, ndonikaelezwa niongeze buku, yaani soda 350ml inauzwa elfu, kwa lipi hasa!

Tangu siku hiyo ni mwiko kwangu kutumia huduma za watu bila kuuliza bei kwanza.
 
We ungesema limeanguka lenyewe Watanzania waoga sana kubishana hapo angekua Mzungu asingekubali Wazungu wabishi sana tena ukute Wataliano au Warusi.
Kuna rafiki yangu ana pub kigamboni, TBL walikuwa wamepiga rangi zao na kuweka Bei za vinyeaji. Kumbe vinywaji vimepanda Bei lakini wao hawajabadilisha Bei ya vinywaji. Wakaja wazungu wameagiza vinywaji wamekunywa wanaondoka wanapewa bili wanagoma, wanasema Bei tunayoijua ni ile iliyobandikwa na siyo hii mnayotupa. Aliyekuja kuamua ugomvi ni baba wa rafiki yangu Ila wazungu waliondoka washindi.
Kesho yake alimwita fundi rangi afute yake matangazo ya Bei.
Baada ya miezi miwili TBL wakaja Tena wanataka kubandika matangazo ilibidi awatoe nduki.
 
Pole sana lakini umefaidi kupata somo hapo. Kati ya mambo nachukia ni kutumia fedha nyingi bila kupata ile kitu wanaita value for money.

Hadi saa naamini si sawa kula mlo unaozidi TZS 7000/- Juzi kati hapo nimekunywa chai na mayai mawili ya kukaanga wananiambia TZS 6,000/- nusura fujo itokee.
 
😂😂😂atakuwa anatumia mkunde pori kama chai haiwezekani we kila tunavyopindua mwaka we una mtoto mng'aa...siku hizi unajikuta mstaarabu mwenyewe 😂😂😂
😹😹😹
Dada wewe si ndo umesema niache ugomvi jamani 🤣

Ila mwafula hapana.!! Kwani kaambiwa dunia aijaze peke yake??
Atamaliza chanjo wengine tukizaa watoto wapate polio bure 🤣
 
Wakati tupo watoto marehebu baba yetu mdogo alikuwa na tabia anatuchukua anatupeleka Oysterbay hotel anatununulia ice cream Sasa Kuna siku katuchukua akaagiza ice cream halafu akatuacha, alipoondoka sisi tukawa tunaendelea kuagiza ice cream.
Aliporudi kuomba bill anakuta bill kubwa kutaka maelezo akaambiwa watoto ndio waliagiza. Akawahoji kwanini waliwasikiliza watoto baada ya ubishi bill iligawanywa Kati yake na wahudumu na ndio ikawa mwisho kutuchukua kula ice cream.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…