Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Do not bite off more than you can chew.Maisha ya kuiga na kujifaragua matokeo yake ndio haya.Ungekufa na tai shingoni baada ya kuamua ulichoamua.Kulalama na kutafuta walioingia cha kike kama wewe haitakusaidia lolote.
mkuu sijataka msaada…nimejifunza tu jambo muhimu na somo la msingi sana.

heshima kwa wajomba nimepata lakini,ndio cha muhimu
 
Kama mlienjoy hakuna shida yeyote,
Hela zinatafutwa ila huo mtoko na wajomba zako utabaki kua ni memory,

Watoto wataulizwa na shemeji,mlienda wapi? Watataje mlipoenda,bila shaka shemeji anajua kua hiyo sehemu vyakula ni gharama,

So,kwa upande mwingine umejijengea heshima fulani mkuu.
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Kuna mitaa hapo mlimani city chakula cha watu watatu bill ilisoma 665,000/=
 
Siku hiyo nimefuata mwenyewe gari langu Dar (wakati huo nimeajiriwa mikoani). Nilikuwa sina uzoefu wa kuendesha umbari mrefu. Ile nakunja kona ya Morogoro naifuata mbuga ya mikumi usingizi ukaanza. Niliamua kuendesha usiku kukwepa matrafiki kwasababu sikuwa vizuri mfukoni ukizingatia ndo nimenunua ndinga na wese la kunifikisha. Basi, ile naianza mbuga ya mikumi usingizi kama woote! (Kama mnavyojua mbuga za wanyama huruhusiwi kusimama! ni sehemu ambayo ni hatari kusimama, au kuegesha gari sijui upige usingizi kidogo). Basi nilipata shida saana ukizingatia ni usiku na nilikuwa peke yangu! Sijui huo usingizi ulitoka wapi maana si kwa kuyumba huko wakati spidi ilikuwa haizidi 40km/h. Mikumi ina urefu kama kilometer 50 - 60 kuivuka na ukiongeza kama kilometer 20 (buffer zone) inafika kama 70km hivi I guess! Nakwambia nilitumia kama masaa 2 kumaliza mbuga na kufika sehemu ya mahoteri. Kipindi hicho ilikuwa mwaka 2014. Basi nikaendesha na kufunguliwa Gate ya hoteli na kuingiza gari ndani ili angalau nikalale pia kwa usalama wa gari. Eeebwaanah wee! Kufika reception naambiwa for a night 🌙 ni 80,000/=. Nilichoka! Kuondoka siwezi! Nikaingiwa na akili ya kujifanya kuna kitu nimesahahu kwenye gari nilivyoingia kwenye gari nikashusha vioo vya nyuma kidogo na kupiga mbonji mpaka asubuhi saa 2. Nashukuru Mungu hakuna aliyenibughudhi na nadhani sijui walinistahi au vipi maana sikuona nikifwatwa au kuuliza nilivyawasha gari asubuhi na kuondoka! Mlinzi alinifungulia Gate kwa tabasamu na kunitakia safari njema na kusema "Karibu tena". Kwakweli bei za uduma sehemu za washua tuwaachie wenyewe!
 
Siku na jamaa mmoja tumetoka kwenda kupiga mdudu tuendelee na mambo ingine, si akaagiza janamke lake lije? Ni ile mikurumbembe ya kuimba taarabu kko huko au migo.
Nikajua hizo ni issue zake hainihusu, e bana likaja na menzie matano.
Ni vibonge aisee wana stamina hatari.
Waligonga menyu , bia kilo 3 ikakata pale mshkaji hana senti kumi.
Kasema kesho narudisha.
Duh tukatoka ikabidi niingie kutoa ulinzi kilo 3 ingine.maana ndo kwanza tunaenda club
Ziliisha zote usiku ule.
Jamaa hajarudisha hata senti.
Kubandeki zake yule fwala
 
Hi
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Hizo bei za kawaida sana. Halafu bia 4000? Hicho kiwanja cha uswazi sana labda ingekuwa 8000 ndo cha kidoni.
 
Back
Top Bottom