PostGE2025 Nilichokishuhudia kwenye maandamano: Serikali ya Tanzania imeshindwa vita

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ni mfano mzuri wa incompetence iliyoko ngazi ya maamuzi

Mzee kama huyo bado ame stuck on the past, mzee kama huyo hawez kufaidisha kizaz cha sasa
Utamaduni wa kutuza wazee nchi hii lazima ufe
 
Miezi 2 kabla ya maandamano kuna mtu nilikuwa najadiliana naye, nika muuliza hizi gari mpya ila plate number za zamani mna taka kuzifanyia nini?.

akashituka na kusema achana nazo, zime gawiwa ila maelekezo hayaja fika kwetu sisi wa chini.
 
Miaka ya nyuma hapo kidogo Serikali ilikuwa na utaratibu mzuri sana wa kuziona hatari, fursa, changamoto na kuzichukulia hatua.

Mfano: kijana alieonekana kufanya vizuri kimasomo, kimichezo, kiubunifu alitambuliwa na kuanza kuwekwa mbele asonge zaidi, alijulikana kwa mkiti wa kijiji/mtaa, mtendaji kisha Mkuu wa Wilaya Mkoa n.k

Palipokuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani sehemu serikali ilitaka kujua kwa nini? Ni asilimia ngapi ya watu wanaunga hoja mkono, na haraka haraka serikali ilichukua wale wenye mlengo huo na kushirikina nao kufanya hitaji husika na mambo yalirejea shwari.

Vyuo vikuu kulikuwa na vijana wa kuhoji, wale vijana pamoja na vikash kash vidogo vya hapa na pale ila wengi wao wwlipewa nafasi wafanye kile walichodhani kinaleta matokeo ya maslahi ya Taifa kwanza.

Tulipokuwa shule za msingi, sekondary, vyuo, katika kambi za mafunzo neno Maslahi ya Taifa kwanza lilisemwa sana, na ni kweli muda mwingine ulipokuwa unaona jambo lisilo na maslahi ya Taifa mara moja roho ilisita na kuliacha au kulisemea sehemu husika wachukue hatua.


Hali hiyo ikabadilika sijui kuanzia lini

Kwa sasa tupo mahali ambapo mtu muongo, mzandiki, mfitini, mvivu, IQ fupi alimaarufu kama chawa ndio wanapewa kipao mbele (hii hali ipo kitaifa na ofisi nyingi za umma kwa sasa)

Nini ninachotaka kusema hapa, ni kwamba pamoja na ushauri mzuri wa upembuzi wa mawazo uliyotoa hakuna atakae kusikiliza sana sana ukifanikiwa ni kutekwa.

Natamani ile hali ya Maslahi ya Taifa irudi miongoni mwa Wananchi wote.

Hii ya kusema nitatekwa, hii ya kusema niwe muongo mnafiki na chawa mambo yangu yaende, hii ya anae onekana kujua na kushauri anakuwa adui, hii ya chukua chako kama kipo funga domo, tunazama shimoni tuliopo na hawa watoto tuliowatema kutoka kwenye nyonga zetu.

Asante
 
Andiko bora kabisa kutoka kwa mtu makini, Mkuu MALCOM LUMUMBA wewe ni hazina kubwa kwa watu tunaopenda kujifunza na kupata Elimu. Dalili nyingi la anguko la Dola yetu zimeanza muda mrefu, Dalili hizi zimetokea kwenye jamii na tawala nyingine nyingi zilizopita hata Maelfu ya miaka huko nyuma. Ukiwa ni mfuatiliaji mzuri wa viashiria ni rahisi sana kubaini kama mnaenda vizuri au mnapotea. Mzee Nyerere alitupa taifa akaliacha likiwa na Nyufa nyingi, yeye mwenyewe amewahi kukili mara kadhaa kwamba kama tutarithi mabaya yake basi tutakuwa wapuuzi, ndivyo walivyoamua kurithi watawala waliofuata baada yake. Lilikuwa ni suala la Wakati tu kuwa kuna siku tungefika hapa tulipo, kwa anayeona mbali ni hali ya huzuni na kusikitisha sana
 
Ni jana tuu niliwaza kuhusu Ikulu ya Dodoma kumuokoa. Cha kushangaza, wakati Magu anaamua kujenga Ikulu kama ile ya Dar, Dodoma, Kikwete alibeza kimzaha, akisema, "sisi watu wa pwani tulipenda ibaki Dar"
Ilikua kama ile movie ya the purge. Usiku fulan marekani kunakua lawless mpaka asubuhi.
Napoleon bonapatre was defeated at the waterloo. Historia mwalim mbaya sana maaana huwa ana tabia ya kurudia.its highy mighty times our profile maker wajikunje watoe intelligence report na wawe wasomi. Tupubguze kukaa baa na kutoa toa bastol hovyo hovyo.soma namna kgb officer putin alikua attache wa embass dressden german. Highly skilled agent yet hamna mahal alikua anagombea madem kitambaa cheupe
 
Vyombo vya dola mihimili na taasisi nyingi zianitaji ukombozi zimetekwa na wahuni zile story za Polepole sio za kutunga au kuchangamsha genge hapana si umeona amepotea hana maelezo yoyote rais anazindua Bunge uliona anamuongelea polepole au ana laani utekaji acha tu
 
Braza Malkom umenifungua kabisa. Mwaka jana nilifunga biashara baada ya kuajiri hawa GenZ biashara ilikuwa inafanya vizuri lkn ni wakorofi balaa.

