Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Binti mmoja mkali enzi hizo dansa Fm marehemu sasa.
E bana katika kupiga sound,
Poa njoo mazoezini.
Nikazama huko sijui Chez ntemba Kino ndani mkwajuni studio.
Ile kufika demu kaja bia zao Heineken, sijakaa vizuri madansa wenzie nao hao km sita hivi.
Halafu hawaulizi ni salamu tu "aa shem pedeshee",
hapo supu , bia zinaenda Tu
Then hao waimbaji hawa wacongo wote hao km 12.
Walifakamia nyama bia, supu km hawana akili nzuri. alafu hao
Wakayeyuka😆.
Nilienda na kilo nikijua bajeti yetu wawili demu hamalizi.
Kuletewa bili "mama nene"🙆‍♂️
K
ilo 3+,
Nikamuita mshkaji aje arekebishe nae ana kilo tu si zaidi.
Duh ikabidi tuache simu, tukazirudia baada ya siku 2
Ndio ikatimia hela ya bill yote.
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Sasa hv unakula mihogo tu huko mbwidu ili kukava loss
 
Shida supermaket ina CCTV but in any case kulikua na upangaji mbovu au kuna mteja ali mix mafile kabla ya mtoa mada
Ule upande wa shelf ni kama ulikuwa umetegeshwa hivi yani Mimi kitendo cha kuchukua chupa ya wine lahaula chupa zipo chini tayari vipande vipande nilitoa macho maana sikutarajia kabisa such a shit to happen
 
😀😀 Sifa zinaua Kaka .
Wewe ulishakuwa mgeni hapo kwa shemeji ulitakiwa kukaa kimya upewe kila kitu alafu jioni ujikatae pekee yako ukale ulabu urudi ulale siku ziishe upande katarama uende zako kwenu Sengerema Sasa ona Yaliyokukuta

By the way hayajawahi kunikuta ,kwasababu pia sipendi kwenda kwenye nyumba za watu ,napendelea kukaa kwangu na kutumia hela zangu pekee yangu sio na mtu au watu
Pili kuukiza bei sio ushamba
 
Ule upande wa shelf ni kama ulikuwa umetegeshwa hivi yani Mimi kitendo cha kuchukua chupa ya wine lahaula chupa zipo chini tayari vipande vipande nilitoa macho maana sikutarajia kabisa such a shit to happen
Kama zilikua shelf za mbao, hua zinaoza mkuu...

Kuna jamaa alienda super market na mtoto yanamkuta pia, ila yeye ilikua wine moja tu...
 
Back
Top Bottom