Niliahirisha uamuzi wangu wa kumtongoza baada ya kuniuliza nafanya kazi wapi

Ungemwambia kazi yako ya kuokota chupa
 
Alijua umemdanganya kutokana na muonekano wako, wanawake waki Tanzania Wana msaminisha ubora wa mwaume kwa muonekano wa mavazi.
 
Mbona ni jambo la kawaida kuuliza mtu anafanya kazi wapi? Unampa hata muhusika uhalisia wako ajue wewe ni mtu wa caliber gani, je kama wewe ni jobless au hufanyi kazi halali?
 
Huu utoto sasa, hujiamini kijana ukaacha kitu kitamu
 
Mbona ni jambo la kawaida kuuliza mtu anafanya kazi wapi?unampa hata muhusika uhalisia wako ajue wewe ni mtu wa caliber gani,je kama wewe ni jobless au hufanyi kazi halali?
Nilijua kitakachofuatia hapo ni baby nikuambie kitu, kwahiyo mfano mimi nikiwa jobless ndo hatonipenda au Gorgeousmimi
 
Ungemwambia kazi yako halafu uone mapokeo yake. Hayo yangekupa picha ya anachomaanisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mwenyewe kama ikitokea ukapata mtoto wa kike, binti yako akiletewa barua, swali la kwanza kumuuliza "mumeo mtarajiwa anafanya kazi wapi ".

Maswali mepesi sana, sasa bora huyo kuna wengine wanaanza kirungu cha laki na msululu wa matatizo.
 
Inawezekana ukawa unafanya kazi benki na yeye anahitaji msaada wa mtu wa benki kufungua akaunti, au sehemu nyingine yoyote anaweza kufanya connection na maisha yake.

Hiyo ni "conversation starter".

Sasa umekimbia conversation starter?
 
Una umri gani? Mbona reasoning yako ya kitoto hivi?..

Ulitaka akuulize nini? Kama kakuhisi jambazi? Asiulize kuwa sure?

Unahisi atakuona una hela? Kwa kula mama ntilie? Seriously?
πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Wanaume wachovu utawajua tu, wachungu kama ndimu.
 
Inawezekana ukawa unafanya kazi benki na yeye anahitaji msaada wa mtu wa benki kufungua akaunti, au sehemu nyingine yoyote anaweza kufanya connection na maisha yake.

Hiyo ni "conversation starter".

Sasa umekimbia conversation starter?
Eti mtu humjui lazima umuanze wewe unaitwa nani, unaishi wapi?
Umeoa ??
Unajishughulisha na nini?
Kwenu wapi na wewe mpo wangapi??
Wa ngapi kwenu?
Unataka urafiki wa kudumu au??
 
Hahahahahaha ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake!!! Kwa kuulizwa unafanya kazi wapi basi akili yako ikahitimisha kwamba anataka kukupiga mzinga!!!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wanawake walio wengi huangukia kwenye penzi la mwanaume anayejiamini. Jiamini kwasababu hata hiyo kazi ya boda boda inakuletea kipato na inaweza kusaidia ukaendesha familia yako kama ilivyo kwa boda boda wengi huku mtaani.

Kuna kijana mmoja yupo Majengo (Arusha) kazi yake ni boda boda lakini mke wake ni Engineer wa masuala ya ujenzi.
 
Huwa najikuta tu nimejitambulisha kama dalali, sijui kwanini..!!
 
Mambo 4 Muhimu ya kujua kwa mtu kabla ya kuwa nae urafiki:

1. Majina yake halisi.
2. Shughuli zake/kazi
3. Anapoishi
4. Familia/rafiki/ndugu wa karibu yake hata mmoja

Ukiona unafikia hatua ya kudate na mtu au kuwa marafiki hajakuuliza hayo maswali au hajui, hajielewi huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…