Nilichokiona Iringa sakata la machinga kuhamishwa maeneo ya mjini kimenisikitisha

Nilichokiona Iringa sakata la machinga kuhamishwa maeneo ya mjini kimenisikitisha

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Machinga niliowaona hapa ni zaidi ya watu elfu tano hii ni wilaya moja tu hivi tunakwenda wapi kama taifa idadi kubwa.

Je, Tanzania nzima machinga wangapi? Tuna ardhi nzuri, mito na maziwa nini kifanyike nani wakulaumiwa. Je, wananchi wanashindwa kuzitumia fursa huko zilizopo ama ni serikali imeamua kutufanya masikini?

Katika zoezi hili la siku mbili lakuhamishwa mjini tayari vijana wengi mitaji ishakata hii ni dhahiri kabisa kuna bomu litakuja kulipuka mbeleni mana mahali penyewe walipoamishwa ni eneo la makaburi halina wateja tutegemee nini? Kama Hawa machinga wakiacha kazi hiyo uchinga.
 
CHADEMA mnakazi. Uharakati wenu sasa. Haya baada ya Iringa?

Mmesahau Wamasai nao.
 
Wametolewa wapi na wamepelekwa wapi?
 
Mdogo mdogo wataondoka wenyewe na kufungua maduka
 
Wametolewa wapi na wamepelekwa wapi?
Wametolewa town center wamepelekwa huko makaburi ya stendi ya mlandege masikini wanapanga nyanya juu ya makaburi hivyo hivyo ilimradi wapate riziki tayari wengi mitaji ilishakata jana siku yakuamishwa
 
Iringa mnpenda sana kufanyia biashara makaburini. Hata hiyo mashine tatu iko makaburini
 
Serikali ya ccm ilishafeli mda sana.
 
Nilishawaambia kuwa ccm inaongoza nchi bila mipango kwa kutumia mifumo ya zamani ndo maana kila siku machinga watapata shida mbele ya ccm hapa pale walipoamia kuna muda utafka watahamishwa tu matatzo yote ya nchi hii yanaletwa na ccm kwakuwa hawana mipango na wanachi wake ila wanamipango na maslai yao polen Sanaa machinga hii ndo ccm endeleni kuichagua akili itawakaa sawaa
 
Watu walo buzzy kupinga ushoga, umachinga sio vipaumbele vyao.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom