Nilichokikuta ukweni imebidi nimsamehe mume wangu

Mshauri mmeo kwenye 1.4ml awe anatoa lak 4 tu kwao nyingine mfanye maisha yenu.
Pili kama atagoma au haeleweki basi atengeneze biashara ya kuwaingizia kipata tofauti na mshahara.
Tatu...wewe mwenyewe anzisha kitu cha ziada ikibidi akuongezee nguvu.
Mimi ninabiashara ambayo nilimuomba aniongezee mtaji akakataa.... Nikamwambia katika kipato chake nikamuambia awe anatoa laki 2 tu anipe ili tuanze maendeleo bado hakunisapot baada ya kuona naongelea maendeleo sana ikabidi siku hz ananificha kipato chake wala akipata semina haniambii wala sijui matumiz yake.... Nikawa kimya tu
 
Tabia za dada na watoto wao na wazazi wote kumtegemea kaka ktk familia ni kawaida kwa wasukuma. Hapo mtanisamehe ndugu zangu wa kabila hiyo sina nia ya kuwadhihaki.

Kuna wakati mwingine unakuta jamaa alisomeshwa na michango ya dada zake kufanya vibiashara vidogo vidogo au kuuza pombe za kienyeji.
Au misaada toka kwa shemeji n.k.

Sasa mtu kama huyo huwezi kumuambia aache kuwasaidia dada zake. Hapo kinachobakia ni kuambukizana na kurithishana umasikini.
It is very difficult to escape from that vicious cycle of poverty.

Ajitahidi ajitolee kutoa misaada ya elimu kwa wadogo zake na watoto wa dada zake ajipangie labda miaka 4 tu baada ya hapo anabaki kuangalia familia yake tu.

Akisema eti awasaidie miaka yote watabweteka na kutofanya juhudi kujikwamua na jamaa na watoto wake watakufa maskini wote.
 
Unavyosema sio ombi ni lazima kivipi?? Hapana aisee basi awasaidie baba na mama ila sio ndg wote wakati wanafamilia zao dah!!
 
mkuu doh upo,..
 
Endelea kupambana tu na wewe kipato chako kiongezeke...
 
Jitahidi sana muwaze mradi utakaoweza kuendesha nyumba yenu. Ikifika hata mahali wote hamna kipato mradi unakuwepo. Mradi wenu ukishasimama wenyewe. Mshauri afungue mradi mwingine kwao. Mradi uwahusishe ndugu zake na uweze kukidhi mahitaji yao. Kiasi kwamba kila ndugu apate kipato toka kwenye mradi huo kwa kadiri ya mchango wake.
Namna hiyo mtaishi huru bila mizigo ya watu. Misaada itakuwa kidogo
 
Unaeza kuta dada zake waliacha shule au kutopelekwa shule kabisa ili baba yake aweze kumsomesha yeye. Pengine dada zake ndio waliamua kuacha kwenda shule wakaenda shamba ili wamlipie ada kaka yao.

Usilolijua liache lipite
 
Mwambie huyo jamaa aache ujinga wa kuhudumia ndugu wengi namna hiyo anatakiwa angalau awakumbuke wazazi mara moja moja kama na wao wana uwezo wa kufanya kazi si lazima hata wao kuwahudumia ila kama wamezeeka hawajiwezi anaweza fanya hivyo

Kaa na mumeo na umueleze kwa lugha nzuri na upole wa hali ya juu umueleze ukweli juu ya future yenu itakuwaje kama yeye ataona ni ngumu hawezi kuacha mwambie akate mawasiliano taratibu mwisho watazoea wataacha kuomba au umwambie awaambie kule kwao kuwa ametumbuliwa kazini na hana kazi na anahangaika kupata kazi nyingine kwa maana hiyo wajipange namna ya wao kufanya.......kutokea hapo mnataanza sasa na nyie kufanya yenu

Msisitize kabisa asipofanya hivyo atajikuta anazeeka bila chochote maishani na nikusihi tu usimuonee huruma huyo ni mjinga mwambie ukweli hata kama ni mchungu

Usisahau kutupa mrejesho
 
Mkuu laki nne yote awatumie ya nini? Wazazi wanapaswa watumie laki 1 tu ya mboga kwa mwezi
 
Huyo jamaa yako ni bwege sana kwa nini asikatae? Kwa mtindo huo yeye ndo kadabisha hiyo familia kujaa mpaka mashangazi wako hapo kwa sababu wanajua kuna kula tu bila shida,mwambie aache undezi anatuaibisha wanaume wenzie
 
Hao ndugu zake kwa akili hizo hata ukiwategemeza kiuchumi watakula mtaji na kurudi tena kukuomba
 
Kwahiyo siku Mungu akimchukua mwenzio hao mashangazi watatembea uchi?

Halaf mtu akikwambia hana simu ukumnunulia si ataanza kukusumbua na vocha?!
 
Kwani hao jamaa ni walemavu? Tafuta mwenye afadhali kati yao weka kamtaji ka pamoja. Iwe kuku wa kienyeji wapate mayai wauze waendeshe maisha.
Mkizaa watoto watasoma?
Walime?
Wafuge?
Wafanye hata buashara ndogondogo. Ebo.
 
Mlete tumpige maombi hayo maroho ya umaskini na chuma ulete yakome.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…