Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi


Ukweli nimezaliwa miaka ya 80
Lakini mimi siyo mtoto tayari nina 35 ni mtu mzima
 
Matokeo yako ndio yaliyoku judge kufika hapo ulipo
. Hizi nifikra zako lakini tunamini Mungu ndio hupanga maisha, Wengi wamesoma shule kubwa lakini siyo matajiri kama waliyo soma shule ndogo au kuna waliyo soma sciences lakini hawawafikii waliyo soma arts kwa mshahara.
 
Binafsi siamini kwenye hii biashara inayoitwa ELIMU! naamini sana kwenye kuheshimu ulichozaliwa nacho kichwani yaani talanta! Tatizo Nikwamba ulishatengenezwa mfumo wakuzuia wavumbuzi au genius people wengine kuja na ideas zitakazopindua hii biashara ELIMU!
 
Elimu ya bongo bwana haya yalishanitokea kipindi nasoma o level nilipanga nine kuwa doctor mpaka baiskeli niliyokuwa natumia kwenda shule niliandika dokta ----------- Ila sasa dunia ikanipangia baada ya kwenda advance mambo yakagoma nilifaulu masomo yote o level ila serikali ili nipangia kusoma hgl japo mi kwenye comb nilichagua PCB na nilifaulu vizuri kabisa tena vizuri kuliko hata hgl hiyo nikaenda advance kufika huko nikaomba kubadili comb wakagoma wakaniambia labda nihame shule familia yangu ilikuwa na uwezo mdogo wakashindwa kunihamisha nikapiga advance nikamaliza nilipomaliza nikawa na ndoto nyingine ya kuwa mwanajeshi baada ya udaktari kugoma nikaenda jkt nikapiga jaramba kufupisha mstori ni kuwa ndoto zangu zote ziligoma hapa nilipo napigika tu kitaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S
Sio kutokuwa serious mkuu, masomo ya science ni magumu wengi wanakuwa serious lakini wanafeli hasa kwa miaka ya nyuma hasa shule za serikali , hiyo pgm imewaumiza wengi wa mkwawa, Mazengo , sengerema , tambaza , afadhali tambaza tution za dsm zilisaidia watu kufaulu
 
Mwaka gani?
 
Lakini jamani tuwe wakweli, hivi ni nani unamfahamu wewe binafsi aliyesomea PGM leo amekuwa rubani?
Mimi mpaka sasa naona ni ndoto za kufikirika sana kuamini kusomea PGM kutakufikisha kuwa rubani.
Maana wote niliwahi kuwaona wakisoma PGM wameishia kwenye fani zingine tofauti kabisa.
 
Miaka hiyo

Ya 2001 kurudi nyuma , watu wengine wamefaulu kwa kusoma Sana tution ukitegemea shule umeliwa
Usidanganye kuanzia mwanzo hadi miaka ya 90 tuitions hazikuwepo, watu tulikuwa serious darasani na kujisomea wenyewe na tulisoma PCM na PCB tukafaulu. Shule haihitaji akili nyingi bali kujituma na kujua kuwa unajisomea kwa faida yako si kumsomea mama yako au baba yako. Imani yangu na hata nilipokuwa shule ni mchana mwalimu anafundisha darasani na usiku ni kujisomea. Ati mwanafunzi anasoma hadi saa 3 usiku na saa nne usiku anakoroma kitandani hadi asubuhi unakuta amejikojolea usingizini! Hapo soma HGL au HKF au archeology
 
Mkuu ungejikita kwenye Sayansi Kimu,Sasa ungekuwa unatumia elimu yako
 
Tatizo ulisoma ukitegemea ajira ukasahau kuwa tunasoma kuongeza maarifa na namna gani tupambane na maisha na ndiyo maana baada ya kuukosa urubani umeishia kuwa mpishi pole sana kuwa mwalimu mzuri kwa wanao nao wanaposoma wasitegemee ajira ya serikali bali kujitegemea na kujipambania wao tofauti na hapo utaandaa ukoo wa wapishi
Ni kweli PGM wengi ni wahandisi na marubani
Hata mimi nimesoma PGM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sekondari wakati huo wengine tushaingia university
Ok sikuwa nimekuelewa, nilidhani unauliza Mazengo wakitoa PGM ilikuwa mwaka gani
maana leo Mazengo haipo ipo St John wengi wa leo hawakuikuta
sorry
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…