Kuna wakati michango yenu hamshirikishi akili wala hamtendi haki.
Zaidi mnajikosha muonekane mko matawi.
Maslay queen watatu mjini sehemu ya maana watatumia sio chini ya 30k kila mtu sawa na 90k plus bolt ya kutoka IFM to Tabata go and return kwasasa sio chini ya 40k.
Ukijumlisha na yeye mtoa out 30k=90+30k+40k=+160k na hapo hatujui huyu jamaa uwezo wake ukoje?.
Naelewa binti huenda alihofia usalama wake lakini alipaswa amtaarifu jamaa kuwa anakuja na rafiki yake angalau mmoja.
Wabongo tunajifanya matajiri kulisha kijiji ilhali wazungu wenyewe hawanyi ujinga huu.
1. Binti alipaswa kutoa taarifa.
2. Kijana
mdukuzi naye asingepaswa kuwatelekeza angemwita pembeni tu pale walipokuja kwenye bolt kabla ya kwenda walipopanga kwenda angalau wabadili location waende sehemu nafuu kidogo ili aweze kuafodi gharama.
Tuache ujinga huu wakulisha vijiji kwa sifa za kijinga hasa katika hatua zetu za awali katika utafutaji.
3. Mabinti elimikeni pia...toeni taarifa kabla hamjatoka ili mkubaliwe kuleta rafiki zenu au mkataliwe na out ifie juu kwa juu badala ya kuaibishana mbeleni:
NOTE: maslay queens ni zaidi ya kupe...mmoja ataagiza wine 2 za 25k@ na msosi wa 20k hapo ni 70k
Yaani hadi mwisho unaweza kujikuta 250k imekata bila kutarajia.