BADO SANAAAAAA
Diamond Show kapiga kuanzia saa 03:30 hadi 05:21
Kapiga ngoma 31 ( 36,2,3,18,43,44,4,6,7,8,11,13,14,16,25,27,28,33,34,37,38,45,46,51,47,30,31,35,49,50,39)kutoka kwenye playlist yake aliyotupostia instagram
Katumia mfumo wa kupiga playback na band pamoja na wacheza show..
1.band ilipwaya maana drumer alikuwa juu ya mziki wote drums zinaakika kuliko mziki wote(kisayansi na hisabati za muziki)
2.wasanii wa Hip Hop bado wamekuwa wageni wa stage( effect ya kubaniwa big stages) hawakujua watu wanataka nini.
3. Kumchukua Dudu baya kutawaangusha Wasafi kwani dudu baya hamna alichofanya. Maneno mengi sana hana kazi wala bazi.
4.moni centrazone na Country boy wameonyesha uzoefu wao wa big stages (fiesta effect)
5. Hawakuwa na stage planner mzuri(kuna gapes kibao stage...kabla ya show na show na stage ipo chini hadi washabiki wanapanda stage.
6. Wasanii wa wasafi hawana uzoefu wa show especially show kubwa...(fiesta effect)
7. Band ya wasafi haina back vocalists wala formation ya band professional.
8.Harmonise anaipa nguvu Theory yangu kuwa akipatikana mastermind kama Ruge akamtengenezea harmonize channel, Diamond hamuwezi Harmonize...Harmonize alitulia stage akacheza na mashabiki...akawaambukiza ile energy yake bila kuwambia piga keleleeee
9. Navy Kenzo bado wageni wa stage kubwa...hapo ndio ubaona tofauti ya wasanii wa club na wasanii wa big stage kama Country Boy na Moni.
10. Mboso peke yake ndiye alitakiwa kuimba na Band hasa ukizingatia uzoefu wake wa stage kubwa na kuomba kwenye team aliotoka nao Yamoto band na ufundi wake wa kupiga chombo.
11. Mboso, ray vanny na lava lava walitakiwa kufanya back vocals wakati wa show ya diamond hiyo ndio definition ya team sio kuwajaza kina tale na fela na salam kwenye stage...na watu wengine wasio wasanii...Stage ni Offisi ya msanii sio offisi ya manager wala mpiga picha wala baunsa, wala kumpandisha steve nyerere na kina aunt ezekiel ni format ya zamani ya show iliyotumiwa na Fiesta... show haikuwa na ubunifu wa stage picture, light wala projection ya picha inayoeleweka... stage ilikosa Theme na Mc (jonijoo) alitakiwa kuhost na yule mwanamke mwengine ila asimpe nafasi hata ya kuwa co host... fela anaingia kila mara na kuwashika wasanii begani huku akiwapa maelekezo fulani maanake anaonyesha stejini yeye ni Boss.