Nilichobaini kwa watu wa Njombe

Nilichobaini kwa watu wa Njombe

Nimewahi kufika huko

Jamaa ni kawarimu sana

Halafu chakula sio shida kule, ukifika na njaa zako za DSM utakula hadi upasuke tumbo 😅🙌

Usisahau pana maambukizi makubwa sana ya HIV/ Ukimwi

Hivyo ukiopoa vaa Kondomu, tumia kilainishi piga kimoja cha Afya ujilalie zako Usingizi

Ukijifanya unajua sana romance, hata kama utakuwa umevaa Kondomu lazima uondoke na mgeni wa Kaptaini Komba
😂😂😂😂😂😂
Mgeni mgeni mgeni huyu mgeniiii
 
Nature ya mazingura huku mkuu.

Ila wafugaji wapo wa kawaida.

Parachichi huku ndio sehemu yake karibu sana.
Ahlaaaaa!😳😳😳😳
We mbena gani unajua kukuna nazi!?
We mzaramo mkuu umeenda kutalii tu huko,fanya urudi Chalinze Njombe hakuna nazi.
 
GoldDhahabu unasema kweli. Kuna jamaa alienda njombe kwa masuala ya posa . Aliporudi alituambia amekuta watu wa Njombe ni wachapa kazi sana. Wote waliokuwa nao waliishangaa kuona biashara zilianza kuchangamka tangia mapema asubuhi kinyume na mijimingi hapa cnini Tz. NJOMBE OYEE.

Sent from my SM-A045F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu uko huko? Najipanga nije kuanzisha shamba la parachichi.

Ila nimeshangazwa na watu wa Njombe! Mbona hamfugi ng'ombe na mbuzi? Au hizo shughuli hazilipi huko?

Nimekuta baadhi ya wakulima wa parachichi wanaagiza mbolea(samadi ya ng'ombe) mikoani kama Dodoma n.k.
kule ishu ya malisho ni ngumu mji umejaa milima kule sisi nguruwe ndio Kila kitu
 
Wakijitahidi vizuri kwenye lishe bora maumbo yao yanaweza kuwa makubwa. Wale nyama, samaki, maziwa na mayai kwa wingi sana.
 
Mimi siyo mrefu wala mfupi, lakini naweza nikawa mrefu kwa watu wengi wa Njombe!

Kwa siku chache nilizokaa Njombe, nilibaini ukweli kuwa ukubwa wa mwili hauamui "ukubwa" wa mtu. Anaweza akawa na umbo dogo sana lakini akawa ni mtu "mkubwa" sana.

Watu wengi wa Njombe wana maumbo madogo, unaweza kusema ni watu wafupi. Lakini akili zao na utu wao si "mfupi".

Kwa niliyoyashuhudia, nilihitimisha kama ifuatavyo kuhusu watu wa Njombe:

1. Ni watu wanaojikubali! Wamerkdhikia na maumbo yao ya kuzaliwa. Hawahangaiki kuwa kama "wengine" kimwonekano.

2. Ni watu wastaarabu sana, na wakarimu pia. Hata ukimwuliza mtu njia, anakuelekeza kwa upendo utafikiri unamlipa.

3. Ni wajasiri sana. Si wanaume wala wanawake. Wanajua kusimamia kile wanachokiamini.

Nakumbuka, tukiwa stendi kuu ya mabasi tukiwa tunataka kwenda Ludewa, wamama fulani waligoma kulipa nauli kabla gari halijaanza safari. Walikuja kulipa baada ya gari kutoka stendi. Si kama wamama wa mikoa fulani ambao wakikoromewa tu kidogo na konda "wanahanya" utafikiri huo usafiri wamepewa msaada.

Hilo basi likiwa njiani kuelekea Ludewa, lilikwama na hivyo kondakta na dereva wakawaomba abiria msaada wa kusukumwa. Mbona waligoma kufanya hivyo!. Hata mimi ilinibidi "nijikaushe" japo nilitamani kuwasaidia.

Walitoa sababu mbili za kukataa kwao:
A). Wamelipa nauli hivyo ni jukumu la watoa huduma kutafuta namna ya kuwafikisha wanakoenda kama tiketi inavyoonesha

B). Pale kuna vijana wanaoweza kuifanya hiyo kazi hivyo kondakta awalipe vijana waliopo eneo hilo ili waitie hiyo huduma.

Walisimama na huo msimamo mpaka wahudumu wa basi walipojiongeza na hatimaye basi kukwamuliwa.

Lakini hao watu si wakatili. Wana upendo mno. Siku iyo hiyo, wakati tukiendelea na safari, mmoja wa abiria aliugua njiani. Abiria walionesha ushirikiano wa hali ya juu katika kumpatia huduma ya kwanza hadi alipofikishwa hospitalini kwa basi ilo hilo.

