Hivi majuzi nilibahatika kufika Ngorongoro National Park eneo la Crater; nikitarajia kuona wanyama wakubwa kwa ufasaha kama inavyosimuliwa kwenye movie mbalimbali za wanyama.
Niseme kwa dhati kabisa baada ya kuzungushwa muda mrefu niliambulia kuona nyati, kiboko, digidigi, punda na ndege flamingo. Lakini Tembo nilioneshwa miguu tu walipokanyaga sikuwaona, Simba nao nilioneshwa kwa mbaali sana tena wawili tu wadogo kama mbwa, nikaoneshwa kichaka cha Faru wanamopenda kukaa lakini sikuona!
Kiufupi roho yangu haikuridhika kabisa bora ningeangalia movie tu!
Matarajio yangu nilidhani nitaona Faru, chui, twiga, Tembo na wanyama wengine kirahisi kumbe sio kazi rahisi kama nilivyotarajia.
Nifanyeje Next time ili niwaone wanyama kiufasaha kama tusimiliwavyo?