Nilichogundua hawa wanaotetea huu uongozi hapa JF ni kama sisi tuu

Nilichogundua hawa wanaotetea huu uongozi hapa JF ni kama sisi tuu

Wana njaa tu hao, hata maovu yakifanywa na CCM hawapo tayari kukemea sasa hao watu maana wenyewe hao!
 
Kabla ya tukio la Nchimbi kujiuzulu kutokea , walikuja jamaa wawili hapa kuleta za ndani kua Nini kitatokea, Mto wa mbu na britanicca, lakini hawa watetezi wa serikali walibisha sana, na kwa reply zao ukiangalia sio kwamba walikua wanaigiza ila ni kwamba kweli walikua hawajui Nini kinaendelea.

Mwisho wa siku kweli yaliyosemwa yametokea.

Inamana hii timu inayosumbua hapa mitandaoni ni kama sisi tuu, hawana taarifa yoyote ya ndani wanayojua, kipindi cha nyuma nlijua ni watu wa mjengoni kabisa kule, nimekuja kugundua hawa ni watu wa KAWAIDA SANA na weupe mno na hawana chochote wanachojua kinachoendelea kuhusu chama chao.

Inawezekana hawa hata kule kwenye ofisi za kijani hawakanyagi kabisa wanaishia tuu kwenye magrup ya Whatsapp kupewa pesa za vocha.
Wengi humu ni machawa wanao pewa hela za Vocha kuja kuandika ujinga humu.

Na tena wapo kwenye ma-group ya Whatsapp wanapewa script then wanaisambaza.
 
Hawa ndio wale kama unawakumbuka shule ya msingi walikua wambea, kimbelembele... kitu kidogo tu washafika kwa ofisi ya walimu kusemelea.

Kwa level zao nao wanakitengo chao katika system wanapushi mambo, na kupushi kwao ajenda wanapushi kama wamekatwa vichwa... Yaani hakuna wanalolijua bali ni kutimiza tu hulka yao ya kimbelembele,umbea na ukuda... Ni cheap sana hawa na wanatumika kirahisi sana.

Ingawa wanaumuhimu wao kama wakichezeshwa vizuri... Ndio wanao-neutralize Mambo yakifika shingoni.
 
Siku zote najua hao ni watu masikini wa utu,akili na fedha
 
Back
Top Bottom