Nilikuwa nawapa falsafa za maisha na mafanikio lakini wapi hawanisikilizi.

Sasa nadhani nikifungua tena nitajua namna ya kuishi nao. Umenipa mwanga. Mimi nilitaka waishi ninavyotaka mimi Milenial😂😂
 
JAMBO LA MUHIMU KUFAHAMU NI HILI: Every war is won on logistics not fighting alone. Serikali ya Tanzania ilizidiwa mno akili na walioratibu maandamano ambao ukweli ni kwamba FingerPrints za matukio zinaonesha kabisa kwamba ni wataalamu waliokubuhu wa mambo ya usalama hasa THE DARK ARTS OF INSURRECTION.

Nakubali hili, lakini sina hakika kwanini kichwa chako cha habari kinasema imeshindwa vita! hasa ukizingatia hayo maneno yako hapo juu, Ni wazi wali organize lengo lao lilikuwa ni kudondosha serikali na utawala! Na halikutokea ! Nani mshindi?

Yes tulishinda kwa njia ninazo ziiita butu pengine (shutting down internet), kama wasingezima sijui tungekuwa wapi kwa sasa!
 
Kisasi lazima kilipwe, sasa watu wanafanya marking tu kujua nani anaishi wapi, hivyo ikianza utashangaa ni surprise tu machawa wote wanakuwa homeless ndani ya siku
 

Vingi ulivyosema vinashabihiana sana na millenials. Kwa upande wangu

1. Kizazi, late 1990's - 2000's ni watoto wa kizazi cha 1970's , 1980's , na cha 2010's kinaanza kuwa cha 1990's. Hawa watu wote ni vizazi vilivyoona vyama vingi na soko huria hivyo, hawauoni uzalendo kwa Rais au Chama ndio uzalendo kwa nchi. Mindset aliyoiweka Nyerere kipindi cha monoparty na ujamaa.

Kwa hiyo hivi ni vizazi vilivyoshuhudia utamu wa demokrasia na usasa,

Kikubwa zaidi Urbanization, internet na tamthilia za nje zilizowafanya watu wachukue malezi ya nje. Kuwapa watoto uhuru zaidi na mtoto kuwa mali ya mzazi na si jamii. Hivyo watoto wakapewa uwezo wa kuhoji na kujisimamia

Kiufupi wapo free minded zaidi na hawajafungwa na traditions wala Ujamaa wa Nyerere


2. Unemployment, kama ulivyosema zamani ni kusoma na kuajiriwa. Siku hizi ajira hakuna kwa hiyo muda umewalazimu 2000's kuwa na spirit ya ujasiriamali ambayo haipo safe. Imejawa risks na kutokana na mifumo kandamizi kwa sekta binafsi. Ugumu wa maisha na kufanikiwa kwa upande wao, imewapunguzia utegemezi kwa serikali na kuwafanya wawe huru kiuchumi na hivyo, kuhitaji accountability & solid strategies kuwasaidia kuliko enzi za ajira ambapo serikali ilionekana kama njia pekee ya kutoboa hivyo loyalty zaidi kwa upande wao. Muda umebadilika, serikali is no longer the only gateway to success. Kizazi risk takers wanaziona njia zingine, hivyo less loyalty

3. Shule za kata na vyuo kuongezeka.. Hii imefanya wananchi wengi kuongezeka uelewa na hivyo kizazi cha 1990's & 2000's , wengi si rahisi kurubunika tofauti na vizazi vilivyopita vilivyojaa illiteracy..

4. Smartphones kushusha influence ya media. Zamani serikali iliweza kucontrol narratives kwa sababu ukizima media, unakuwa umezima kila kitu. Ila ujio wa smartphone ambazo zina

camera (rahisi kunasa matukio & ushahidi)

Social media (rahisi kusambaza taarifa, imagine mtu ana followers milioni mbili, likes hadi laki) this is not a joke na huko twitter watu wana anonymous accounts za kuvujishia taarifa za siri

Kwa hiyo si rahisi kucontrol taarifa tena ndio maana ilizimwa internet, media zikanyamazishwa. Yet hakuna kilichofichwa kwa sababu traditional media imeanza kuwa replaced na digital media

5. Maria, sativa, Mange, Polepole, hawa wote waliongeza joto kali la maandamano maana ni kama waliwafungua watu macho. Imagine zile scandals zote za embezzlement na vijana wakiangalia hawana hili wala lile. Wakiangalia kina lissu wapo ndani mara kuna watekaji. Yote haya yalichangia

6. Global Gen Z movement.. Hii naiita "the new decolonization process".. Hata zamani nchi zilidai uhuru baada ya wenzao kupata, ilionesha possibility kwa hiyo , maandamano ya morocco, kenya, madagascar, nepal.. Yote yalitumika kama symbol za harakati..

Bottom line is SERIKALI isitumie njia zile zile za kung'ata na kupuliza, maana yaliyotokea hayatopozwa kirahisi maana nyoyo za vijana zishatolewa bikra ya uoga. Hata kama wasiporipuka hiyo tarehe 9/12.. Serikali isijipe assurance, hekma na busara itumike
 
Point to note: "NOBODY is SAFE".
 
Kwa uliyoyashuhudia kipindi cha maandamano, je kuna mkono toka nje ya mipaka yetu ulikuwa unapush haya maandamano au ni kazi ya ndani tu? Na kama ni ndio, je kwa dhamira gani kulingana na uafahamu wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…