Niliamua Kuitest Nissan Dualis barabarani

Niliamua Kuitest Nissan Dualis barabarani

Joined
Nov 24, 2018
Posts
48
Reaction score
224
Heshima kwenu wakuu.

Wiki iliyopita niliamua kuifanyia nissan dualis majaribio ya mbio barabarani.( nilikua natafuta ligi kwa udi na uvumba)

Nilitenga hela ya faini 150,000.00 kwa safari ya kutoka Dsm to Singida. Ilipigwa 100,000 nikabaki na 50,000.

Nilianza ligi na Vanguard, crown, subaru. Crown alikuwa ni mjeshi yeye anapita tuu

Ila hadi tunaingia Morogoro crown na subaru tumeziacha nyuma sana.

Kufika Moro, vanguard na mimi na Nissan patrol (DFP)

Vanguard mziki ulimshinda akakaa nyuma nahisi aliogopa trafiki,

Nilifika Mbande ilibidi nikachungulie dereva wa Nisan Patrol ni nani, yule mzee anaendesha gari kama pikipiki anaovertake sehemu hatari balaa

Alikuwa anakimbia aseee, huyu ndio alinipa challenge kwakuwa alikuwa haniachi 500m.

Nissan Dualis ni mnyama sana, hata nikisema nipate gari, narudi kwa Dualisi tena.

Hongereni sana trafiki mnafanya kazi ipasavyo.

Upadates:

Dar es Salaam to Dodoma_( Masaa 5 net) mafuta yaliyotumika 3/4 tank
 
Mmenichekesha sana na comment zenu looh.
Kiufupi napenda sana kundesha gari na napenda ligi ila kuna muda hjwa nasema je likitokea la kutokea.......!! Naanza kiwakumbuka wote waliokwishaniambia wananipenda, nafikiria vile watakuwa wanalia kwa uchungu nikiwa nimekufa kwa ajali......

Basi narudisha kisigino nyuma naanza kwenda mwendo wa kibalozi km 80 pale inapobidi, na 50 mpaka 30 pale nnapotakiwa kutii.

Na safari za nje ya Dar nikiwa naendesha binafsi huwa naifanya sehemu ya starehe, ambapo mwendo usio na ligi unaniondolea stress za kuovertake na kukaza tako 🤣🤣🤣🤣
 
Sisi wa Single hatuna wa kumuacha
 
x trail gari moja ya kijinga sana.....kaulizie mafundi
Mafundi wabongo ndiyo wakijinga...kawaulize Wajapani......wakishindwa kutengeneza kitu hawataki kukubali kuwa wameshindwa...wanaaza kusingizia kuwa hakifai.....

Ingekuwa ni gari ya kijinga ungeshasikia recall huko kiwandani na leo hii kusingekuwepo na Xtrail Generation ya tatu..
 
Back
Top Bottom