Nilichogundua kuhusu Wanawake wa Mombasa...

Nilichogundua kuhusu Wanawake wa Mombasa...

Hivi unaweza ukawatizama watu kwenye Tv, kisha ukapata picha ya tabia zao halisi kweli?? Kwa hiyo wewe baada ya kutazama harusi kwenye Tv tayari umepata picha kuwa hivyo ndivyo wanawake wote wa Mombasa ndivyo walivyo?

Kwa hilo sikubaliani na wewe hata kidogo. Iko hivi, Mombasa hakuna tofauti na miji mingine mikubwa kama vile hapa Dar. Kuna mchanganyiko wa watu wa kila namna, wapo wenye kujisitiri na wasiojua kujisitiri. Nasema hivyo sababu binafsi nimewahi kukaa Mombasa na sikuona tofauti ya tabia za Wanawake wa Mombasa na Dar es salaam.
 
Mie naomba kujua KOJA na KISINIA

Bwana harusi kaveshwa KOJA na best man KISINIA

Sijui maana yake ni nini, japo nimeona wameveshwa taji na best man ua ila kubwa.

MC wa kiume yuko simple kapiga T-shirt na kapelo shughulini heheheheheh.

Nimemuona madimples na koti lake jekundu.

Mmhh ngoja niwaachie wenyewe mie sio ripota wa mambo haya, kwaherini.
 
Alikiba si mchezo ,harusi yake pia imehudhuriwa na raisi wa Mambasa Ustaadhi Hassan Joho wote wakiwa wamevaa kiunoni majambia ya Oman-Muha /Mmanyema na majambia wapi na wapi bana.
 
Kiswahili chenu kipi wabongo au watanganyika kiswahili hamjui kabisa
 
Hapana mkuu sijawahi ila kama ni kweli basi wanapenda tabia ya kitanzania(kumzoea na kumchukulia kila Mtu kama rafiki) ambayo nchi zingine haipo kabisa.
Binafsi nimeoa kule na nachokisema jamaa ni kweli kabisa.

Wanapenda watz na vitu vingi vyetu wanafuatilia na lafudhi ya kiswahili chetu wanakipenda sana.
 
Back
Top Bottom