Nilichowafanya hawa mabinti wa IFM hawatanisahau

Nilichowafanya hawa mabinti wa IFM hawatanisahau

Mkuu niseme tu. Nakupongeza kwa maamuzi magumu ya kumwacha huyo bint ajifunze maana huwezi kualika mtu mmoja aje na kijiji.

Bora angekwambia kuwa atakuja na watu wengine nawe ungejipanga ila kitendo cha kuja na kijiji je kama ungemfuata na usafiri wako wa miguu miwili ingekuwaje kuhusu hao wenzakeee?

Wadada acheni utoto. Ukitolewa out nawe usijifanye kuwatoa mashoga zako out kwa mgongo wa mwingne
 
Mabinti wa vyuoni wengi sijui wanayaonaje maisha, nadhani wanajua maisha ni kitu rahisi tu coz wanakula, wanalala, wanahongwa na life linasonga. Jamaa kakosea kuwaachia kisanga, angemwita pembeni baada tu ya kukutana nao, date ikaishia pale pale, akalipia bolt warudi walipotoka.

Jioendekeze uonekane unazo, kesho unaamka huna hata jero ya kuendea jobu.
Mjinga hufunzwa kijinga na funzo lake huwa halisahau
 
Ujafikia umri wakufanya mapenzi first date unataka aje pekee anajuaje wewe kama ni mtu mwema unaushamba sana mtoto wa kiume unakuja kuadithia upuuzi hapa katika shamba la wanaume?? Wewe unaona kama umewakomoa yawezekana kuna mahali walipata changamoto kutokana na hilo ulilolifanya! Basi nikwambie KARMA NEVER SLEEP,KARMA IS BITCH KARMA WILL REVENGE IN OTHER WAY! Ndiyo ujumbe nakuachia.
Waje wawili basi
 
Eeeh bhana eeh!! Hii inanikumbusha mbali sana aisee, kuna manzi mmoja nilikuwa namfukuzia Muda Mwingi sana lakini sikuweza bahatika kukutana nae yaani outing kwan alikuwa anakataa kutoka!!

Mwamba sikukata tamaa niliendelea kumsumbua sana aisee, ikafika mwisho akakubali kutoka na Mimi hapo sina shida na Pesa kwani teyar Mwamba Mfuko unasoma na Boom la kutosha aisee kipindi icho tunatolea Pesa Pale Azikiwe Branch Posta!!

Muda ukafika kama saa Moja hiv jioni nikaita Uber nikamwambia aje karibia na Freemason area!! Eeh bhana eeh kuangalia yuko na Mtu 3 na yeye wa nne hiv!! Then kucheki nawaona wale wadada wa Kujirusha sana coz nawajua si unajua kichuochuo!!

Mwamba nikaona hii hali sio ya kawaida wakafika pale tukaingia kwa Uber sasa Akili ikanicheza sasa hapa tunaelekea wap kwa Hiki kikundi lakini mala ya kwanza Dereva nilimwambia anipeleke masaki coz mtoto ni mmoja najua !!

Mara paap masaki hiyo tukaenda sehem moja hilikuwa imechangamka sana na watoto wa kishua balaa tukafika pale!! Kila mtu anaagiza anajo Jua yaaani hapo akili haisomi kabisa najikuta kila kitu naitikia Yeah kwelii!!

Baada ya Muda nikamtumia message Yule manzi kwamba naomba nikatoe ela kwenye ATM si unajua sikujua kama unakuja na Ndugu zako!!

Faster mwamba nikatoka weeeeh! Nikaenda kwa Ndugu yangu Gongo la mboto na Simu nikazima!! Aisee siku nakutananae alinitukana sana
Safi sana hawa viumbe ukieaendekeza utaumbuka
 
Sasa umeandika nini unaleta mambo ya kisingeli kama ujajipanga na starehe acha kwani lazima??kulikuwa na sababu gani kuwatoa IFM hadi huko barakuda??Kwanini asiende viwanja vya masaki,kinndoni,sinza,goba mpaka awapeleke kinyerezi huo unabaki niushamba labda na wewe unateteni jamii hiyo hiyo yakpumbfu!
Unajua bei ya bia masaki,small planet haiko kinyerezi ni tabata bima,goba ni mbali sana
 
Utetezi kwa Bint kuwa alitaka kujihakikishia usalama bado una mapungufu! Huyo Bint alikuwa na nfs ya kuchagua sehemu ya mtoko anayoona ina usalama mkubwa kwake ikiwemo msaada kwa watu, angechagua hata kwenda kula kuku KFC
 
Weekend nilikutana na binti mmoja mrembo sana akasema anasoma IFM. Tukabadilishana namba, nikamwambia Jumapili jioni ajiandae nitamtoa out

Nikachukua bolt hadi Shaaban Robert Street chuoni kwa binti mida ya saa mbili. Cha kushangaza akaja na wenzake watatu wananukia kama majini.

Safari ikaanza mpaka small planet Tabata.

Wakaagiza savana, mi nikaita mtu wa jikoni wakaagiza kila mtu msosi aupendao na mimi nikaagiza. Tukaanza kula nikajifanya naongea na simu nikachukua bodaboda kitandani.

Asubuhi nikakuta matusi mengine mapya kabisa yaani sms za matusi zinapishana tu kwenye simu

Ofa nilikupa wewe Suraiya wewe unaniletea timu ya Twiga stars,

Kwanza sijui kama hao walikuwa binadamu au majini, binadamu wa kawaida amashindwa kumaliza samaki changu wa saizi ya kiganja?

Taifa limefika hapa
 
Kuna wakati michango yenu hamshirikishi akili wala hamtendi haki.

Zaidi mnajikosha muonekane mko matawi.
Maslay queen watatu mjini sehemu ya maana watatumia sio chini ya 30k kila mtu sawa na 90k plus bolt ya kutoka IFM to Tabata go and return kwasasa sio chini ya 40k.
Ukijumlisha na yeye mtoa out 30k=90+30k+40k=+160k na hapo hatujui huyu jamaa uwezo wake ukoje?.

Naelewa binti huenda alihofia usalama wake lakini alipaswa amtaarifu jamaa kuwa anakuja na rafiki yake angalau mmoja.

Wabongo tunajifanya matajiri kulisha kijiji ilhali wazungu wenyewe hawanyi ujinga huu.
1. Binti alipaswa kutoa taarifa.
2. Kijana mdukuzi naye asingepaswa kuwatelekeza angemwita pembeni tu pale walipokuja kwenye bolt kabla ya kwenda walipopanga kwenda angalau wabadili location waende sehemu nafuu kidogo ili aweze kuafodi gharama.

Tuache ujinga huu wakulisha vijiji kwa sifa za kijinga hasa katika hatua zetu za awali katika utafutaji.

3. Mabinti elimikeni pia...toeni taarifa kabla hamjatoka ili mkubaliwe kuleta rafiki zenu au mkataliwe na out ifie juu kwa juu badala ya kuaibishana mbeleni:

NOTE: maslay queens ni zaidi ya kupe...mmoja ataagiza wine 2 za 25k@ na msosi wa 20k hapo ni 70k
Yaani hadi mwisho unaweza kujikuta 250k imekata bila kutarajia.
Concurred....!

Tatizo wana JF huwa wananishangaza sana kwa kujimwambafai kuwa wana uwezo mkubwa sana na ni Matajiri

Ila wengine wanaset mitego hapa pia
 
Back
Top Bottom