Tetesi: Nilichosikia kinaendelea CHADEMA kati ya Lissu na viongozi waandamizi wa Chama

KIBST

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2017
Posts
517
Reaction score
2,152
Naomba wale BAVICHA au BAWACHA wote mliomo humu JF mniambie hivi kwanini siku hizi Tundu Lissu amekuwa akitoa matamko bila kuandamana na viongozi waandamizi wa chama?

Pia naomba mniambie kwanini siku hizi Tundu Lissu anavaa viatu vya Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu kutoa matamko?bHawa wahusika wapo wapi?

Inasemekana kama kichwa cha habari kinavyojieleza kuna sintofahamu kubwa sana inayoendelea ndani ya CHADEMA kwa sasa kati ya Tundu Lissu na viongozi waandamizi wa chama wanamuona Lissu akitaka kukivuruga chama kwa matakwa yake binafsi ya kujinufaisha kuelekea 2020 ili hali kuna Lowassa mwenye hatimiliki ya kuwa mgombea pekee wa uraisi kupitia CHADEMA 2020.

Ndio maana tulizoeautaratibu wa hiki chama kila kinapotaka kutoa tamko siku zote kuna kujumuisha kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa chama kwenye hiyo press ya matamko ila tunachokiona sasa ni kupaniki kwa huyu jamaa baada ya kuona anatengwa na kusimangwa na kundi la Mbowe na Lowassa inafikia mpaka hatua ya kuanza kuropoka kwenye mambo wakati mwingne yana msingi lakini presentation yake inakua as if ni mtu ambaye ana msongo mkubwa sana wa mawazo na ambayo yanasababishwa na kuhisi kutengwa na chama.

Na hii inapelekea mpaka sasa wabunge walio wengi wapo majimboni mwao kipindi hiki ila yeye ndio kwanza yupo Dar kutetea watuhumiwa wa kutumia mihadarati na kutoa matamko yasiokuwa kuwa na kichwa wala mguu. Yeye badala ya kujenga chama anajenga jina lake.
 
Kwasasa hata Lisu mwenyewe hajijui anaongea kama nani!Maana matamko ya Chadema utamuona Mbowe, Mashinji, Lowasa na viongozi wengine wakuu!Lisu yeye anakurupuka na kuropoka ili akamatwe na polisi apate kiki

Hatuangalii mtoa tamko tunaangalia ukweli wa tamko. Hili la Lissu ni la ukweli, alitoe akiwa na viongozi au mwenyewe haipunguzi ukweli wa alichosema.
 
Kuna ule wimbo wa jamani sana unasema hivi.."Mapenzi hapana kificho yaingiapo moyoni mwako,mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayooooooo...."Mkuu unaonyesha jinai ulivyo na mapenzi ya dhati ya moto kabisa na Chadema.
 
Reactions: BAK
Haya tunasema kila siku na kila wakati. Chama kimepotea kinawayawaya kama puto.

Hilo andiko la Lissu tayari limekuwa tamko la chama wakati ni la msaka tonge fulani tu.
 
Yaani kwa hii post, hata ile posho yenu ya buku 7 pale mtaa wa Lumumba utaikosa leo!

Kwa kuwa hiyo propaganda yako ipo "so low" kiasi ambacho hata mtoto anayesoma chekechea atagundua tu kuwa unampiga fix.........
 
Hebu punguza jabza na uendelee kuucheza mziki wa Lissu kwa step.
 
Hahahahah Lissu endelea kuwa chezesha makirikiri piga bababaaa yanacheza babaaaa
 
Kwa hii press release ya comrade lissu ,Leo magogon chakula hakiendeki

Lzm atafutwe mchaw anaeshirikiana na TL

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Wewe kutokea huko ccm umejuaje kuwa anachosema hakina ridhaa ya chama? afterall yeye ni mkuu wa kitengo cha sharia na anayozungumzia ni masuala yahusuyo sharia tatizo liko wapi? umewahi kumsikia anazungumzia masuala ya utawala kama uongezaji wa matawi? au kuhama madiwani kwa kununuliwa? na mambo kama hayo maana ni ya KM au mwenyekiti.
Msituingilie pale anapowatwanga kisheria na mkatwangika, nyie jueni ya huko kwenu tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…