Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

Poleni sana, ila Jifunzeni kusema HAPANA, sio jukumu lenu kuhakikisha wao wanaishi, wana ulemavu? yani wameolewa bado mnawahudumia?

Saidia nduguyako ila usisizidi uwezo, umri haurudi nyuma, kesho kesho kutwa mtazeeka, ijengeni kesho yenu, hao watu hawajaanza kuishi baada ya mumeo kupata kazi, bila roho ngumu kwenye hii dunia hutosimama kamwe,

leo mumeo kibarua kikiota nyasi hawatoishi??
 
"Poverty circle". Kuna dhana kwenye uchumi isemayo "mduara wa umaskini". Hii dhana imejikita katika kuonyesha jinsi ilivyo vigumu kwa mtu aliezungukwa na umaskini (wa kipato) kufanikiwa hata kama akifanya juhudi za kutoka humu kwa sababu wale wanaobaki kwenye mduara huo humvuta kumrudisha ima kwa kujua au kwa kutokujua(ndicho kinachomtokea mumeo). Ndio maana suala la kuushinda umaskini ni la jamii nzima na si la mtu mmoja mmoja.

Mumeo kwa kushirikiana na wewe mnayo nafasi ya kusonga mbele. Mosi kaeni pamoja mjaribu kupanga namna ya kujiwekea akiba. Pili, tafuteni namna ya kuongeza kipato nje ya mishahara yenu. Tatu, tafuteni njia ya kupunguza namna ya kutoa misaada huko ukweni ili muweze kufanikisha ya hapo juu. Kwa hili shirikiana na mumeo na lenu liwe moja. Mfano katika ya mwezi mnaweza kuwataarifu wazazi(wa mumeo). Kuwa kuna matatizo ya kikazi yametokea na ofisi imeamuru kila mfanyakazi afidie hasara kwa kukatwa mshahara wake kwa kiasi kisichopungua laki tatu kwa mwezi kwa kipindi cha mwaka mzima. Kitu cha muhimu ni kulishana yamini ili siri hii isitoke ima mpo pamoja au mmefarakana.
Uso umeubwa na haya na kuna watu wenye mioyo yenye kuguswa na matatizo ya wengine na kusahau yake. Mumeo ni mmoja wao. Jitahidi umsaidie.
 
Nafikiri una machaguo mawili tuu
1. Umuache
Hii ni kama unahisi huwezi kuprosper nae kiuchumi kwa mawazo yako yanavo kutuma juu ya mzigo alio nao.

2. Usimuache

Kwa kuwa umeona hali halisi ya ukweni , kaa naye ongea naye kwa kirefu na kwa kutoa mapendekezo juu ya nn mkifanye ili maisha yenu yawe sawa pasipo kuathiri harakati za kuwasaidia hao ndugu zake, coz hujui hao wamemtoa wapi na wamemsaidiaje hadi kufika hapo alipo na kukukutana na ww hivyo huwezi ukamwambia aache kuwasaidia,
Namna nzuri ni kupanga mipango ya kuanzisha kitu ambacho kitakuwa kinawasaidia hao ndugu zake kujisimamia ( kama unampenda kweli huyo jamaa ako ) Pasipo kumtegemea jamaa ako .
Ndugu nilishakaa nae nikamwambia kila mwisho wa mwezi anipe laki 2 tu nami niongeze za kwangu angalau kila mwezi tunafanya kitu,,, akakubalu ila nimiez 5 tangu tukubaliane hivyo hajafanya kitu kama icho
 
Tatizo mtu akiwa njaa mnampa hela akanunue chakula badala ya kumpa mbegu na jembe akalime ili apate chakula na kesho atakitoa kwa mwengine hatimae atakuwa ameshatengeneza kundi la wengi watakaosaidia wengine hata kama yeye akijitoa na hawatamsahau milele.

Aanze kuangalia changamoto zinazowakabili ili kuzibadili ziwe fursa. Pili aanze kuwapa mitaji midogo midogo isiyozid laki tatu kwa ndugu ake anaowaamini wanauwezo wa kufanya biashara kwa kuwaambia huu ndio msaada wa mwisho na sasa anawakopesha ila watamrudishia. Katika hili awe na roho ya ukatili litakuwa na lawama ila mbeleni watamshukuru sana pindi watapofanikiwa.
Kwa wale wataoendeleza mitaji ndio ataowaongeza kitunisha mtaji kwa wale wataoshindwa inamaana wameamua kushindwa kujisaidia wenyewe.

Nampango wa kutengeneza movie sasa nikipata hela ya kubet itaitwa " Two option One chance " , die or alive. Huyo mumeo asifikiri anawasaidia ngoja kibarua kiote nyasi ndio atajua yule uliemfaa kwenye dhiki kakukimbia na wewe hakuna wa kukufaa tena kwenye dhiki. Endeleeni kuendekeza ujinga ila jua kuwa chanzo cha kuwaharibu ndugu zake ni yeye.
 
Poleni sana,hakuna mahali imeandikwa lazima usaidie familia nzima.Kipato chenu lazima kwanza mpange :
1.Hela ya matumizi ya kawaida
2.Hela ya maendeleo
3.Hela ya akiba
4.Hela ya kusaidia watu na hii ni asilimia ndogo sana
 
Bado unaamini hapo una mme..

