Nilichokisikia kuhusu mkakati wa kummaliza kimuziki Belle 9

Nilichokisikia kuhusu mkakati wa kummaliza kimuziki Belle 9

yeah ni kweli kuna kukubaliwa na kukataliwa
ila kama ulinikataa mwanzo na kuniona siwezi je kuna umuhim wa kunifata
na kutaka niwe chini ya label yenu........

kama ilivyo ukiombwa kuna kukubaliwa na kukataliwa je kuna haja ya kutaka
kunishusha kimuziki kisa nilikataa kuwa chini yenu.....

naomba uclouds uuweke pembeni @be real

kweli baby ninaye
 
kwani tuna jumla ya tv na radio station ngapi hapa TZ?
 
Aanze kuvuta musharraf ndo tutajua kama nae keshakata ringi

Hana menejiment yoyote ya maana

Amezungukwa na masharo wapiga mizinga new ideas atatoa wapi

Yeye aendelee kutoa nyimbo nzuri tuuu bila promo ndo atajua maana ya promo kwenye game!
 
Kama kutowapenda Clouds ni dhambi,acha nkachomwe moto tu
 
Hata zile tuzo alizochukua diamond kipind belle yuko kwenye ubora wake hakustahili ila fitna tu.........sumu ya penzi na masogange zilikuwa ni mwiba
 
Jana nilikuwa napiga story mbili tatu na mdau mmoja wa muziki kuhusu kifo cha Mangwea pia zinazoitwa tuzo za KILI...Ni mengi tuliongea, ila lililonifanya nije na hii post ni kuhusu msanii Belle 9, ni habari iliyonishtua kidogo nikaona si mbaya nikija kushare hapa ili ukweli ujulikane, na hata kama ni story za kupika basi iwe wazi!!

Takribani miaka kama minne iliyopita inasemekana Belle 9 alienda kuonana na uongozi wa Clouds katika kuomba support juu ya kipaji chake, ila cha kusikitisha Ruge pamoja na wenzake wakamwambia dogo hawezi kuimba.

Belle aliondoka na akaenda RocaTz Records na kwa mara ya kwanza akarekodi "Sumu ya Penzi", ngoma ambayo ilipenya masikioni mwa wengi...
Katika kuonesha kwamba hakubahatisha, Belle 9 alikuja na "Masogange" ngoma ambayo ilisumbua vilivyo hali ilipolekea Clouds kumwita tena na kutaka kufanya naye kazi!!! Kilichotokea ni kwamba dogo alikataa na aliwaambia kuwa walisema hawezi kuimba na leo imekuwaje tena...Belle 9 alizidi kupewa msimamo na Afande Sele wa kuendelea kuwatosa Ruge na wenzake...
Baada ya hili sakata, ndipo Ruge na wenzake wakaapa kummaliza kimuziki Belle 9..
Mikakati ikawa kuwabeba kwa nguvu zote wasanii walioonekana kuzidiwa au kuwa sawa na naye!!

Ndiyo maana ukiwaangalia wasanii kama Ben Pol na Diamond huwez sema wana uwezo kumzidi Belle 9 ila ndiyo wanaopata airtime ya kutosha na kupewa tuzo. Cha kushangaza Belle 9 hatokei hata kwenye category ya hizo tuzo zao.

Kama umeusikiliza wimbo unaoitwa "listen" ni takribani miezi mitatu toka utoke, lakini sasa upo kapuni!!

Kila mtu anajiuliza kulikoni, wengine wanasema hana nyota, ila kilichopo kwake ni huo mkakati ambao kwa mujibu wa wapangaji wake...wameapa kwamba Belle 9 hawezi kumaliza hata mwaka toka sasa katika huu muziki!!!

@@@******@@@@


mshauri atafute management ya ukweli kwa ajili ya promo, kwani kituo cha redio ni kimoja? kituo cha televisheni je? mm binafc sijaona mantiki
 
Back
Top Bottom