Nilichojifunza kwenye teuzi za Wakuu wa Wilaya Juni 19, 2021

Nilichojifunza kwenye teuzi za Wakuu wa Wilaya Juni 19, 2021

Kwanza nianze kwa kunena kuwa kwa mujibu wa muundo wa uongozi kwa katiba tuliyo nayo kwa sasa ni sahihi kuwa na wakuu wa wilaya.

Kwa vile sasa tuko awamu mpya (ya awamu ya sita) ni sahihi pia kwa Raise mpya kusuka timu yake ya uongozi. Namna mojawapo ya kufanya hivi ni kuteua viongozi mbalimbali (wakuu wa wilaya wakiwa ni sehemu ya viongozi wanaoteuliwa na Rais).

Sasa jana (19/06/2021) mkeka alioahadi Madam President ukatoka. Kumekuwa na hisia mchanganyiko juu ya mkeka huo. Wengine wakisema baadhi ya wateuliwa hawakupaswa kuwemo na wengine wakisema hawaoni tatizo kwenye mkeka ule sababu walioteuliwa ni Watanzania wenzetu hivyo sio mbaya nao wakipata nafasi ya kutuongoza. Ni katika mchanganyiko huu ambapo wengine wanadhani ni muda sasa vyeo hivi kuangaliwa upya (kama bado vina tija kwa maendeleo ya Taifa katika enzi hizi).

Nilichojifunza katika teuzi hizi kulingana na "reactions" za wadau wengi ni kwamba;
Mosi: Tuna tatizo kubwa la ajira nchini (huu ni ukweli wa wazi kabisa). Na hivyo wengi wanasubiria nafasi hizi kama sehemu za kupatia ajira. Hii inafanya hata wanaopata nafasi hizi kupambana kujinufaisha badala ya kuwatumikia wananchi waungwana. Hivyo basi mtu anapopata hii nafasi watu wanakuwa na kawivu flani hivi kuwa mwenzangu kapata ajira wakati mimi nipo nipo tu. Hii huzidisha kelele nyingi kutoka kwa wananchi (hasa vijana wasio na ajira).

Pili: Kusema ukweli hizi nafasi za uteuzi zina masilahi mazuri (tofauti na nafasi nyingi za utumishi wa umma mf. Ualimu, uuguzi, nk.). Hii huwafanya watu waone kwamba wanaopata hizi nafasi wameula (kitu ambacho kwa wenye maisha ya kawaida ni kuna ukweli). Hii huwafanya watu wengi wapambane kupata hizi nafasi. Hivyo kawivu kanakuja kuwa kwanini apate yeye na sio mimi?

Way forward??
Kwenye hoja ya kwanza nashauri kuwa hizi nafasi zisiwe sehemu ya kulipana fadhila na kupeana ulaji kishkaji. Zitolewe kwa watu ambao kweli wamethibitika kuwa wana spirit ya kuwatumikia wananchi.

Kwenye hoja ya pili nashauri masilahi ya watumishi wa kawaida na wale wa kuteuliwa na wa kisiasa yaangaliwe vizuri. Pengo kubwa la kimasilahi lililopo kati ya haya makundi yanashawishi watu wa upande huu kutamani kwenda upande ule. Kusiwe na pengo kubwa la masilahi kati ya watumishi wanaojiita wa umma (wakiwemo wale wa kisiasa). Hii itapunguza vishawishi vya watumishi kutamani kupata hizo nafasi ambazo kwa sasa zinatambilika kama za ulaji.

Nawasilisha.
Kwanini umekuja na ID nyingine halafu umekuja Kujipa 'Like' kwa ID yako ile 'inayozoeleka' hapa?

Japo umejitahidi sana Kujificha katika 'uandishi' wako ila bado ile andika yako imebakia vile vile.

JamiiForums ni raha sana halafu kuna Vituko. Usijali Mama atakukumbuka katika DAS au DED.
 
TUNAPOSEMA:
THE HALLMARKS OF BAD GOVERNANCE:

1. ARBITRARINESS
2. AMBIGUITY
3. CAPRICIOUSNESS

NDIYO KAMA MNAVYOONA!
Hakuna cha ajabu hapo.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Way forward??
Kwenye hoja ya kwanza nashauri kuwa hizi nafasi zisiwe sehemu ya kulipana fadhila na kupeana ulaji kishkaji. Zitolewe kwa watu ambao kweli wamethibitika kuwa wana spirit ya kuwatumikia wananchi.

Kwenye hoja ya pili nashauri masilahi ya watumishi wa kawaida na wale wa kuteuliwa na wa kisiasa yaangaliwe vizuri. Pengo kubwa la kimasilahi lililopo kati ya haya makundi yanashawishi watu wa upande huu kutamani kwenda upande ule
All in all ajira zote nchini ziwekewe utaratibu wa kuomba (application) na vetting ifanyike openly kuondoa tabia ya kujenga himaya za kuyanufaisha magenge fulani ya wahuni wasio na nia njema na viongozi wa ngazi za juu
 
Hakika. Vyeo vingi vya uteuzi viko kwa ajili ya kuwanufaisha washkaji wa viongozi. Kuwe na kuomba kwa uwazi kabsa. Na ndio hivyo vyeo unakuta hata masilahi ni makubwa kweli.
 
Kwanini umekuja na ID nyingine halafu umekuja Kujipa 'Like' kwa ID yako ile 'inayozoeleka' hapa?

Japo umejitahidi sana Kujificha katika 'uandishi' wako ila bado ile andika yako imebakia vile vile.

JamiiForums ni raha sana halafu kuna Vituko. Usijali Mama atakukumbuka katika DAS au DED.
Sijakuelewa mkuu. Sina haja ya kuwa na multiple IDs (though sio dhambi kuwa nazo). Sio mhanga wa hivi vyeo. Ninatoa mtazamo wangu kama raia wa kawaida. Mimi sio popoma. Wacha niishie hapa.
 
Mimi nasema kuteua wanajeshi ni kukosa hekima, kama wanapenda kuwa viongozi wa kiraia wavue magwanda waombe nafasi hizo za chama.
Ila wao kazi yao iwe kuwalinda mipakani mkilala na vimada guest house,??!
au
 
Back
Top Bottom