Nilichogundua hawa wanaotetea huu uongozi hapa JF ni kama sisi tuu

Nilichogundua hawa wanaotetea huu uongozi hapa JF ni kama sisi tuu

comrade_kipepe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2019
Posts
8,748
Reaction score
18,096
Kabla ya tukio la Nchimbi kujiuzulu kutokea , walikuja jamaa wawili hapa kuleta za ndani kua Nini kitatokea, Mto wa mbu na britanicca, lakini hawa watetezi wa serikali walibisha sana, na kwa reply zao ukiangalia sio kwamba walikua wanaigiza ila ni kwamba kweli walikua hawajui Nini kinaendelea.

Mwisho wa siku kweli yaliyosemwa yametokea.

Inamana hii timu inayosumbua hapa mitandaoni ni kama sisi tuu, hawana taarifa yoyote ya ndani wanayojua, kipindi cha nyuma nlijua ni watu wa mjengoni kabisa kule, nimekuja kugundua hawa ni watu wa KAWAIDA SANA na weupe mno na hawana chochote wanachojua kinachoendelea kuhusu chama chao.

Inawezekana hawa hata kule kwenye ofisi za kijani hawakanyagi kabisa wanaishia tuu kwenye magrup ya Whatsapp kupewa pesa za vocha.
 
Back
Top Bottom