Nilichojifunza kwenye msiba wa kaka

Inatosha kuwa kifo kuwa ni mawaidha kwa waliobaki.

Kama mtu hastuki kwa kifo Cha mwenzake huyo sio mtu tena mana moyo wake ulishajifia.siku nyingi

Mtu asijipe umuhimu katika maisha ya wengine kiasi Cha kudhani kwamba bila yeye maisha ya watu wengine hayatakwenda.

Watu wanaweza kuishi bila ww na maisha yakasonga vizuri tu.

Kifo kipo ndugu zangu na hakikwepeki kwa namna yeyote Ile.
 
Ulichelewa sana kulijua hili mdogo wangu! Nawahurumiaga sana wanaopandisha mabega wanapokuwa na madaraka! Sisi siyo kitu! Tumtangulize Mungu mbele huku tukijitahidi sana kuheshimu watu bila kuwabagua!
 

Poleni Sana Ndugu , Jamaa na Marafiki...M.A.P Brother

Huwa nawashangaa sana watu wanaojiona miungu watu.

Mtu akiwa na nyumba kali ,gari ,demu mzuri na fedha za kwenda kununua bidhaa super market anatanua makwapa utafikiri amepigwa ngumi ya mgongo.

Inatupaswa kuishi low key/Low profile hata kama BANKWA una vibunda.
 
Hivi aliyeishi vibaya au vizuri na watu akifa kuna tofauti gani baina ya hao watu wawili?
Hakuna tofauti! Tofauti huzizua sisi waadaamu. MAHOHEHAHE wa mungu tusiojua hata kesho zetu.

Wote watazikwa tu na maisha yataendelea.
 
Life is illusion 😭😭😭
 
Usiwatumainie binadamu Kamwe.Wengi mpo karibu sababu ya maslahi/kazi na watakuwa benet na wewe ukidhani ni ndugu kumbe sio.Ndio maana utakapokufa wengine hawatafika na wengine baada ya hapo ndio imekwisha.Familia yako itabaki kukukumbuka daima.Somo usiwategemee au kuwatumainia binadamu bali Mwenyezi Mungu pekee.
 
Very true
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…