Nilichobaini kwa watu wa Njombe

Umesahau kukuna nazi πŸ˜‚
 
Ila mbona kuna matukio ya ajabu ajabu sana yanaripotiwa kutoka pande hizo
Njombe
Geita
Kwa siku chache nilizokaa huko, sikukutana na tukio lolote la ajabu, labda mambo na mazingira ya ajabu kama:
1. Miteremko mikali ambayo wakati mwingine nilitamani kushika garini na kutembea kwa miguu

2. Watu kulima mashamba yaliyo kwenye miteremko mikali sana ambayo kama siyo kuona mazao yaliyolimwa, nisingeamini kama kuna raia angeweza kutembea kwenye eneo lenye mteremko mkali kiasi hicho

3. Mabilionea wenye mionekano ya kawaida. Unakuta mtu ana shamba la parachichi zaidi ya ekari 200 lililoajiri wafanyakazi wengi wanaolipwa kwa mwezi lakini hana "makelele"

4. Upatikanaji wa kitimoto kwa wingi na bei rahisi

5. Ukijani karibia mji mzima kama siyo mji wote kutokana na mazingira kutunzwa vizuri

6. Baadhi ya watu kuotesha miti ya miparachichi aina ya HASS kama miti ya mapambo kwenye makazi yao na ofisi zao

7. Mabwana shamba wenye "hela". Wengi wao wana mikataba ya kusimamia mashamba ya wakulima wa parachichi, na hivyo kujikuta wanajikusanyia kitita kizuri cha hela kuzidi baadhi ya waajiriwa wenye masters degree ingawa wao wengi wao wana certificate kutoka Vyuo vya kilimo
 
Wee jamaa ni wa hovyo sana
πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Utaoa kweli ww na kichwa hicho
Huyo nitakayemuoa aje na kitu cha ziada
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mgeni mgeni mgeni huyu mgeniiii
Huyo mgeni anatisha

Najua Vijana wa sasa hawamjui vizuri ndiyo maana wacheza peku mechi zao Kwa kiburi cha Arv πŸ™Œ
 
Hilo basi likiwa njiani kuelekea Ludewa, lilikwama na hivyo kondakta na dereva wakawaomba abiria msaada wa kusukumwa. Mbona waligoma kufanya hivyo!. Hata mimi ilinibidi "nijikaushe" japo nilitamani kuwasaidia.
Sasa huu si ujinga ...kadiri gari linavyochelewa si nyote mnachelewa?
Au Kondakta alilizima kwa kukusudia?
 

Hiyo mipango ya kiccm isiyokuwa na mbele wala nyuma kila mahali ipo.
 
ukiweka utani wote pembeni, watu wa njombe kwa maana ya wabena, wakinga na wapangwa, wanaweza kushika usukani kwenye wanadamu wachapakazi kwa makabila ya Tanzania. mimi sio mtu wa huko, ila nilishawahi kuishi maeneo mengi including huko. wabena kwa mfano wapo vizuri sana kwenye kilimo na maduka ya kawaida. ila wakinga, akizaliwa anawaza tu biashara tena biashara kubwa. wapangwa wanajisogeza polepole ila nao asili yao ileile, wanachapa sana kazi wakipata opportunity. UKioa mke, oa mbena au mpangwa, ila uishi naye kwa amani ama la......, wanao uwezo kuchukua maamuzi magumu. mkinga ukioa hakikisha wewe ni mfanyabiashara pia, hapo mtaendana, ila kama ni mtu mzembe mzembe usiyetafuta pesa, hamtadumu. all in all hayo yapo kwa wanadamu wote ila hicho ndicho hilichokiona kwa watu wa kule wawe wanaishi kule au hawaishi kule ndivyo walivyo.

wanaweza kuonekana wadumavu sio kwasababu hawana chakula, bali kwasababu hawali chakula bora, mkinga yupo tayari ashindie mkate wa asili, hata mbena yupo tayari ale vibaya ila biashara yake iendelee, wanao uwezo mkubwa sana kusevu pesa na hii inasaidia sana kwa vizazi vyao vya mbeleni. mtu ana pesa nyingi hata 100m lakini hali chakula bora anaogopa hela itapungua. ndivyo walivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…