Kwanza nianze kwa kunena kuwa kwa mujibu wa muundo wa uongozi kwa katiba tuliyo nayo kwa sasa ni sahihi kuwa na wakuu wa wilaya.
Kwa vile sasa tuko awamu mpya (ya awamu ya sita) ni sahihi pia kwa Raise mpya kusuka timu yake ya uongozi. Namna mojawapo ya kufanya hivi ni kuteua viongozi mbalimbali (wakuu wa wilaya wakiwa ni sehemu ya viongozi wanaoteuliwa na Rais).
Sasa jana (19/06/2021) mkeka alioahadi Madam President ukatoka. Kumekuwa na hisia mchanganyiko juu ya mkeka huo. Wengine wakisema baadhi ya wateuliwa hawakupaswa kuwemo na wengine wakisema hawaoni tatizo kwenye mkeka ule sababu walioteuliwa ni Watanzania wenzetu hivyo sio mbaya nao wakipata nafasi ya kutuongoza. Ni katika mchanganyiko huu ambapo wengine wanadhani ni muda sasa vyeo hivi kuangaliwa upya (kama bado vina tija kwa maendeleo ya Taifa katika enzi hizi).
Nilichojifunza katika teuzi hizi kulingana na "reactions" za wadau wengi ni kwamba:
Mosi: Tuna tatizo kubwa la ajira nchini (huu ni ukweli wa wazi kabisa). Na hivyo wengi wanasubiria nafasi hizi kama sehemu za kupatia ajira. Hii inafanya hata wanaopata nafasi hizi kupambana kujinufaisha badala ya kuwatumikia wananchi waungwana. Hivyo basi mtu anapopata hii nafasi watu wanakuwa na kawivu flani hivi kuwa mwenzangu kapata ajira wakati mimi nipo nipo tu. Hii huzidisha kelele nyingi kutoka kwa wananchi (hasa vijana wasio na ajira).
Pili: Kusema ukweli hizi nafasi za uteuzi zina masilahi mazuri (tofauti na nafasi nyingi za utumishi wa umma mf. Ualimu, uuguzi, nk.). Hii huwafanya watu waone kwamba wanaopata hizi nafasi wameula (kitu ambacho kwa wenye maisha ya kawaida ni kuna ukweli). Hii huwafanya watu wengi wapambane kupata hizi nafasi. Hivyo kawivu kanakuja kuwa kwanini apate yeye na sio mimi?
Way forward?
Kwenye hoja ya kwanza nashauri kuwa hizi nafasi zisiwe sehemu ya kulipana fadhila na kupeana ulaji kishkaji. Zitolewe kwa watu ambao kweli wamethibitika kuwa wana spirit ya kuwatumikia wananchi.
Kwenye hoja ya pili nashauri masilahi ya watumishi wa kawaida na wale wa kuteuliwa na wa kisiasa yaangaliwe vizuri. Pengo kubwa la kimasilahi lililopo kati ya haya makundi yanashawishi watu wa upande huu kutamani kwenda upande ule. Kusiwe na pengo kubwa la masilahi kati ya watumishi wanaojiita wa umma (wakiwemo wale wa kisiasa). Hii itapunguza vishawishi vya watumishi kutamani kupata hizo nafasi ambazo kwa sasa zinatambilika kama za ulaji.
Nawasilisha.