4. Ni wachapa kazi sana. Kule kuna wenyeji wenye mashamba makubwa ya parachichi na miti ya mbao na nguzo. Inaonekana kuna mabilionea japo hawapigi kelele.

5. Ni watunzaji wa mazingira. Hata stendi yao ya mabasi, ukiiangalia, inavutia sana. Ina ukijani mzuri ambao umetokana na kupata matunzo stahiki.

Kwa kifupi, watu wa Njombe ni wajasiri, wakarimu, wastaarabu, wanajikubali, wachapa kazi na matajiri wasio na makelele.

Aliyewahi kuwa Mbunge maarufu kipindi cha utawala wa Kikwete, marehemu Deo Filikonjombe alikuwa Mbunge wa Ludewa. Ni zao la Njombe.

Sishangai kwa nini alikuwa jasiri! Ni asili ya watu wa Njombe.

Hongereni watu wa Njombe[emoji122][emoji122][emoji122]

Keep it up!
You said it all bro!!
Karibu sana Njombe.
 
Mkuu uko huko? Najipanga nije kuanzisha shamba la parachichi.

Ila nimeshangazwa na watu wa Njombe! Mbona hamfugi ng'ombe na mbuzi? Au hizo shughuli hazilipi huko?

Nimekuta baadhi ya wakulima wa parachichi wanaagiza mbolea(samadi ya ng'ombe) mikoani kama Dodoma n.k.
Zamani tulikuwa tunafuga ufugaji huria ila kutokana na ardhi nyingi kuwa imewekezwa kwa kilimo cha miti ya mbao na matunda ufugaji huo ukakosa maeneo ya kuchungia hivyo waliobakia wengi wanafuga ufugaji wa kisasa na nyasi za kulisha zinalimwa katika mashamba maalum. Siyo rahisi kujua kama watu wanafuga kwakua mifugo hairandirandi.
Ukitaka kujua wanafuga utaona viwanda vya maziwa maeneo kama Uwemba,Njombe mjini nk
Kuhusu mbolea mahitaji ni makubwa kuzidi wafugaji,mpaka sasa Wilaya inayofuga zaidi mkoani njombe ni Wanging'ombe ambako wanategemea zaidi kilimo cha kutumia wanyama kazi(ng'ombe)
 
Njombe kuna wabena pia.
Wabena ni watu poa sana ila wanaendekeza ulokole to the infinixy.
Wabena wastaarabu,hawana mambo mengi na akikupenda kakupenda.
wabena hao watu wa maana kabisa. nawapenda mnooo. lakini wabena kwao hasa sio Iringa?
 
Njombe ni paziri sana na wenyeji ni wakarimu mnoo, lkn naomba kujua na kuuliza pia, walio jijenga sana pale Mjini ni waKinga au wa Bena wenyewe? maana nimekaa km miezi 6 pale, huwez amini karibu % kubwa ukienda ktk nyumba/makazi yao Baba kafariki !!(Nina ushahidi wa kutosha kutokana na kazi ya mipangomiji niliokua naifanya), je ni kwa ajili HIV kua ipo kwa kiwango kikubwa au kuna tabia flan ya kuhusu Mali!??
Njombe Mjini Wabena,Wapangwa na Wakinga kiasi.
Wakinga wengi wapo Makete na Makambako.
Kuhusu vifo huenda ni suala la kibaolojia tu, hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa mali na vifo hilo suala halipo kabisa Njombe. Kwanza ukijulikana umefanya hivyo hawawezi kukuacha salama.
Labda sababu ya maradhi inaweza kunishawishi maana wengi wa wanaume miaka ya nyuma walikuwa wanaoa wanawake wengi inawezekana ndo chanzo cha magonjwa kusambaa kirahisi na kuwazoa.
 
Tanzania nzima hakuna watu wenye sifa zote hizo labda kama umeamua kuwa chawa wa watu wa njombe.

Ni sehemu gani watu wanahangaika na maumbo yao ya kuzaliwa iwe urefu, ufupi, uwebamba au unene. Kama ni wanawake kutafuta uweupe wa mchina, wanawake wa njombe nao ni mafundi.

Wangekua majasiri, wakarimu, wasitarabu na kujiamini mkoa huo usingeongoza kwa takwimu za HIV, wasingekuwa wanaburuzwa CCM na mkoa ungekua na maendeleo lakini badala yake wamejaa imani potofu za kishirikina.

Uchapakazi unaakisi maisha halisi ya watu, lakini uchapakazi wa watu wa njombe ni kizamani usiozingatia tija, wanawake kwa wanaume kutwa wako shamba lakini mwisho wa siku masilahi kisoda kama ilivyo sehemu zingine za nchi..

Njombe ukimtoa yule jamaa anayelima parachichi nyingi Nemes, mexison na mwenye hillside waliobaki wana hela za ugali na niliowataja nao sio mabillionea. Njombe hakuna mabillionea.

