Niliahirisha uamuzi wangu wa kumtongoza baada ya kuniuliza nafanya kazi wapi

Unaishi kwa wasiwasi sana. Mbona swali la kawaida.
 
Ni swali muhimu tatizo kaliuliza haraka na moja kwa moja, angejizungusha akazuga kidogo,
 
Hilo swali huwa silipendi hata mimi,na mara zote huwa nadanganya kwa kutaja kazi ya hovyo zaidi, ndio mana niko singo, japo ni swali la msingi sana ambalo hata mimi huwa nauliza.

Swali hilo hata siku unaenda kuposa sehemu pia utaulizwa na baba mkwe na pengine mama mkwe.
 
Mwanaume hupaswi kuwa na gubu hivyo
 
Mleta mada umeshapewa darasa la kutosha kabisa, kwamba swali uliloulizwa si tatizo, ni swali jema, mdada wa Mama Ntilie inaonekana anajitambua na alikuwa sahihi kukuliza swali, inaonekana tatizo ni wewe, wasiwasi na mashaka yako tu, na pia ongeza kujiamini na si kila anayeuliza maswali ana mbaya. Sasa, rudi kwa dada mtajie kazi yako (Kama ni kweli ama si kweli) na kisha uendelee na mchakato uliotaka kuuanzisha.

Na ukimaliza kuonana na dada ba kitakachojiri urudi hapa uje kuleta mrejesho
 
Mie nishawahi kupitia changamoto iyo,ila ninachokifanya nikimoja tu akiniuliza nataja kazi ambayo ni ya hali chini,kama yupo tayari basi hatoangalia kazi uliyomtajia
 
I wonder why wanawake wengi sana hapa mjini kitu Cha muhimu Zaid kwao kukuuliza ni unafanya wapi kaz, au una Kaz gani.
Kuna dada mmoja mwanafunz wa chuo kimoja hapa dar tumekutana TU mtandaoni baada ya kuniuliza jina swali la pili unafanya kazi wapi? Na mimi kwa Unaa nikamwambia ni Manager katka kampuni X hapa mjini kumbe ni Kapuku TU niliye mtaani. Amerizika na tunachat Kila cku fresh Tu japo anakomaa tuonane live kabisa anione sa sijui ndo Anataka ajirizishe zaidi, I don't know.
 
alikuwa kabila gani, sio manka kweli huyo? ulifeli wapi mzee, ungemwambia nafanya kazi TRA, au BOT.
 
Mbona ni jambo la kawaida kuuliza mtu anafanya kazi wapi?unampa hata muhusika uhalisia wako ajue wewe ni mtu wa caliber gani,je kama wewe ni jobless au hufanyi kazi halali?
Mkiskia jobless si ndio mwisho wa kujibu sms
 
Point hii
 
Kwa hiyo sisi mafundi jenereta za benki tunakuwepo kwenye kundi gani? Si tunafanya kazi benki pia?
 
Huyo mwanamke anajielewa...kukuuliza kuwa unafanya kazi gani lilikuwa Jambo zuri...maana kazi ni kipimo Cha utu...angedharau kazi yako hapo ulikuwa na haki ya kuacha kumtongoza....hata Adam alipewa bustani na MUNGU ailime kabla ya Hawa kutuchafulia Hali ya hewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…