Dolla_Mbili
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 1,207
- 2,981
Afumbe macho kwa mwezi mmoja tu asipahudumie huko kwao then 1.4m akiongeza na 300k yako mfanye kuongeza nguvu ya pamojaSiku zote nimekua nikilalamika humu mme/mwenzangu kutohudumia nyumbani na kuhamishia nguvu kwao ila nilichokiona mpaka nimemuonea huruma.
Iko hivi mimi na mwenzangu tulikua tunaishi pamoja tangu mwaka Jana mwaka huu wazazi wakaamua wakamilishe taratibu zote ikabaki ndoa tu sasa katika maisha na mwenzangu wajibu wake ndani umekua mdogo maendeleo hakuna hafanyi.
Nimeenda kwao likizo nimechoka mwili na roho nimepoteza ndoto za kua na maisha mazuri kabisa jamaa ukoo mzima iwe shangazi, mjomba,Dada zake hata walioolewa yeye ndio anawahudumia.
Nimemuonea huruma maana sio ombi nilazima familia ile dada zake wavae aanunulie nguo kila siku ikifika mwisho wa mwezi hela zote zinaenda kwao ikifika tarehe 10 mshahara umeisha nilikua nachukia namuona hana akili za maendeleo lakini kwa hali nilivyoiona hata yeye hana jinsi.
Jamani nishauri nifanyeje tue na maendeleo na sisi? Sababu kipato changu ni lak 3 binafsi mwenzangu yeye anapokea mil 1.4_5 lakini majukumu ni mengi kwao hawezi kufanya chochote.
Nifanyeje jamani?
1.4M akiitunza ww unatumia 300k yako kuhudumia chakula na mahitaji yako na yake kwa mwezi huo pamoja na chakula kama mko wawili tu naamini itatosha hivyo hapo mnabaki na akiba ya 1.4M
Mwezi unaofuatia anatoa 1M anaongezea pale unanunua bodaboda mmnapatia kijana muaminifu akutetee 10k per day kwa mkataba wa mwaka mmoja
Utabakiwa na 300k yako na yeye 400k itakuwepo, mwezi huo mnatuma nyumbani kwao 200k na 200k kwenu 300k inabaki kuwahudumia tena ninyi ukiongeza na 10k za kila siku hamtashindwa kuishi
Mshahara wa mwezi wa tatu ukija unakua ni wenu sasa ile pikipiki itatosha kuhudumia kwao huko maana 10k per day kwa mwezi ni 300k mkuu
Maisha inasonga mdogo mdogo tu lakini