Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
Mwanzilishi Wa hotel za holiday inn duniani alikuwa mpishi,muhimu ndoto tu,pata uzoefu ukikusanya mtaji utafungua mgahawa wako ukiusimamia vizuri inakuwa hotel kubwa unapiga hela mara kumi ya rubani
 
Uliambiwa usome wewe ukacheza unafikiri nini? Lazima adhabu ya kutokusoma ikuandame. Ungalipata div one A physics, A maths ungeenda engineering tu. Angalia vyuo vya engineering vinavyohaha kutafuta wanafunzi. Rubani kwa taarifa yako ni dereva kama wa Passo ila yeye Passo yake inaruka angani.
Mbona kuna hadi div three wanasomea engineering?
 
Umedanganywa mangapi? Ukiwa Chalinze ukaoneshwa njia ya kwenda Dar, ila wewe ukaishia Kibaha, bado utakuwa ulidanganywa njia ya kwenda Dar au wewe utakuwa hujafika Dar? Kwani PGM ni urubani? Basi wote waliosoma PCB tuwaite madaktari na wafamasia na tuwaruhusu wakatibu.

Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
 
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
Ni kweli PGM wengi ni wahandisi na marubani
Hata mimi nimesoma PGM
 
Wewe uliambiwa usome na kufaulu vizuri ukaishia kunywa uji na kula ugali kwa maharage ukapata division 0, ukatumia cheti chako cha form four kwenda kusoma hotel management (probably certificate ) ukapata ajira kwa mhindi.

Sasa unalalamika nini, badala umshukuru huyo mhindi hata kakusaidia ajira ya ulichosomea, unaanza kulalama kwa uzembe wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli PGM wengi ni wahandisi na marubani
Hata mimi nimesoma PGM
Mkuu kuna sehemu umesema wewe ni Muhenga wa miaka 72,
kwa hapa JF ndiye unongoza kwani ulizaliwa 1948 wakati wa Vita vikuu vya pili
Masomo yaliyotolewa enzi hizo ni useremala na Uashi, labda Ualimu na askari (KAR)
JF haidanganywi km umesoma PGM ni mtoto wa 1979 - 1990
 
Impogo hawwz kuwa wa 90 mkuu! No!
 
Mkuu tatizo lako ni umaskini wa familia yenu.
Kwa kutumia cheti chako cha kidato cha nne tu ungeweza kusomea urubani kwa miaka uliyomaliza elimu hiyo.
Hata sasa unaeza kusomea urubani tatizo umri wako, vipo vyo kibao hata hapa bongo vinafundisha urubani kuanzia milioni kumi na kuendelea.
 
Wewe uliambiwa usome na kufaulu vizuri ukaishia kunywa uji na kula ugali kwa maharage ukapata division 0, ukatumia cheti chako cha form four kwenda kusoma hotel management (probably certificate ) ukapata ajira kwa mhindi.
Sasa unalalamika nini, badala umshukuru huyo mhindi hata kakusaidia ajira ya ulichosomea, unaanza kulalama kwa uzembe wako.
Ushauri mzuri sana,Mm naona angemuibia huyo Mhindi akajinunulia ndege yake
kuna jamaa aliitwa BOB SAMBEKE pale Moshi mjini alianza na njugu mpaka akawa tajiri akajinunulia kandege kake akaendesha mwenyewe
Kikamtupa na kumuua
Kwa hiyo ni malengo tu, aache kwa Muhindi akacheze Jackpot Bingo
lkn mawazo ya kurusha KLM ni ndoto
Natamani kurusha KLM
 
Wengi sana walidanganywa kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakudanganywa ila alifanya vibaya mitaihani ya a-level, pili hakuwa na taarifa sahii juu ya wapi atasomea urubani, na tatu ni uwezo mdogo wa kifedha wa familia yake.

Serikali haikuahidi itasomesha hao watu urubani miaka hiyo.
Yupo mtu wa karibu sana namimi ambae alimtangulia huyo mdau mwaka mmoja kumaliza shule alisoma hiyo PGM na sasa yupo level ya juu sana kwenye aviation industry.

Jamaa hawakuambiwa hivyo na serikali lakini waliambiwa possibilities za fani ambazo wanaweza kusomea kutokana na masomo ya PGM, yeye akachukulia literally wameahidiwa watasomea urubani, kibaya zaidi inaonekana alifanya vibaya mtihani wa kidato cha sita.

Hiyo anayofanya sasa nayo ni kazi, akijipanga anaweza kuwa tajiri na maarufu kuliko marubani, anaweza kutembea duniani kote kwa kazi ya Culinary arts kama kuwa culinarian (or chef), anaweza kufanya monesho na mafunzo duniani kote.

Ajifunze kukipenda anacho fanya sasa, maisha ni sasa , yaliyopita yamepita na yajayo hatuyajui ila tunaweza kujaribu kuyatabiri na kujiandaa nayo. Hakuna kuchelewa, Henry Ford alipata utajiri uzeeni.

Kwa kuanzia atunze kidogo kidogo huo mshahara wake kisha mwaka ujao aende akasome Bachelor Degree ya Culinary Arts chuo cha serikali nadhani bado kipo pale Mbagala.

Wapo watu ambao kazi yao ni upishi wana elimu ya kidato cha nne au elimu ya msingi tu lakini wanalipwa zaidi ya 2,500,000/- kwa mwezi na benefits zingine kama matibabu n.k.

Usiidharau kazi inayo kutunza hapa mjini na kuwapatia ridhiki familia yako. Unaweza kuwa rubani na ukasababisha ajali moja kubwa na usiaminiwe tena kwenye shirika lolote ukaishia kunywa chang'aa mitaani.
 
Back
Top Bottom