Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

Siku zote nimekua nikilalamika humu mme/mwenzangu kutohudumia nyumbani na kuhamishia nguvu kwao ila nilichokiona mpaka nimemuonea huruma

Iko hivi mi na mwenzangu tulikua tunaishi pamoja tangu mwaka Jana mwaka huu wazazi wakaamua wakamilishe taratibu zote ikabaki ndoa tu sasa katika maisha na mwenzangu wajibu wake ndani umekua mdogo maendeleo hakuna hafanyi

Nimeenda kwao likizo nimechoka mwili na roho nimepoteza ndoto za kua na maisha mazuri kabisa jamaa ukoo mzima iwe shangazi, mjomba,Dada zake hata walioolewa yeye ndio anawahudumia

Nimemuonea huruma maana sio ombi nilazima familia ile dada zake wavae aanunulie nguo kila siku ikifika mwisho wa mwezi hela zote zinaenda kwao ikifika tarehe 10 mshahara umeisha nilikua nachukia namuona hana akili za maendeleo lakini kwa hali nilivyoiona hata yeye hana jinsi

Jamani nishauri nifanyeje tue na maendeleo na sisi? sababu kipato changu ni lak 3 binafsi mwenzangu yeye anapokea mil 1.4_5 lakini majukumu ni mengi kwao hawezi kufanya chochote

Nifanyeje jamani?
Anza kuuza vitumbua.inalipa sana
 
Ndio maana masikini watabaki masikini na matajiri watabaki matajiri
 
We mwanamke mwema sana I wish ungekuwa wangu,kaa na jamaa umueleze majukumu yake ni wazazi wake baba na mama na familia yake hao dada zake wakadange
 
Saidia ndg kwa kiwango kisizidi hao unaowasaidia sasa Siku ukiwa nanshida hutamuona hata mmoja
 
Hata sisi hatuna kipato, ila tunajua jinsi ya kuishi kwa mipaka, ni muhimu tu ahakikishe wazee wake (mama na baba) wanakuwa na makazi bora kisha chakula wajitafutie au awe anawapa 60,000 tu kwa mwezi, kuhusu ndugu wengine wote wakiwemo dada zake anatakiw akutoawapa hata mia sababu wanajiweza labda kama ni vilema.

akija kukaa sawa awatafutie kazi ndogo ama awape mtaji usiozidis laki 2. asisaidie kuzidi uwezo, atoe pale anapoweza na si kuzidisha
 
Kimsingi hili ndio tatizo linalosababisha vijana wengi wanashindwa kuendelea,ukichomoza tu kama unatokea kwenye ukoo masikini wote wanataka uwahudumie na huwezi kufika mbali.Na ukiishiwa hao hao wanaanza kukusema vibaya kwamba ulikuwa na pesa ukazitumia vibaya, sasa nini kifanyike kama uwezo wako ni Mdogo wahudumie watu wa nyumbani mwako hasa yaani mke watoto na wazazi wengine waeleze ukweli kuwa huna uwezo wa kuhudumia ukoo mzima.
 
Pole sana kwa changamoto unayokumbana nayo.
Ni kweli kuna mazingira ambayo unaweza kuwa umekulia yakakubana ikabidi tu ufanye vile ili kulipa fadhira

Nitakupa mifano miwili mfano kuna sista mmoja na mfahamu yeye hakusoma alikuwa anauza tu kimgawa ila akawa na mdogo wake anasoma yule sista akapata mchumba aolewe lkn alikataa akasema nikiolewa majukumu yatazidi nishindwa kumsomesha dogo. Yule mdogo wake alisoma hadi akamaliza chuo Mungu mwema alipopata Kazi ndipo akaolewa ila kwa kuchelewa sana hadi watu mtaani wakawa wanamcheka. Sasa kwa mazingira hayo jamaaa aatashindwa kumsaidia ndugu yake.

Ila mfano wa pili. Kuna jamaa yangu yeye alikuwa anasaidia ndugu lakn sio wale wa kuzaliwa nao. Unakuta ndugu wa baba mdogo,, shangazi. Jamaaa alikuwa na Kazi na akafungua duka. Huwezi amini wale watu wakikosa hela ya kula wanaenda kwa jamaa wanasaini tu kwenye daftari wanaondoka na hela. Jamaa kimya akawa hasemi sijui ndo roho nzuri kupindukia. Miaka ikaenda jamaaa Maendeleo hana wenzako wanaofanya nao kazi washampita Maendeleo mbali sana. Baadae si wale ndugu wakaanza kumcheka,,,kukiwa na vikao vya familia wengine na magari yeye hata baiskeli hana.Baada ya hapo ndo akili ikamkaaa kusema hela zote nawasaidia wao Leo wananisema. Hadi Leo ndo angalau amepiga hatua si haba amefungua na kampuni yake anaendesha.

