Wengi sana walidanganywa kama wewe
Sent using
Jamii Forums mobile app
Hakudanganywa ila alifanya vibaya mitaihani ya a-level, pili hakuwa na taarifa sahii juu ya wapi atasomea urubani, na tatu ni uwezo mdogo wa kifedha wa familia yake.
Serikali haikuahidi itasomesha hao watu urubani miaka hiyo.
Yupo mtu wa karibu sana namimi ambae alimtangulia huyo mdau mwaka mmoja kumaliza shule alisoma hiyo PGM na sasa yupo level ya juu sana kwenye aviation industry.
Jamaa hawakuambiwa hivyo na serikali lakini waliambiwa possibilities za fani ambazo wanaweza kusomea kutokana na masomo ya PGM, yeye akachukulia literally wameahidiwa watasomea urubani, kibaya zaidi inaonekana alifanya vibaya mtihani wa kidato cha sita.
Hiyo anayofanya sasa nayo ni kazi, akijipanga anaweza kuwa tajiri na maarufu kuliko marubani, anaweza kutembea duniani kote kwa kazi ya Culinary arts kama kuwa culinarian (or chef), anaweza kufanya monesho na mafunzo duniani kote.
Ajifunze kukipenda anacho fanya sasa, maisha ni sasa , yaliyopita yamepita na yajayo hatuyajui ila tunaweza kujaribu kuyatabiri na kujiandaa nayo. Hakuna kuchelewa, Henry Ford alipata utajiri uzeeni.
Kwa kuanzia atunze kidogo kidogo huo mshahara wake kisha mwaka ujao aende akasome Bachelor Degree ya Culinary Arts chuo cha serikali nadhani bado kipo pale Mbagala.
Wapo watu ambao kazi yao ni upishi wana elimu ya kidato cha nne au elimu ya msingi tu lakini wanalipwa zaidi ya 2,500,000/- kwa mwezi na benefits zingine kama matibabu n.k.
Usiidharau kazi inayo kutunza hapa mjini na kuwapatia ridhiki familia yako. Unaweza kuwa rubani na ukasababisha ajali moja kubwa na usiaminiwe tena kwenye shirika lolote ukaishia kunywa chang'aa mitaani.