Nilichojifunza kwenye Corona Tanzania viongozi wengi wa dini kubwa za Kikristo hawamwamini Mungu, wanaamini sayansi

Nilichojifunza kwenye Corona Tanzania viongozi wengi wa dini kubwa za Kikristo hawamwamini Mungu, wanaamini sayansi

Maaslkofu ni wanasayansi?

Hakuna cheo cha uaskofu au u sheikh katika hierarchy za uongozi wa nchi hii.

Ya kaisari na yabakie kwa kaisari kama ambavyo ya madhehebu na yakabakie huko.

Wapo watanzania wenye dini na wasio na dini. Wote watanzania hao. Ila hawapo ma sheikh wala maaskofu wasio na dini.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Matapeli ya dini hayo mkuu! Hayana imani yoyote mimi siku hizi siwaikilizi kabisa najijua mwenyewe tu na dini yangu!
Wewe mbwa acha kutukania viongozi wa dini, nwanaharamu mkubwa wewe, achana na dini za watu wewe mbwa. Huwezi kukashifu dini yaa mtu kwa maslhi yako wewe kibwengo
 
IMG_20210126_192556.png

Tangu kuumbwa kwa ulimwengu, Mungu aliweka sheria zitakazoongoza vitu vyote alivyoviumba. Maarifa mbalimbali ndiyo yamebeba sheria za uumbaji ambao mwanadamu amepewa uwezo huo wa kutambua maarifa ili kumkinga na maradhi na hivyo kuendeleza kizazi chake na kinachofuata. Hivyo basi, Mungu ndiye mwanasayansi mkuu.
 
Wanufaika hizo dini kubwa wanawinda pesa za wafadhili wa chanjo ya Corona kwenye hospital zao wanataka wawaibie kupitia chanjo na pesa za misaada za kupambana na corona hewa...
1. Unakumbuka serekali iliandika write up na ikachukua hela za wafadhili kupambana na Korona ambayo mnasema haipo? Nayo ni kibaka?

2. Unajua kama mkuu anafanyia kazi nyumbani sasa hivi, work from home?

3. Una uhakika waisilamu wako kimya kwenye hili swala la korona?

4. Katika huo waraka wa wakristu nadhani hakuna la ziada zaidi ya kusema watu wachukue tahadhari, wanawe mikono, watumie sanitaiza na wajipe sosho distansi, unajua wizara ya afya nayo inasisitiza haya kila siku? Nayo inataka kupiga hela za wafadhili?

5. Wewe unamuamini Mungu peke yake, kwanini unalala na neti? Kwanini unatumia kondom? Kwanini unakunywa maji ya kuchemsha?
 
Ni wanasayansi waliosema kuna ugonjwa wa Corona hapa duniani na unaua watu ulimwenguni, sote tukaamini.

Ni wanasayansi hao hao waliosema ugonjwa wa Corona umeendelea kuwepo duniani na watu tuchukue tahadhari zote muhimu kadri inavyowezekana. Kwanini tusisite kuamini hilo?
 
Chukua taadhari huku selian hospital kuna wakulungwa nane wamelazwa..
 
Imeandikwa usimjaribu Bwana Mungu wako. Hivi ukishauriwa na Wataalam kuwa usijenge nyumba mabondeni nawe ukakaidi eti Mungu ataikinga nyumba yako dhidi ya mafuriko. Hapo ndiyo kumjaribu Muumba wako.
Je mtu anapokojoa mende, mara amekohoa nyoka na anatoa ushuhuda kanisani, je, kwa imani hiuo corona itapita kona gani?
 
Kwahiyo sayansi haikuletwa na Mungu ??

Je, kama Mungu anapaswa kufanya directly mwenyewe ni Kwanini haya matukio hayakuwa hivi...
Jf kuna watu mnajua mambo hadi mnakera.. ..

punguzeni facts mnapojadiliana na wapumbuvu.
 
Ukisikia utapeli kwenye dini njoo Tanzania.

Nilichojifunza kwenye Corona Tanzaia viongozi wengi wa dini kubwa za Kikristo hawamwamini Mungu wanaamini sayansi na sio Mungu wanayemsingizia kuwa aliwaita wamtumikie...

Nasonga na stimu na ndoto kede ,aiii,dini biashara tutaaminije,waambie Diiii.
 
Ukisikia utapeli kwenye dini njoo Tanzania...
Magufuli yupo vizuri kakataa huo ujinga wa hawa wazungu eti tutangaze tuna korona tukae lockdown,kenya walijifanya kukaa lockdown kukawashinda,uholanzi wananchi wanaandamana hawataki tena kufungiwa ndani.
Watu wanakufa kwa magonjwa mengine wanasingizia korona ili kuleta hofu kwa watu na dunia kwa ujumla.

Screenshot_20210101-150534_WhatsApp.jpg
 

Mithali 14:15​

"Mjinga huamini kila kitu anachoambiwa, lakini mwenye busara huwa na tahadhari."
 
Mungu alimpa mwanadamu utashi, kuna mambo ya kutumia utashi.
Ukiugua malaria huwa unaenda kanisani au msikitini?
 
Watanzania hatuna upekee wowote kiasi eti Mungu atuondoshee sisi tu Corona halafu waja wake wengine wafe tu kwa maradhi hayo hayo Mungu hawezi kufanya upendeleo huo, naamini Corona ilikuwa bado ipo
SIO TULIMUOMBA WAO HAWAJAMUOMBA NDIO UPEKEE WETU
 
Ukisikia utapeli kwenye dini njoo Tanzania.

Nilichojifunza kwenye Corona Tanzaia viongozi wengi wa dini kubwa za Kikristo hawamwamini Mungu wanaamini sayansi na sio Mungu wanayemsingizia kuwa aliwaita wamtumikie.

Kuamini Mungu kuwa aweza Saidia vita dhidi ya Corona kumebaki Kwa waumini wa kawaida yaani walei wakiongozwa na mlei Rais Magufuli.

Viongozi wengi wakubwa wa dini za Kikristo wamemtelekeza Mungu kwa walei wao wametimkia kwa wanasayansi.

They believe in scientists not God. Hii kali ya mwaka! Role ya Mungu katika nchi na katika changamoto wameitupilia mbali na kuwaweka wanasayansi kuwa superior kuliko Mungu wakati mwanasayansi aliyebobea kwenye usomi wa sayansi Dk Magufuli anamtukuza Mungu wao waliokariri elimu wanayoita ya Mungu wanatukuza wanasayansi. NI UTAPELI
Mpaka leo hakuna mtu aliyeweza kuthibitisha Mungu yupo.

Tunazugana tu.
 
Mpaka leo hakuna mtu aliyeweza kuthibitisha Mungu yupo.

Tunazugana tu.
Wewe una uhakika gani kuwa mama yako aliyekuzaa ni huyo na kuwa hukuokotwa porini baada ya kutelekezwa na mama yako halisi
 
Wewe una uhakika gani kuwa mama yako aliyekuzaa ni huyo na kuwa hukuokotwa porini baada ya kutelekezwa na mama yako halisi
Hata kama nimeokotwa porini.

Hili bado halithibitishi Mungu yupo.

Kwa nini unataka kunifanya mimi niwe mjadala wakati mjadala ni Mungu?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Back
Top Bottom