Nilichojifunza kwenye msiba wa kaka

Amini chief
 
Pole sana dogo,
Yapo mambo ambayo ni vizuri kuyajua:
1. Kumheshimu kwa nafasi yake kila aliepo mbele yako.
2. Asali, sukari na hata chocolate ni vitamu na vinavutia lakini huwezi vitumia kama mbadala wa chumvi.
3. Mara zote wengi wamezikwa na watu ambao sio wa "level" zao (mfano huyo bro wako)
4. Ni vyema sana kuijali familia yako kwani ndo pekee utakuwa nayo hadi siku ya mwisho.
 
Buried my mom's last month. Ni boda boda wakiwa sambamba na traffic waliongoza msafara hadi makaburini kinondoni kwenda kumzika mama yetu. Tuishi na watu vizuri
 
ivi kuna mtu ambaye sio level ya mtu flani?
 
hata jiwe naye alijiita Mungu lakini wapiiii kaishia kufukiwa na mangozi ya kondoo kule kitovuni chttle kimsingi binadamu sisi ni mavi tu, nashangaa watu tunanyanyasana ,be humble life is too short.
 
ivi kuna mtu ambaye sio level ya mtu flani?
Kwa Imagination ndio, kuna watu wako hivyo, wanafeel kwamba wao wako tofauti na wengine, Binafsi katika maisha nimeona na kujifunza mambo mengi sana, Ukishakufa sio issue tena, lazima utazikwa tu, haijalishi ulikuwa nani, haijalishi una pesa au huna,Utazikwa tu.
 
Hili liko wazi mbona, wewe nenda kwenye misiba yote mara nyingi wanaokuwa mbele kusaidia mazishi, kufukia na kazi nyingi ni watu ambao hata huwajui na wale unaowajua labda utakuta wamesimama tu pembeni kuepuka vumbi na kuchafuka labda na hapo ukiangalia kwa jicho la tatu ujuwe na wewe utazikwa na watu usiowajua kabisa. Funzo heshimu kila mtu unamjuwa au humjui napia hudhuria misiba ya watu, sio kufika na kusimama tu ila shughulika japo kidogo. Sio watu wanazika wewe umekaa pembeni unapiga story au uko na simu.
 
Mkuu ulitaka Rais au waziri akamuoshe blaza mochwale?
 
Pole sana,
maisha ni kujifunza, lakini hakuna mtu ambaye hawezi kuzikwa, japo lazima ujue kuwa watu wa kwenu ndio watu wako, Maana ndio watakaolia na wewe na kufurai na wewe wajali sana.
jali familia yako,jali ndugu zako, jali jirani zako kwani siku ukifa nafasi yako itajazwa siku hiyohiyo, kama sio kwa kukaimu ujuwe ni kwa kutangazwa au kuteuliwa mtu mpya.
Suala la kuosha maiti linatofautiana kwa dini ya wakristo na waislamu, wakristo mtu anaoshwa kawaida tu, lakini motuary kuna watu wanafanyaga hizo kazi, ukifiwa wakati wa kuosha maiti unaweza kuingia wakati ndugu yenu anaoshwa hili kuhakikisha kuwa anaoshwa vizuri na anaandaliwa ipasavyo, wewe hutomuosha utalipia tu.
Kaburi linachimbwa kwa pesa au kwa jamaa wa karibu, napo mnachaguana nani atasimamia zoezi hilo, Mfanyakazi wa serikali akifa ni jukumu la serikali kusimamia msiba wake.
Rais au Waziri kuja msibani inategemeana na ukaribu wa mtu aliyefariki, lakini kwa nafasi sio lazima uwaone hao ni watu wazito kiserikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…