Ujanja hapo ni kumtandika nyundo ya kupasulia miamba ya kichwa hadi ummwage ubongo ndiyo akili imkae sawa

Huyo pimbi ana nyota ya kufa maskini na atakufa maskini kweli kweli
 
"Poverty circle". Kuna dhana kwenye uchumi isemayo "mduara wa umaskini". Hii dhana imejikita katika kuonyesha jinsi ilivyo vigumu kwa mtu aliezungukwa na umaskini (wa kipato) kufanikiwa hata kama akifanya juhudi za kutoka humu kwa sababu wale wanaobaki kwenye mduara huo humvuta kumrudisha ima kwa kujua au kwa kutokujua(ndicho kinachomtokea mumeo). Ndio maana suala la kuushinda umaskini ni la jamii nzima na si la mtu mmoja mmoja.

Mumeo kwa kushirikiana na wewe mnayo nafasi ya kusonga mbele. Mosi kaeni pamoja mjaribu kupanga namna ya kujiwekea akiba. Pili, tafuteni namna ya kuongeza kipato nje ya mishahara yenu. Tatu, tafuteni njia ya kupunguza namna ya kutoa misaada huko ukweni ili muweze kufanikisha ya hapo juu. Kwa hili shirikiana na mumeo na lenu liwe moja. Mfano katika ya mwezi mnaweza kuwataarifu wazazi(wa mumeo). Kuwa kuna matatizo ya kikazi yametokea na ofisi imeamuru kila mfanyakazi afidie hasara kwa kukatwa mshahara wake kwa kiasi kisichopungua laki tatu kwa mwezi kwa kipindi cha mwaka mzima. Kitu cha muhimu ni kulishana yamini ili siri hii isitoke ima mpo pamoja au mmefarakana.
Uso umeubwa na haya na kuna watu wenye mioyo yenye kuguswa na matatizo ya wengine na kusahau yake. Mumeo ni mmoja wao. Jitahidi umsaidie.
Jaman mi sijui namsaidiaje sababu tulishakaa nikamwambia kila mwisho wa mwezi anipe laki 3 au 2 tufanye maendeleo lkn hataki ikafikia hatua alipoona namwambia maendeleo ikabidi anifiche kipato chake,,,mshahara ukiingia siambiwi wala akipata semina haniambii kapata ngapi mi nafanyaje?
 
Acha kuniangusha dada yangu. Mwanaume ni shujaa na jasiri kwenye uwanja wa vita na si kwenye mahaba. Wanawake Mungu kawapa kipawa kikubwa katika ushawishi. Kaa chini, waza huku ukiwazua, mumeo huyo unamjua na unajua "angle" ipi utapitia. Kila la kheri na Mungu akutangulie.
 
Sasa nifanyeje? maana mwenzangu yeye dizain kama anawaogopa wazazi
Zungumzeni dada yangu.

Ninyi ndio mnamaamuzi na kipato chenu.Siwaombei baya ila kesho ikitokea hamna hicho kipato hao ndugu itakuaje?Tumieni tuu hekima hata hao ndugu zenu watawaelewa.Huenda ndugu zenu wanajua mna hela nyingi sana na mnachofanya ni kuwasaidia kutoka kwenye chenchi zenu za mjini.Sio kawaida ndugu kuwategemea hadi nguo, ingekua matibabu ningeelewa kidogo ...

Mmewahi kuwaambia hamna hela?Ilikuaje?
 
Dhaaa........huo nao ni upofu, yaani mtu umesota kusoma umepata kazi kisha unaanza kununulia nguo dada zako, hii ndio akili gani sasa. Jambo analopaswa kufanya ni moja tu. Aachanr na familia na ashughulike kwa kiasi tu na baba na mama yake pekee kwa kiwasaidia makazi bora chakula wapambane wenyewe. Hao ndugu wapambane na hali zao tu. Hiyo lazima kuwasaidia imewekwa na nani. Otherwise mtayumba sana na huyo mwanaume asiye na msimamo
Unaweza kuta kusoma kwake,waliuza Mali zote za familia na hao ndugu zake walitumia nguvu zao pia,kwahyo lazma alipe fadhila
 
Kwanza lazima yeye mumeo/mwenzako afahamu kwamba sasa hivi yeye ana jukumu la lazima la kudili na familia yake tu kwa maana ya wewe mkewe na watoto wenu full stop........mambo ya kupeleka msaada kwao haizuiliwi lakini hiyo misaada inatakiwa iwe ni ile muhimu ya kuwalenga wazazi au kuna ugonjwa au kuna msiba, lakini tofauti na hapo na hapo nakwambia maendeleo mtabaki kuyasubiri yeletwe na mbunge wengu kama jinsi mnavyohubiriwa kwenye mikutano yao, hata wahenga waliwahi kusema wema usizidi uwezo huo utakuwa ni ubwege sasa
 
Mshauri mmeo kwenye 1.4ml awe anatoa lak 4 tu kwao nyingine mfanye maisha yenu.
Pili kama atagoma au haeleweki basi atengeneze biashara ya kuwaingizia kipata tofauti na mshahara.
Tatu...wewe mwenyewe anzisha kitu cha ziada ikibidi akuongezee nguvu.
NB: USITHUBUTU KUMROGA ETI ASAHAU KWAO... wakati wa kwao umewaona wanavyomtolea macho, UTAKUFA SIKU SIO ZAKO.
 
Back
Top Bottom