Siku zote nimekua nikilalamika humu mme/mwenzangu kutohudumia nyumbani na kuhamishia nguvu kwao ila nilichokiona mpaka nimemuonea huruma
Iko hivi mi na mwenzangu tulikua tunaishi pamoja tangu mwaka Jana mwaka huu wazazi wakaamua wakamilishe taratibu zote ikabaki ndoa tu sasa katika maisha na mwenzangu wajibu wake ndani umekua mdogo maendeleo hakuna hafanyi
Nimeenda kwao likizo nimechoka mwili na roho nimepoteza ndoto za kua na maisha mazuri kabisa jamaa ukoo mzima iwe shangazi, mjomba,Dada zake hata walioolewa yeye ndio anawahudumia
Nimemuonea huruma maana sio ombi nilazima familia ile dada zake wavae aanunulie nguo kila siku ikifika mwisho wa mwezi hela zote zinaenda kwao ikifika tarehe 10 mshahara umeisha nilikua nachukia namuona hana akili za maendeleo lakini kwa hali nilivyoiona hata yeye hana jinsi
Jamani nishauri nifanyeje tue na maendeleo na sisi? sababu kipato changu ni lak 3 binafsi mwenzangu yeye anapokea mil 1.4_5 lakini majukumu ni mengi kwao hawezi kufanya chochote
Nifanyeje jamani?