Naipenda sana jamii yangu
Nilitamani sana kuwa mwenye mchango katika jamii lakini bahati mbaya mpaka naingia utu uzima sikufanikiwa kutoka kimaisha na kuweza kuifanyia jambo la maana. Niliangalia shughuli niifanyayo, kwa mifano hai ya waliotangulia kuifanya kabla yangu, HAKUNA KUTOKA.
Nilijipima uwezo wangu wa kiakili na ubunifu, nako huko pia sijabarikiwa kiasi cha pekee. Ni uwezo wa kawaida tu kama walionao watu wengi, sina maajabu.
Baada ya kuona hivyo basi nikajikubali na nikaona nifanye jambo lolote hata dogo tu ili mradi awepo wa kufaidika nalo katika jamii. Kwa msaada wa imani yangu ya dini, nikapa la kufanya....kupanda miti ya matunda sehemu ya wazi itakayofikika na yeyote yule.
Ilinigharimu kokwa za embe kumi tu kuweza kufanikisha ukuzaji wa miembe mitatu katika eneo la taasisi fulani hivi ya umma ninayofanyia kazi. Mwaka jana zimeanza kuzaa na vitoto vimeanza kupata chimbo jingine la kuzamia, furaha ilioje! Ahsante Mungu.
Nimehama huko na sasa nipo sehemu nyingine na dhamira yangu ni ileile na ninahusudu sana miembe sababu haina usumbufu sana na inafaidisha wengi zaidi na inadumu sana. Niliwahi kuwapandia mipapai lakini walikula kwa muda mfupi kabla ya haijamaliza maisha. Eneo lina changamoto ya ardhi yenye mawe na chumvi na uoteshaji ni mgumu lakini nitajitahidi tu.
*jamii yangu = pale ninapoishi na kufanyia shughuli zangu.