Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Nilidanganywa kusoma PGM nitakuwa rubani, leo hii mpishi kwa Mhindi

Changamoto ni ada ya mafunzo tu, elimu ya kidato cha nne ingekutosha kusoma hiyo fani
 
Pole sana. Nadhani umaskini ndio ulizima ndoto zako. Kusoma na kuhitimu kozi ya urubani ada si chini ya shilingi milioni 150. Sipati picha wakati unasoma 'A' level jinsi ulivyokuwa unajimwambafai (rubani mtarajiwa) mbele ya wadada wa Maghembe East kumbe ni mpishi mtarajiwa. Life is not fair wallah!
Umenikumbusha life ya Mkwawa: Mama Uswege, Makongoro West/East, Lumumba West/East, Shabani Robert West/East.
Nilisoma hapo enzi za utawala wa awamu ya kwanza wa nchi hii enzi hizo ni wewe mwenyewe utakavyo pasua paper unakwenda chuo kikuu
 
Uliambiwa usome wewe ukacheza unafikiri nini? Lazima adhabu ya kutokusoma ikuandame. Ungalipata div one A physics, A maths ungeenda engineering tu. Angalia vyuo vya engineering vinavyohaha kutafuta wanafunzi. Rubani kwa taarifa yako ni dereva kama wa Passo ila yeye Passo yake inaruka angani.
Heh!
 
Mbona umepata moja ya kazi maridadi kabisa duniani yaani wewe huwezi kulala njaa hata usipolipwa mshahara. Hizo Ndege utaendesha kwenye playstation sio mbaya mkuu.
Very fun!
Tena anapikia kwa 'wazito '. Kuna waliosoma, wakafaulu hizo PGM, na sasa wanahudumia migahawa ya makuti, kwa nje imeandikwa Sheraton Hotel
 
Wakati nasoma A-level, Mkwawa High School (1999-2001) ulipita uvumi kuwa tunaosoma PGM tunaandaliwa kuwa marubani lakini leo hii ninafanya kibarua kama mpishi kwa Mhindi Masaki. Kwa mshahara wa 250,000/= kwa mwezi

Aisee elimu hii ovyo sana.
View attachment 1274044
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila wasomi wengi wananipa raha, hasa hawa fresh graduate wa kipindi hiki cha STONE aka ngumi jiwe


Yaan unamkuta mfano kaja ofisini kuomba kazi, cv zake sasa eti kamaliza la saba anaomba kufagia na kunyeshea maua, hapo hapo full kujifanya mshamba hajui hata neno moja la kiingereza usije kumshtukia[emoji1787][emoji28]

Badae wenzake waliosoma nae wanamchoma kuwa huyo mbona B.C.S

Kiufupi sio rahisi kuwagundua hawa special case
 
Kweli PGM imejua kunifurahisha. Mimi Leo ndo wa kumpigia Mhindi?
 

Attachments

  • 1214208_xsa.jpg
    1214208_xsa.jpg
    38.5 KB · Views: 6
Kama ulifaulu vizuri, kuna siku utaacha urubani wa jiko na kuwa rubani wa ndege. Usikate tamaa, wengi waliofanikiwa kitaaluma wamepitia mambo mengi.
Ipo siku? Raia aliyekuwa advance 1999 ukimwambia ipo siku labda kaburini
 
Kupitia upishi huo huo unaeza kutengeneza visheti vya ndege,ukachukua sahani ile yenye umbo la samaki kama uwanja ndoto inakuwa imetimia.
 
Mwanangu mimi nimemaliza form six mwaka 1983.Habari za kudanganyana kuwa ukisoma PGM unakuwa rubani ilikuwa toka Enzi zetu.Ukweli ni kwamba watu walikuwa hawajui ili uwe rubani lazima uwe rubani wa serikali na je serikali ilikuwa na ndege ngapi?Kudanganyana huku kulipelekea wanafunzi wanaosoma PGM hata ukipata A zote huwezi ingia chuo kikuu cha DSM kwa sababu ili usome engineering lazima uwe na chemistry ambayo hawakuwa nayo matokeo yake walikuwa wanaishia kusoma chuo cha Aridhi japo sio vibaya ila je kilikuwa kinachukua wangapi?
Hata hivyo ni kutokujua tu na uwezo unaweza jisomesha hata sasa urubani wewe mwenyewe kwa hela yako shule ziko nyingi hata za hapo dar tatizo ngarama ni kubwa mno wanakaa angani kwa masaa kwa ufupi urubani ngazi ndogo ya kuanzia gharama yake sio chini ya shs80,000,000
Kuna kijana mmoja nilisoma naye A level namuhifadhi jina alikuwa hata madaftari yake yote juu ameandika air TANZANIA alikuwa anapenda sana urubani na kweli akaenda kusoma PGM kule akapata division one akaenda kusomea urubani akaanzia Addis Ababa kisha Soroti Uganda.Ila je nani alimpeleka huko jibu ni kwamba baba yake alikuwa na uwezo sana hivyo alisomeshwa kwa hela ya baba yake jamaa flani mchaga.Ni rubani hadi sasa.
USHAURI:-Urubani hauna tofauti na udereva wa lori tofauti ni kuwa wenyewe unafanya mitihani migumu na lazima ufaulu na unahitaji akili iliyotulia.Tukija kwenye maisha wewe unaweza kuwa na maisha mazuri na upishi wako kuliko huyo rubani huyu jamaa yangu mimi sikusomea urubani lakini kwa muonekano hana maisha mabaya ila maisha yake ni ya ki standard ya kawaida kama yangu alichonizidi tu ni kwamba mwenzangu tunaweza kunywa naye banana usiku kesho yake anaenda kazini tukikutana ananimbia leo nimefika Kigali,Bujumbura,Nairobi Lusaka na Zanzibar.
Hiyo kazi unayofanya inaweza kuwa bora kuliko urubani afterall urubani ni kazi ya risk mno nilivokuwa mtoto nilikuwa na ndoto hizo ila kwa sasa sitaki hata kusikia hasa nikikumbuka kifo cha rubani mmoja kijana mdogo mtoto wa dada yangu wale waliofia Mbuga za wanyama.
Urubani hauna deal siku hizi hata wenyewe kwa sasa kuna mahali wanakosaga kazi inabidi waendeshe ndege za kiraia
Nina kijana wangu anafanya kazi mgodini elimu yake ni ya kawaida mshahara wake utakuwa mkubwa kuliko wa rubani.
Upishi ni moja ya kazi very rare kwa taarifa yako pengine labda ungefikiria tu kubadili sasa uwe unajifunza vyakula vya kizungu maana wenzetu wahindi wana tatizo moja hawana sera ya kumwendeleza mtu sana sana akiona unapata kitambi anaingiwa na wasiwasi unamuibia.
Mungu ametuumba tufanye kazi zinazotofautiana heshimu chako usiangalie cha mwingine ambacho hukiwezi ukiishi kwa hali hii utaishi kwa raha sana
 
Back
Top Bottom