Ni kweli njombe watu wanajituma sana kazi za kilimo lakini efficiency ni ndogo sana kwa sababu wanafanya kilimo cha kizamani .

Namalizia kwa kusema watu wa njombe hawana hizo sifa zote ulizoandika,ni watanzania kama watanzia wengine waliojaa ujinga na umaskini mwing,mtu maskini na mjinga hawezikuwa mstaarabu,mjasiri wala kujiamini.
Pole sana.
Huijui Njombe wewe.
Matajiri wa Njombe wanashinda na watu wengine kikawaida sana. Siyo ajabu kumkuta tajiri anakula supu mahali wanapokula vijana wanaoingiza elfu kumi kwa siku.
Hawana kujitutumua,mtu anapakia semi kadhaa za mbao anaenda Dar anauza halafu anarudi na pesa zake zote mfukoni kiunoni amefunga koti kama mshamba fulani kumbe amebeba mizigo.
Ila msiwakabe sasa[emoji23]
 
Mimi siyo mrefu wala mfupi, lakini naweza nikawa mrefu kwa watu wengi wa Njombe!

Kwa siku chache nilizokaa Njombe, nilibaini ukweli kuwa ukubwa wa mwili hauamui "ukubwa" wa mtu. Anaweza akawa na umbo dogo sana lakini akawa ni mtu "mkubwa" sana.

Watu wengi wa Njombe wana maumbo madogo, unaweza kusema ni watu wafupi. Lakini akili zao na utu wao si "mfupi".

Kwa niliyoyashuhudia, nilihitimisha kama ifuatavyo kuhusu watu wa Njombe:

1. Ni watu wanaojikubali! Wamerkdhikia na maumbo yao ya kuzaliwa. Hawahangaiki kuwa kama "wengine" kimwonekano.

2. Ni watu wastaarabu sana, na wakarimu pia. Hata ukimwuliza mtu njia, anakuelekeza kwa upendo utafikiri unamlipa.

3. Ni wajasiri sana. Si wanaume wala wanawake. Wanajua kusimamia kile wanachokiamini.

Nakumbuka, tukiwa stendi kuu ya mabasi tukiwa tunataka kwenda Ludewa, wamama fulani waligoma kulipa nauli kabla gari halijaanza safari. Walikuja kulipa baada ya gari kutoka stendi. Si kama wamama wa mikoa fulani ambao wakikoromewa tu kidogo na konda "wanahanya" utafikiri huo usafiri wamepewa msaada.

Hilo basi likiwa njiani kuelekea Ludewa, lilikwama na hivyo kondakta na dereva wakawaomba abiria msaada wa kusukumwa. Mbona waligoma kufanya hivyo!. Hata mimi ilinibidi "nijikaushe" japo nilitamani kuwasaidia.

Walitoa sababu mbili za kukataa kwao:
A). Wamelipa nauli hivyo ni jukumu la watoa huduma kutafuta namna ya kuwafikisha wanakoenda kama tiketi inavyoonesha

B). Pale kuna vijana wanaoweza kuifanya hiyo kazi hivyo kondakta awalipe vijana waliopo eneo hilo ili waitie hiyo huduma.

Walisimama na huo msimamo mpaka wahudumu wa basi walipojiongeza na hatimaye basi kukwamuliwa.

Lakini hao watu si wakatili. Wana upendo mno. Siku iyo hiyo, wakati tukiendelea na safari, mmoja wa abiria aliugua njiani. Abiria walionesha ushirikiano wa hali ya juu katika kumpatia huduma ya kwanza hadi alipofikishwa hospitalini kwa basi ilo hilo.

4. Ni wachapa kazi sana. Kule kuna wenyeji wenye mashamba makubwa ya parachichi na miti ya mbao na nguzo. Inaonekana kuna mabilionea japo hawapigi kelele.

5. Ni watunzaji wa mazingira. Hata stendi yao ya mabasi, ukiiangalia, inavutia sana. Ina ukijani mzuri ambao umetokana na kupata matunzo stahiki.

Kwa kifupi, watu wa Njombe ni wajasiri, wakarimu, wastaarabu, wanajikubali, wachapa kazi na matajiri wasio na makelele.

Aliyewahi kuwa Mbunge maarufu kipindi cha utawala wa Kikwete, marehemu Deo Filikonjombe alikuwa Mbunge wa Ludewa. Ni zao la Njombe.

Sishangai kwa nini alikuwa jasiri! Ni asili ya watu wa Njombe.

Hongereni watu wa Njombe👏👏👏

Keep it up!
Kuna jambo umesahau kule njombe kila nyumba kuna mgonjwa wa HIV..... hiii ni moja ya changamoto ya mkoa huo
 
Back
Top Bottom