nilipata kazi na kuajiriwa as mwalimu serikalini hiyo ni baada ya kusota sana kutafta ajira ya fani yangu ya Sheria . Nilikula msoto sana kupata ajira ya sheria , no connection in town huna ajira zaidi ya kufanya KAZI ya kujitolea kweny law firm .
pamoja na familia yangu kuwa na biashara ,mashamba ,magari , B mkubwa hakuwahi niamini na kuniweka mbali na miradi ya home kiasi kwamba nilianza kuhisi mimi sio mtoto wa ile familia why mzee wangu tangu afe natengwa sana na kuwekwa mbali na mali za marehemu baba , wakati wa uhai Mzee mimi nilikuwa karibu sana na mzee,kuna mali mfano Kuna kuna nyumba na shamba la miti nilikuwa nalifahamu mimi tu na mzee alinionyesha na kunitambulisha kwa watu waliokuwa wanalitunza hiyo ni mufundi( siwezi taja Kijiji kwa sababu binafsi) kutengwa na bi mkubwa , kaka na dada zangu kukaa kimya kulinipa jibu kuwa mimi so sehemu ya ile familia either mzee alinizaa kwa mwanamke tofauti au Kuna namna ,hili jambo niliwauliza sana baba wadogo , wajomba na mashangazi jibu lilikuwa nambiwa mimi bado sijakomaa kabisa kuendesha mali . ( Familia yangu nimewasamehe japo nashindwa kusahau)
Hiyo hali ilinafanya nihangaike Sana na Connection nilizokuwa nazo ni zile TU za majeshini , huko ningepata kazi mapema ningetaka lakini sikutaka kabisa kazi ya kuvaa uniform na kuwa mtu wa kusema yes, niliamini kazi za huko haziwezi fanya nitimize ndoto ZANGU, niliapa sitakuwa askari na imebaki hivo. Baada ya kupata ajira ya ualimu i learnt at first kuwa nimepata KAZI isiyokuwa sahihi kabisa kwa ustawi wangu na familia ninayotaka kuwa nayo . So niliamua kutafta side work na nilingia kwenye biashara na kilimo siriasi sana . Mtaji niliutoa mufundi baada ya kuvuna miti haikuwa pesa nyingi ilikuwa kama milioni 20 ya kipindi kile .
Nilitumia platform ya Mzee na kukutan na watu aliokuwa anafanya biashara nao enzi zake , katika pambana yangu nimewahi fanya kazi na mhindi na mchina na ndicho nilichojifunza , 1. Jamaa ni waminifu na kifupi wamenyooka sana ,katika kazi Wana lugha Moja TU 2. Wanachapa sana kazi mfano wachina ninao wafahamu Mimi aisee hawana mapumziko , sijui weekend ni kazi kazi 3. Wana imaani sana 4. Wapo makini sana kuchagua watu wa kufanya nao kazi na marafiki( wengi Wana marafiki wachache sana. Japo mafanikio ya kiuchumi Yana siri nyingi ila tunaweza sikiliza mawaz ya huyu Mzee na kujifunza .
Mimi binafsi sio tajili ila sipo kabisa kwenye list ya watanzania maskini, najaribu kunyoka sana kwenye KAZI zangu ila nimeshindwa kabisa kuwa mkweli kwenye mapenzi huko nimefeeli kabisa na hili linanitesa , japo sasa nimepanga kuoa rasmi hata single mother.