Nilichobaini kwa watu wa Njombe

Nilichobaini kwa watu wa Njombe

Nakili kuwa nisengeoa njombe sijuw maisha yangekuwaje kuna wakati mambo yaligoma kabsa nikamwambia wife arud home ili nijipange akagoma na kusema kama kufa njaa basi tufe wote just emegin kwao wana kila kitu kwa upendo alionao kwangu hata nikitaka kuchepuka mwili unasinyaa kabsa najiona nitatenda kosa kubwa sana saruti sana wananjombe
 
Mimi siyo mrefu wala mfupi, lakini naweza nikawa mrefu kwa watu wengi wa Njombe!

Kwa siku chache nilizokaa Njombe, nilibaini ukweli kuwa ukubwa wa mwili hauamui "ukubwa" wa mtu. Anaweza akawa na umbo dogo sana lakini akawa ni mtu "mkubwa" sana.

Watu wengi wa Njombe wana maumbo madogo, unaweza kusema ni watu wafupi. Lakini akili zao na utu wao si "mfupi".

Kwa niliyoyashuhudia, nilihitimisha kama ifuatavyo kuhusu watu wa Njombe:

1. Ni watu wanaojikubali! Wamerkdhikia na maumbo yao ya kuzaliwa. Hawahangaiki kuwa kama "wengine" kimwonekano.

2. Ni watu wastaarabu sana, na wakarimu pia. Hata ukimwuliza mtu njia, anakuelekeza kwa upendo utafikiri unamlipa.

3. Ni wajasiri sana. Si wanaume wala wanawake. Wanajua kusimamia kile wanachokiamini.

Nakumbuka, tukiwa stendi kuu ya mabasi tukiwa tunataka kwenda Ludewa, wamama fulani waligoma kulipa nauli kabla gari halijaanza safari. Walikuja kulipa baada ya gari kutoka stendi. Si kama wamama wa mikoa fulani ambao wakikoromewa tu kidogo na konda "wanahanya" utafikiri huo usafiri wamepewa msaada.

Hilo basi likiwa njiani kuelekea Ludewa, lilikwama na hivyo kondakta na dereva wakawaomba abiria msaada wa kusukumwa. Mbona waligoma kufanya hivyo!. Hata mimi ilinibidi "nijikaushe" japo nilitamani kuwasaidia.

Walitoa sababu mbili za kukataa kwao:
A). Wamelipa nauli hivyo ni jukumu la watoa huduma kutafuta namna ya kuwafikisha wanakoenda kama tiketi inavyoonesha

B). Pale kuna vijana wanaoweza kuifanya hiyo kazi hivyo kondakta awalipe vijana waliopo eneo hilo ili waitie hiyo huduma.

Walisimama na huo msimamo mpaka wahudumu wa basi walipojiongeza na hatimaye basi kukwamuliwa.

Lakini hao watu si wakatili. Wana upendo mno. Siku iyo hiyo, wakati tukiendelea na safari, mmoja wa abiria aliugua njiani. Abiria walionesha ushirikiano wa hali ya juu katika kumpatia huduma ya kwanza hadi alipofikishwa hospitalini kwa basi ilo hilo.

4. Ni wachapa kazi sana. Kule kuna wenyeji wenye mashamba makubwa ya parachichi na miti ya mbao na nguzo. Inaonekana kuna mabilionea japo hawapigi kelele.

5. Ni watunzaji wa mazingira. Hata stendi yao ya mabasi, ukiiangalia, inavutia sana. Ina ukijani mzuri ambao umetokana na kupata matunzo stahiki.

Kwa kifupi, watu wa Njombe ni wajasiri, wakarimu, wastaarabu, wanajikubali, wachapa kazi na matajiri wasio na makelele.

Aliyewahi kuwa Mbunge maarufu kipindi cha utawala wa Kikwete, marehemu Deo Filikonjombe alikuwa Mbunge wa Ludewa. Ni zao la Njombe.

Sishangai kwa nini alikuwa jasiri! Ni asili ya watu wa Njombe.

Hongereni watu wa Njombe👏👏👏

Keep it up!
Unakaribishwa mno Njombe!
 