Ushauri wangu! Fanya uchunguzi kwenye hiyo familia yake je aliwezaje kufika hapo alipo.
Lkn pia Maendeleo ni maamuzi binafsi kama unampigia kelele hakuelewi. Kama mwanamke tafuta vikundi vinavyoeleweka cheza hisa baada ya mwaka utapata mtaji fanya biashara ukipata kidogo unaweza kununua kiwanja ukaandika jina la mwanao. Akishaona umefanya kitu basi hata yeye atajiongeza tu.
 
Siku zote nimekua nikilalamika humu mme/mwenzangu kutohudumia nyumbani na kuhamishia nguvu kwao ila nilichokiona mpaka nimemuonea huruma

Iko hivi mi na mwenzangu tulikua tunaishi pamoja tangu mwaka Jana mwaka huu wazazi wakaamua wakamilishe taratibu zote ikabaki ndoa tu sasa katika maisha na mwenzangu wajibu wake ndani umekua mdogo maendeleo hakuna hafanyi

Nimeenda kwao likizo nimechoka mwili na roho nimepoteza ndoto za kua na maisha mazuri kabisa jamaa ukoo mzima iwe shangazi, mjomba,Dada zake hata walioolewa yeye ndio anawahudumia

Nimemuonea huruma maana sio ombi nilazima familia ile dada zake wavae aanunulie nguo kila siku ikifika mwisho wa mwezi hela zote zinaenda kwao ikifika tarehe 10 mshahara umeisha nilikua nachukia namuona hana akili za maendeleo lakini kwa hali nilivyoiona hata yeye hana jinsi

Jamani nishauri nifanyeje tue na maendeleo na sisi? sababu kipato changu ni lak 3 binafsi mwenzangu yeye anapokea mil 1.4_5 lakini majukumu ni mengi kwao hawezi kufanya chochote

Nifanyeje jamani?

Ni miaka mingi imepita. Leta mrejesho
 
Dhaaa........huo nao ni upofu, yaani mtu umesota kusoma umepata kazi kisha unaanza kununulia nguo dada zako, hii ndio akili gani sasa. Jambo analopaswa kufanya ni moja tu. Aachanr na familia na ashughulike kwa kiasi tu na baba na mama yake pekee kwa kiwasaidia makazi bora chakula wapambane wenyewe. Hao ndugu wapambane na hali zao tu. Hiyo lazima kuwasaidia imewekwa na nani. Otherwise mtayumba sana na huyo mwanaume asiye na msimamo
hivi unaweza ukala ukashiba ukalala, baba yako na mama yako hawajala
 
Kuna vitu huwa yunavipuuza na kuamini mradi mnapendana basi hamna kitu kingine cha kutizama.
Kwa mume wa aina hiyo , na kwa madada wa aina hiyo.
Trust me , SIO TU MAENDELEO , HATA MAENDEJANA HAMTAKUWA NAYO.
UKIOLEWA HIYO FAMILIA, utakuja kukumbuka hii comment yangu...
Naiacha hapa.

Uzuri JF ipo hata miaka 10 ijayo.
 
Atoe msaada kwa wazazi,na wadogo zake walio shule,hao wengine atoe pale anapojiweza tena sio kwa kulazimishwa.
 
Hapa beting lazima ihusike..,
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dhaaa........huo nao ni upofu, yaani mtu umesota kusoma umepata kazi kisha unaanza kununulia nguo dada zako, hii ndio akili gani sasa. Jambo analopaswa kufanya ni moja tu. Aachanr na familia na ashughulike kwa kiasi tu na baba na mama yake pekee kwa kiwasaidia makazi bora chakula wapambane wenyewe. Hao ndugu wapambane na hali zao tu. Hiyo lazima kuwasaidia imewekwa na nani. Otherwise mtayumba sana na huyo mwanaume asiye na msimamo

Labda ndo walikua wanamchangia ada mzee wengne kulipiwa ada mpk familia ikae kikao mzee
 
Mwambie mume wako hivi!yeye sio mungu hawezi tatua shida zote za nduguze!!!Ajikite kuwasaidia wazazi tu!hao wengine kama wana miaka zaidi ya 18 wajitegemee!!hawawezi kuwa tegemezi!!!kuwasaidia ndugu vitu sio msaada bali unawalemaza!!!FIKRA TEGEMEZI NI ADUI WA MAENDELEO BINAFSI!!
 
Dhaaa........huo nao ni upofu, yaani mtu umesota kusoma umepata kazi kisha unaanza kununulia nguo dada zako, hii ndio akili gani sasa. Jambo analopaswa kufanya ni moja tu. Aachanr na familia na ashughulike kwa kiasi tu na baba na mama yake pekee kwa kiwasaidia makazi bora chakula wapambane wenyewe. Hao ndugu wapambane na hali zao tu. Hiyo lazima kuwasaidia imewekwa na nani. Otherwise mtayumba sana na huyo mwanaume asiye na msimamo
Huwezi jua ni kwann anashughulikia dada zake na ndugu zake mkuu pengine ndio watu pekee waliomfikisha alipo
Screenshot_20210603-095258_GBWhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom