Nilichokiona usiku wa leo, msaada wenu wanaJF

Ndoto hiyo haina maana.
Umeota mtu anakukanda mkono.
Ndoto nyingi hazina maana.
Au unaweza kutoa ndoto ina maana, lakini mambo yakawa ni personal.
Au unaweza kutoa ndoto ukaamia ndoto hii lazima nimueleze kila mtu.
 
Kuna kipindi miezi kadhaa iliyopita nilipata kuteguka kwenye Enka nilipokua huko Milimani lushoto sasa niliporudi mjini hapa nilikaa kama mwezi hivi huku nikitibia mguu!

Sasa usiku nimelala akatokea mtu kwenye NDOTO simjui akaushika mguu wangu huo huo nilioteguka akachukua mafuta kwenye chupa akamimina kwenye Enka akaanza kama kuuchua huku yeye amekaa kwenye kiti cha miguu mitatu na mimi nimekaa chini nimemwelekezea mguu wangu ulioteguka huwezi amini hivi kesho asubuhi naamka Nimepona kabisa mpaka leo! Nikamsimulia mpaka wife hilo tukio akashangaa sana
 
Kwa kweli nina malazi ambayo yananisumbua na shida kiroho na maradhi haya yasemekana ni kutokana na kurogwa
Vizuri, Kama una maradhi basi endelea kuomba na kusoma hizo sura kila unapotaka kulala, Ila ongeza pia asubuhi kabla ya jua kuchomoza zisome kama sio mtu wa ibada anza kusali sala tano na kila baada ya sala ya faradh soma ayatul kursi.
Sura ulizosoma ndio sura zilizokuja katika sunnah na hadith kuwa ndio surah za kupambana na uchawi, hasadi na kijicho hivyo usiwe na shaka unafanya kitu sahihi.
Kikubwa jitahidi kujiweka mbali na madhambi kadri uwezavyo, Utapona maradhi yako. INSHAALLAH..
 
Shukrani jazakhaAllahu Khaira 🙏
 
Kataa ukubali huo ndo ukweli,bado ujajua siri na yaliyo jificha kwenye ulimwengu wa roho
Sasa kama tunaishi kwenye ulimwengu wa nyama yanini kuyajua ya ulimwengu wa roho wakati hayatuhusu, hapo ndipo matatizo yanapoanzia. Ndiyo maana wengine mpaka wanaita majini kwa sababu ya ujuaji wao wa mambo yasiyowahusu
 
Kwanza kabisa nianze Kwa salamu: Asalam alaykum na kwawale wasiopenda salamu hii basi habari za asubuhi ndugu zanguni wana JF.

Kwanza kabisa ningependa kwenda moja kwa moja kwenye pointi husika nayo ni kile nilichokiona usiku wa Leo.

Kwa kawaida yangu na ratiba zangu za kulala siku za hivi karibu zimekuwa kabla ya kulala lazima nichome ubani chumbani na pale ninapotaka kulala ni lazima nishike udhu na Baada ya hapo nasoma surat nas X3 surat faraq X3 surat ikhas X3 na ayatul qurs X3 Kisha huplay Quran na kuiacha ikisomwa kuanzia surat fatiha Kisha Baada ya hapo ndipo hulala zangu nikiongezea na maombi mengine ya kiswahili na udambwi dambwi kama kuomba maisha marefu afya njema na mengine mengine si mnajua life yetu hii "pangu pakavu tia mchuzi" bila maombi haiendi.

Basi bhana leo mida ya saa 10 kama sio Kumi basi 11 au 12 alfajir Giza lilikuwepo si haba kwani sikutoka nje na niliona ni Giza kupitia dilisha ambalo japokuwa lilikuwa na pazia ila I trust my eyes.. bila shaka palikuwa Bado hapajakucha.

Nilichokishuhudia ni kwamba wakati nimelala nimeona viumbe wawili wakiwa na mavazi meupe juu mpaka chini mmoja akiwa karibu na kona ya mlango na wapili akiwa kitandani nilipolala nahisi alikuwa akinikanda kanda mkono wangu wa kushoto yani ubavu wangu wa kushoto kwani nilikuwa nimelalia ubavu mmoja nao ni ule wa kulia na uwa kushoto ukiwa huru na ndio ulikuwa juu nae ndio alikuwa kama kanishika na kufanya kama vile anakanda lakini sielewi kitendo kile dhumuni lake au maana yake nini hasa my point ni hapo alikuwa katika ubavu wa kushoto akidili nao wakati huo huo mwingine akiwa katika Kona ya mlango Yani pembe iliyokaeibu na mlango kwa maana ukifungua mlango inakuwa kama Kona.

Huyu aliekuwa nyuma yangu sikufanikiwa kumuona sura na aliepo mbele yangu aliekuwa kasimama karibu na Kona ya mlango huyu pia sikumuona sura bali niliona tu jinsi alivyosimama sijui kama alikuwa kanipa mgongo au la ila nina walakini alikuwa akinitazama tu Kwa maana hiyo sura ilikuwa mbele ila sikuona zaidi ya vazi lake la rangi nyeupe alilovaa kuanzia chini mpaka juu kama kanzu tu ila Tofauti na yake ni kuwa lake lilifika mpaka kichwani.

Wakati nashuhudia ni kama nilikuwa ndotoni lakini ndoto ambayo ni kama nilikuwa naona kinachoendelea ila Sina la Kufanya zaidi ya kutulia tuli kama mtu aliemwagiwa Maji ya baridi sababu sikuweza kufanya chochote zaidi ya kushuhudia tu kitendo kile kwa sekunde zipatazo 30 hadi 40 Kisha nikashituka kutoka katika hali Ile ya kutoweza kufanya lolote nikiwa kama niko ndotoni.

Enyi wana JF naombeni ushauri na msaada wenu ni nini hiki..
Unaomba maisha marefu hapa duniani na imeandikwa kwenye kuruani kwamba kuzimu Kuna mito ya pombe tamu na vibinti vibichi?

Yaani mtu kakaa nyuma Yako na anakukanda kanda na umetulia tu eti unajisikia raha kweli?

Basi sote kwa pamoja tuseme takbiiiir.
 
Uliiwaita walikuja
 
Uliowaita walikutembelea
 
Sasa hayo si ndo mnayoyaabudu yamekutokea laivu unashangaa nini? Si ndo majini yenyewe? Yaambie yakupe hela!
Wenyewe wanaita majini wema hadi wanawachomea sijuwi madude gani eti ubani.Lengo ni kuwavutia hao viumbe na wamerusiwa
 
We itaita tu maruhani leo wamekupapasa kesho watafanya kitu kikubwa zaidi makalioni mwako
 
Kwanza kabisa nianze Kwa salamu: Asalam alaykum na kwawale wasiopenda salamu hii basi habari za asubuhi ndugu zanguni wana JF.

Kwanza kabisa ningependa kwenda moja kwa moja kwenye pointi husika nayo ni kile nilichokiona usiku wa Leo.

Kwa kawaida yangu na ratiba zangu za kulala siku za hivi karibu zimekuwa kabla ya kulala lazima nichome ubani chumbani na pale ninapotaka kulala ni lazima nishike udhu na Baada ya hapo nasoma surat nas X3 surat faraq X3 surat ikhas X3 na ayatul qurs X3 Kisha huplay Quran na kuiacha ikisomwa kuanzia surat fatiha Kisha Baada ya hapo ndipo hulala zangu nikiongezea na maombi mengine ya kiswahili na udambwi dambwi kama kuomba maisha marefu afya njema na mengine mengine si mnajua life yetu hii "pangu pakavu tia mchuzi" bila maombi haiendi.

Basi bhana leo mida ya saa 10 kama sio Kumi basi 11 au 12 alfajir Giza lilikuwepo si haba kwani sikutoka nje na niliona ni Giza kupitia dilisha ambalo japokuwa lilikuwa na pazia ila I trust my eyes.. bila shaka palikuwa Bado hapajakucha.

Nilichokishuhudia ni kwamba wakati nimelala nimeona viumbe wawili wakiwa na mavazi meupe juu mpaka chini mmoja akiwa karibu na kona ya mlango na wapili akiwa kitandani nilipolala nahisi alikuwa akinikanda kanda mkono wangu wa kushoto yani ubavu wangu wa kushoto kwani nilikuwa nimelalia ubavu mmoja nao ni ule wa kulia na uwa kushoto ukiwa huru na ndio ulikuwa juu nae ndio alikuwa kama kanishika na kufanya kama vile anakanda lakini sielewi kitendo kile dhumuni lake au maana yake nini hasa my point ni hapo alikuwa katika ubavu wa kushoto akidili nao wakati huo huo mwingine akiwa katika Kona ya mlango Yani pembe iliyokaeibu na mlango kwa maana ukifungua mlango inakuwa kama Kona.

Huyu aliekuwa nyuma yangu sikufanikiwa kumuona sura na aliepo mbele yangu aliekuwa kasimama karibu na Kona ya mlango huyu pia sikumuona sura bali niliona tu jinsi alivyosimama sijui kama alikuwa kanipa mgongo au la ila nina walakini alikuwa akinitazama tu Kwa maana hiyo sura ilikuwa mbele ila sikuona zaidi ya vazi lake la rangi nyeupe alilovaa kuanzia chini mpaka juu kama kanzu tu ila Tofauti na yake ni kuwa lake lilifika mpaka kichwani.

Wakati nashuhudia ni kama nilikuwa ndotoni lakini ndoto ambayo ni kama nilikuwa naona kinachoendelea ila Sina la Kufanya zaidi ya kutulia tuli kama mtu aliemwagiwa Maji ya baridi sababu sikuweza kufanya chochote zaidi ya kushuhudia tu kitendo kile kwa sekunde zipatazo 30 hadi 40 Kisha nikashituka kutoka katika hali Ile ya kutoweza kufanya lolote nikiwa kama niko ndotoni.

Enyi wana JF naombeni ushauri na msaada wenu ni nini hiki..
Oohoo! Mkuu isije ikawa ni popo bawa! 🥺 Chukua hatua kwa kuacha mara moja kuyabipu madubwashika hayo.
 
Hao uliowaona ni majini mapepo na sio malaika.Pia inaweza ikawa ni wachawi ambao wanatumia nguvu za giza wakishirikiana na majini.
Tofauti ya imani yangu na imani nyingine zina amini kuna majini wazuri au wanawaita walimu au wazee au mafundi au wataalamu au wasaidizi.
Ninachokifahamu mimi hakuna jini mzuri na hakuna jini anayekusaidia au mwenye urafiki mwema na mwanadamu.Wale ni maadui za wanadamu,ila ni waongo hupenda kuwaongopea wanadamu kuwa wao ni wema na wasaidizi wa wanadamu.
WALICHOKUWA wanakufanyia ni vitendo vya ushirikina.
HASARA ni nyingi uharibufu ndio kazi yao ni roho za uharibifu za kuzimu.Hakuna faida,zaidi ya kukuingiza kwenye ushirikina uganga wa kienyeji wa vitabu visomo,kuwanga na ushirikina.
DAWA SULUHISHO.
Dawa pekee ni YESU PEKEE NDIO KIBOKO YA KUYAONDOA hayo makitu yasikusimburme tena na kukuokoa .
Ukitaka elimu zaidi juu ya hayo majini
jifunze ILIMU au elimu ya Maarifa chuo cha maarifa ya uchawi
na SHEIKH OMARY MNYESHENI aliyekuwa anauafuga hayo majinj na mwalimu ya uchawi Tanga--mfuatilie youtube tv channel inaitwa PROMOVER TV
mwingine
Sheikh HUSSEIN MUBARAKA huyu yupo dodoma makulu youtube channel promover tv
mwingine
AMIEL KATEKELA promover tv youtube
 
Back
Top Bottom