Washamba sio wasafi na wanaongoza kwa ushirikina & utapiamlo
Screenshot_20240411-085645.png
 
Njombe ni paziri sana na wenyeji ni wakarimu mnoo, lkn naomba kujua na kuuliza pia, walio jijenga sana pale Mjini ni waKinga au wa Bena wenyewe? maana nimekaa km miezi 6 pale, huwez amini karibu % kubwa ukienda ktk nyumba/makazi yao Baba kafariki !!(Nina ushahidi wa kutosha kutokana na kazi ya mipangomiji niliokua naifanya), je ni kwa ajili HIV kua ipo kwa kiwango kikubwa au kuna tabia flan ya kuhusu Mali!??
 
kalibu njombe-makowo kwa kilimo cha viazi
Nashukuru sana mkuu!

Kumbe Makowonni eneo? Mimi nilifikiri ni msamiati wa kikwenu wenye maana nyingine tofauti na nijuacho.

Nashukuru kwa mwaliko, lakini Mimi nimelenga kilimo cha parachichi.

Nataka na mimi niwe "bilionea" wa parachichi kama akina NEMES GREEN GARDEN!
 
Mimi siyo mrefu wala mfupi, lakini naweza nikawa mrefu kwa watu wengi wa Njombe!

Kwa siku chache nilizokaa Njombe, nilibaini ukweli kuwa ukubwa wa mwili hauamui "ukubwa" wa mtu. Anaweza akawa na umbo dogo sana lakini akawa ni mtu "mkubwa" sana.

Watu wengi wa Njombe wana maumbo madogo, unaweza kusema ni watu wafupi. Lakini akili zao na utu wao si "mfupi".

Kwa niliyoyashuhudia, nilihitimisha kama ifuatavyo kuhusu watu wa Njombe:

1. Ni watu wanaojikubali! Wamerkdhikia na maumbo yao ya kuzaliwa. Hawahangaiki kuwa kama "wengine" kimwonekano.

2. Ni watu wastaarabu sana, na wakarimu pia. Hata ukimwuliza mtu njia, anakuelekeza kwa upendo utafikiri unamlipa.

3. Ni wajasiri sana. Si wanaume wala wanawake. Wanajua kusimamia kile wanachokiamini.

Nakumbuka, tukiwa stendi kuu ya mabasi tukiwa tunataka kwenda Ludewa, wamama fulani waligoma kulipa nauli kabla gari halijaanza safari. Walikuja kulipa baada ya gari kutoka stendi. Si kama wamama wa mikoa fulani ambao wakikoromewa tu kidogo na konda "wanahanya" utafikiri huo usafiri wamepewa msaada.

Hilo basi likiwa njiani kuelekea Ludewa, lilikwama na hivyo kondakta na dereva wakawaomba abiria msaada wa kusukumwa. Mbona waligoma kufanya hivyo!. Hata mimi ilinibidi "nijikaushe" japo nilitamani kuwasaidia.

Walitoa sababu mbili za kukataa kwao:
A). Wamelipa nauli hivyo ni jukumu la watoa huduma kutafuta namna ya kuwafikisha wanakoenda kama tiketi inavyoonesha

B). Pale kuna vijana wanaoweza kuifanya hiyo kazi hivyo kondakta awalipe vijana waliopo eneo hilo ili waitie hiyo huduma.

Walisimama na huo msimamo mpaka wahudumu wa basi walipojiongeza na hatimaye basi kukwamuliwa.

Lakini hao watu si wakatili. Wana upendo mno. Siku iyo hiyo, wakati tukiendelea na safari, mmoja wa abiria aliugua njiani. Abiria walionesha ushirikiano wa hali ya juu katika kumpatia huduma ya kwanza hadi alipofikishwa hospitalini kwa basi ilo hilo.

4. Ni wachapa kazi sana. Kule kuna wenyeji wenye mashamba makubwa ya parachichi na miti ya mbao na nguzo. Inaonekana kuna mabilionea japo hawapigi kelele.

5. Ni watunzaji wa mazingira. Hata stendi yao ya mabasi, ukiiangalia, inavutia sana. Ina ukijani mzuri ambao umetokana na kupata matunzo stahiki.

Kwa kifupi, watu wa Njombe ni wajasiri, wakarimu, wastaarabu, wanajikubali, wachapa kazi na matajiri wasio na makelele.

Aliyewahi kuwa Mbunge maarufu kipindi cha utawala wa Kikwete, marehemu Deo Filikonjombe alikuwa Mbunge wa Ludewa. Ni zao la Njombe.

Sishangai kwa nini alikuwa jasiri! Ni asili ya watu wa Njombe.

Hongereni watu wa Njombe👏👏👏

Keep it up!
Tuwekee picha zao japo hata moja tuthibitishe tu
 
Rate ya ukimwi huko iko juu sana sana kuwa makini
 
Back
Top Bottom