Nilichojifunza kwa Rais Mteule Ruto na Hayati Rais Magufuli, kwa Mungu kila kitu kinawezekana

Nilichojifunza kwa Rais Mteule Ruto na Hayati Rais Magufuli, kwa Mungu kila kitu kinawezekana

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Ninajua machache juu ya Rais Mteule Ruto juu ya Imani yake kwa Mungu lakini kwa uchache huo yatosha kusema Ruto NI muumini wa Mungu wa kweli Kama alivyokuwa Hayati Magufuli.

Nakumbuka Hayati Magufuli aliwahi kukiri ni Mkapa ndie aliyemshawishi kugombea Urais na Magufuli alipoonesha kutaka kusita Mkapa akamwambia nenda Mungu atakutangulia.

Hofu aliyokuwa nayo Rais Magufuli kabla ya kuchukua fomu ni hofu sawasawa na ile aliyokuwa nayo Rais Mteule Ruto alipoona kiongozi wake na mshirika wake wa karibu akimuunga mkono mpinzani wake Mkuu lakini wote wawili waliweza kushinda hofu hiyo kwa Imani waliyonayo kwa Mungu.

Hakika ukianza na Mungu naye Mungu atamaliza nawe na tukiishuhudia imani Mungu atatusamia. Na hapo ndipo Odinga alipokosea na makosa yake hayasameheki mbinguni wala dunia. Kosa la kumteua mgombea asiyeamini Mungu limemgharimu.

Kabla ya mgombea Odinga kumpendekeza niliamini angeshinda na nikawa namuombea Sana lakini siku alipompendeza mtu asiyeamini Mungu kuwa mgombea mwenza ndio siku nikibadili gia angani na nikasema KAMA BWANA UISHIVYO ODINGA HATOKUWA RAIS baada ya kusema hayo moyoni nikasema ikulu ya nchi inaenda kukaliwa na mpagani siku moja.

Odinga alisahau neno la Mungu linalosema kwamba mamlaka zote zinatoka kwa Bwana na Bwana asingeruhusu mpagani kuwa Rais.

Baada ya kusema hayo nikiri kusema ni Imani tu ndo inatulinda na kutusimamia na Rais Mteule wa Kenya Ruto na Hayati Rais Magufuli wamepigana Vita kwa Imani ni kufanikiwa kushinda maadui zao.
 
Kama Magufuli, Ruto anatuhuma nzito juu ya uhai wa watu fulani huko Kenya.
Hiyo inamfanya kuwa katika bad taste.
 
Kama Magufuli, Ruto anatuhuma nzito juu ya uhai wa watu fulani huko Kenya.
Hiyo inamfanya kuwa katika bad taste.
Watanzania mmelemazwa na siasa za maji taka; ukiulizwa ulete ushahidi utautoa wapi kuthibitisha madai hayo hewa? Wewe siku zote ulikuwa na chuki binafsi na JPM kwa kuwa ulizibiwa kupakua asali bila kuumwa na nyuki....mlamba asali in 'somebody's voice'
 
Mungu hapa ndipo anapofanana na chikaptula. Ruto na magufuli nao ni wachamungu kumbe.
 
Watanzania mmelemazwa na siasa za maji taka; ukiulizwa ulete ushahidi utautoa wapi kuthibitisha madai hayo hewa? Wewe siku zote ulikuwa na chuki binafsi na JPM kwa kuwa ulizibiwa kupakua asali bila kuumwa na nyuki....mlamba asali in 'somebody's voice'
Mmelemazwa?
Naona mpaka uuwawe au upigwe risasi kama Lissu ndio utaamini!
 
Umekosea kumfananisha William Rutto na Magufuli. Magufuli hakuwa mcha Mungu bali alilitumia Kanisa Katoliki kuwapumbaza wananchi wajinga wa Tanzania.

Mcha Mungu hawezi kuua Watanzania wenzie kwa sababu za mtazamo tu kama aluvyowaua akina Ben Saanane, Azory Gwanda, wale wa kwenye viroba aliowatupa baharini na alivyorisha Tundu Lissu ashambuliwe.

Mcha Mungu hawezi kubagua maeneo ya wapinzania kwa ajili ya maendeleo wakati wote wanalipa Kodi.
Kamwe usirudie tena kumfananisha Rais Mteule William Rutto na vitu vya HOVYO
 
Kumbuka hii ni namba 5 kama ya jiwe..ukiijua sili ya namba hiyo kinachotoka vinywani mwao ni tofauti na matendo yao.
Namba 5 sio namba ya kawaida.
Jiwe kaja na slogan ya hapa kazi tu.
Ruto kaja na kazi kazi kakazia na kenya kwanza.

Jiwe kaja na mpango wa rais wa wanyonge.
Ruto kaja na mpango wa bottom up.

Hivyo hii slogan ya kenya kwanza ..ujue huyu ni wa mlengo wa kulia.hivyo atakar cheza na kenye ajiandae kuhama nchi.
Kwa kivuri cha kuombewa na mistari ya niblia ndio itakua kibwagizo chake.
 
msimshirikishe Mwenyezi Mungu kwenye vitu msivyo na uhakika navyo.

Kwa Mungu sio maneno bali ni matendo, matendo ya mja anayajua mwenyewe mwenyezi Mungu sio wewe mwanadamu.

Hata wazinifu, wezi, majambazi, wachawi nk wanaingia sana makanisani na misikitini na humtaja sana Mwenyezi Mungu.
 
JPM alikuwa Mcha Mungu kweli kweli.
Tatizo kubwa linalowakabili baadhi ya Watanzania ni ufinyu wa uelewa.

Wengine wanadhani ukiwa Mcha Mungu hata kama utakuta kuna watenda maovu unatakiwa kukaa kimya tu, kitu ambacho si kweli.
Wengi kwenye hilo ni wabovu sana kuelewa.
 
Ukifahamu uwanja wa siasa utajua kilichotokea nyuma ya pazia
 
Mkuu umezaliwa lini? iyo ni kujionesha mbele za watu kuwa yupo ivyo ila moyoni mwake mwenyewe anajijua yupoje marehemu alikuwa anaomba kila siku watanzania wamuombee cha kushangaza alikataza watu waliotaka kumuombe tundu lissu apone ila yeye anataka watu wamuombee ..mungu siyo mzee mpili ukimfanyia dhiaka lazima atakuhumbua ni ayo tu ..
 
Back
Top Bottom